Mnyika Kwishney, awasilisha ushahidi mwepesi na kwa sasa asubiri huruma ya spika tu

Kuna kitu sikielewi hapa, ni kwa vipi Mnyika alipomshutumu Mwigulu akaambiwa alete ushihidi, lakini Manyanya alipoishutumu CHADEMA kwamba inaengineer mgomo, hata pale CHADEMA walipoomba alilete ushahidi mwenyekiti alijikausha. Inakuwaje hii? Tuzuke bungeni na malungu nini?
 
Mnyika anapaswa kuacha jazba na uropokaji ili awe mwanasiasa mzuri huko tuendako.kama ataendelea kutoa shutuma hewa atajishushia heshma alojijengea kwny jamii. Atumie akili badala ya kile kiungo kingine anapofikiri.

Kwa jinsi unavyoporomosha upuuzi nina imani unatumia kiungo chenye matumizi tofauti
 
Jana trh 10.07.2012 kwenye mida ya saa 11.10 jioni, Mh. Mnyika aliwasilisha ushahidi wa utetezi wake wa kuthibitisha uhusikaji wa Mh. Mwigulu Mchemba na kashfa ya EPA. Kwenye dodosa zangu na wahusika wa ofisi ya katibu wa Bunge, walinihabarisha kuwa mambo yaliyoandikwa na Mnyika ni too general , ambayo ni yale yale yanayosemwa magazetini, mitandaoni, na ushahidi wake mkubwa ni ripoti ya BOT kuhusiana na sakata la EPA. Kwa minajili hiyo basi, ushahidi wa Mnyika wa kumuhusisha Mh. Mwigulu moja kwa moja na ushiriki wake kwenye EPA waonyesha haupo, na hili ndilo lilikuwa agizo la Mh. Mhagama ambalo alilo toa kuwa Mnyika aonyeshe ushiriki wa Mwigulu Mchemba personally na kashfa ya EPA na sio ushahidi wa BOT kwa ujumla wake.
My take: Kwa hali hii ni wazi kabisa Mh. Mnyika amejiabisha yeye mwenyewe, amewaibisha wananchi wa ubungo, amewaibisha vijana, amewaibisha CDM, amewaibisha wabunge vijana nk kwa kutokuwa na hoja zenye mashiko na zisizo kweli na uhakika. Kwa sasa anategemea huruma ya spika tu kwenye jambo hili.
Subiri tuuone kwanza, umeshajionyesha kwamba umeegemea upande gani.
Hizo dodosa kwa lugha nyingine ni umbea toka maafisa wa bunge, halafu ndio umeshafanyia conclusion!?
 
Umbeya tu unakusumbua.....
Una haraka gani?
Na huyo mfanyakazi wa Bunge awajibishwe kwa kutoa Siri.
Tunamsubiri Spika.
 
Kuna kitu sikielewi hapa, ni kwa vipi Mnyika alipomshutumu Mwigulu akaambiwa alete ushihidi, lakini Manyanya alipoishutumu CHADEMA kwamba inaengineer mgomo, hata pale CHADEMA walipoomba alilete ushahidi mwenyekiti alijikausha. Inakuwaje hii? Tuzuke bungeni na malungu nini?
Kwa sababu tuhuma za mnyika zilijulikana hapo hapo kuwa za uongo lakini suala la mgomo wala halihitaji ushahidi. Ni kweli CDM wako nyuma ya mgomo.
 
unachekesha kweli,hivi kwa nini mnapenda sana kuropoka ropoka,samahani unatumia kiungo gani kufikiri.au bilicanas imewaharibu ubongo mmebakia na mzigo wa kichwa usio na kitu ndani.
Trilion tatu SA, Billion 300/= Swiss Banks, RICHMOND, KAGODA, EPA, MEREMETA vyote hivyo ni kuropoka tuuuuuu, nadhani unaishi ulaya sio TANZANIA TUISHIO SOTE!!!

Kwa sababu tuhuma za mnyika zilijulikana hapo hapo kuwa za uongo lakini suala la mgomo wala halihitaji ushahidi. Ni kweli CDM wako nyuma ya mgomo.
mkuu hapa si unatumia jina la bandia, weka basi hapa ushahidi wa tuhuma zako dhidi ya chadema
 
My take: Kwa hali hii ni wazi kabisa Mh. Mnyika amejiabisha yeye mwenyewe, amewaibisha wananchi wa ubungo, amewaibisha vijana, amewaibisha CDM, amewaibisha wabunge vijana nk kwa kutokuwa na hoja zenye mashiko na zisizo kweli na uhakika. Kwa sasa anategemea huruma ya spika tu kwenye jambo hili.
Kwa nini umehitimisha mapema hivo? Si usubiri uone? Wenzio mbona bado tunasubiri ya Lema na Zitto. Si nao walipeleka uthibitisho? Ukitolewa hadharani tutaweza kujua wamemuaibisha nani. Tusubiri.
 
Subiri wajichanganye wenyewe uone moto wake!! I am sure hata kama Mnyika angesema tu Mwigulu Nchemba alikuwa mchumi BOT wakata wa fedha hizo zinafanyiwa uharamia akaweka nukta, magamba yasingefanya chochote.
 
Hivi Mnyika amejiaibisha kwa lipi?
Kwa uzuri gani alio nao Mwigulu Nchemba mpaka wana Ubungo wamsuse Mnyika?
Hivi mambo yote aliyotetea Mnyika toka aingie Bungeni yafutwe na kauli hiyo, ambapo nayo bado one way or the other iko correct!
Mleta mada ni MwanaMagamba na huenda unaishi Mabwepande!
Achana nae huyo, anaumwa ugonjwa wa mwiguluni.
 
Mie ninaishi Sinza D karibu na Vatican part of Ubungo jimbo la Myika hatujapata maji mwaka sasa, myika ashughulikie matizo ya jimbo lake, mpaka juzi mbunge mwigine kamzodoa kwamba huku hakuna maji. all we want is water, sijamsikia akifanya chochote juu ya hilo. wabunge wengine wamejikita kwenye majimbo yao yeye kigeugeu.
 
Kwani vile vielelezo vyote vinavyotolewa bungeni tangu bibi kiroboto achukue usukani vilisha somwa??
ripoti ngapi anawaambia wabunge wa upinzani wathibitishe kwa maandishi halafu havisemwi hadharani??
kabla hajaisoma hiyo ya mnyika aanze zile za nyuma zilizotangulia kila moja kwa utaratibu wa upokeaje hadi aje aifikie hii ya mnyika nadhani uchaguzi mkuu utakuwa umefika...
:popcorn:huku nikisubiria sinema ya bikiroboto na ripoti ya mnyika ianze

Asante mdau kwa hili.
 
Huyo Jamaa yako, a.k.a Gamba mwenzio amekwambiaje kuhusu Ushahidi wa Lema? Na kuhusu ushahidi wa Zitto amekwambiaje? Amekwambia ni kwanini mpaka leo shahidi hizo hazisomwi!

Mkuu Muongezee na hili;

--KAGODA = CCM
--CCM ilichota 40Billion za EPA
--Mwenyekiti aliomba wezi warudishe fedha za EPA!
--Mpaka leo hatujasikia kuwa fedha za EPA kutoka CCM zimerejeshwa!!!
--NCHEMBA NI MWEKA HAZINA WA FEDHA za EPA...
.; MWIGULU NCHEMBA ANAHUSIKA 100% kwenye kashfa ya EPA kwakuwa ni MWEKA HAZINA wa FEDHA ZILIZOTOKANA NA WIZI WA EPA...
 
Mie ninaishi Sinza D karibu na Vatican part of Ubungo jimbo la Myika hatujapata maji mwaka sasa, myika ashughulikie matizo ya jimbo lake, mpaka juzi mbunge mwigine kamzodoa kwamba huku hakuna maji. all we want is water, sijamsikia akifanya chochote juu ya hilo. wabunge wengine wamejikita kwenye majimbo yao yeye kigeugeu.

Mnyika yuko busy na miongozo, unadhani anawakumbuka wana ubungo?????

Mnyika toka alipojitukana mwenyewe nimemweweka kwenye kundi la waropokaji...Badala angejikita kutatua kero za wana Ubungo hawana maji ya uhakika, barabara nyingi za barabara kuu ni mbovu zinapitika kwa taabu isiyoelezeka, mabomba ya umma karibu yote hayatoi maji ndoo moja ya maji 2,000 wasaidie wana ubungo sio kila kukicha muongozo spika.
 
Mkuu Muongezee na hili;

--KAGODA = CCM
--CCM ilichota 40Billion za EPA
--Mwenyekiti aliomba wezi warudishe fedha za EPA!
--Mpaka leo hatujasikia kuwa fedha za EPA kutoka CCM zimerejeshwa!!!
--NCHEMBA NI MWEKA HAZINA WA FEDHA za EPA...
.; MWIGULU NCHEMBA ANAHUSIKA 100% kwenye kashfa ya EPA kwakuwa ni MWEKA HAZINA wa FEDHA ZILIZOTOKANA NA WIZI WA EPA...

Majibu kama haya ndio aliyoyatoa Mnyika, na ndio tunasema majibu mepesiiiii, yeye aliambiwa atoe ushahidi directly unaomuhusu personally Mwigulu, huu ushahidi km wako ni wa kuunga unga , ndio nasema ni huruma tu ya spika ndio inayotarajiwa

Back
Top Bottom