Mnyika kinara bungeni

mpigauzi

JF-Expert Member
Jul 17, 2012
275
71
Mnyika kinara bungeni
MBUNGE wa Ubungo, John Mnyika (CHADEMA), kwa sasa ndiye anashikilia rekodi ya ukinara wa kuchangia mara nyingi bungeni, akifuatiwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto (CHADEMA) na Godfrey Zambi wa Mbozi Mashariki (CCM).

Kwa mujibu ya rekodi zalizomo kwenye mtandao wa Bunge, Mnyika ambaye ni kipindi chake cha kwanza bungeni, ameonekana kufanya vizuri zaidi sambamba na wabunge wenzake kadhaa wa CHADEMA.

Takwimu hizo hazijawahusisha mawaziri, manaibu wao, Spika, naibu wake, wenyeviti watatu wa Bunge, Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa vile nafasi zao zinawapa uwezekano mkubwa wa kuchangia hoja wakati wowote.
Wabunge kumi ambao wameshika nafasi za juu ni Mnyika akiwa amechangia (184), kuuliza maswali ya nyongeza (28) na msingi (7), akifuatiwa na Zitto (79), (25) na (8) wakati Zambi anashika nafasi ya tatu kwa (70), (26) na (9).

Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu anashika nafasi ya nne akiwa amechangia mara 93, maswali ya nyongeza 19 na yale ya msingi 7, akifuatiwa na Diana Chilolo wa Viti Maalumu (CCM) aliyechangia mara 61, maswali ya nyongeza 41 na msingi 9.

Nafasi ya sita inashikiliwa na Halima Mdee wa Kawe (CHADEMA) akiwa na rekodi ya 59, 15 na 6 akifuatiwa na Moses Machali wa Kasulu Mjini (NCCR-Mageuzi) mwenye michango 57, nyongeza 30 na maswali ya msingi 7.

Magdalena Sakaya wa Viti Maalumu (CUF) amejinyakulia nafasi ya nane akiwa na michango 52, maswali ya nyongeza 13 na ya msingi 4, huku Mbunge wa Kisarawe, Seleman Jafo (CCM) akifuatia kwa 51, 10 na 6.

Anayefunga dimba kwa kumi bora ni Ester Bulaya wa Viti Maalumu (CCM) mwenye michango 47, nyongeza 17 na maswali ya msingi 3, akiwa amefungana na Martha Mlata wa Viti Maalumu (CCM) mwenye rekodi ya michango 47, nyongeza 11 na maswali ya msingi 5.
Ni takriban miaka miwili tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu, ambapo vyama vya upinzani hususan CHADEMA, wabunge wake wameendelea kuonesha umahiri bungeni, kwani hata Bunge la tisa lililopita kwa mujibu wa utafiti wa shirika moja, Zitto na Dk. Willibrod Slaa akiwa mbunge wa Karatu wakati huo, walishika nafasi za juu.

Katika mtiririko huo wa takwimu hizo kwenye mtandao wa Bunge, wabunge wanaoonekana kuwa na alama ndogo wengi ni wale wa Viti Maalumu CCM na baadhi ya CUF.


Source: Tanzania Daima 20/8/12
 
Sasa mnyika anajenga barabara..we vipi bana .mbona huulizi kigoma kuwa dubai

Kigoma ikiwa Dubai itamsaidia nini Mnyika akija kuomba kura. Wakati anatuahidi kushughulikia kero ikiwemo hiyo bara bara alikuwa kalewa?
 
jaman wana pendelea je uyu gwij mbunge we2 mahiri mCHEMBA mwigulu?
 
Juzi mnyika katoa wazo ambalo hata Makinda alinyanyua mikono na Cheyo nae akadandia ikabidi waziri wa fedha nae akakubali.Wazo la kupitia bajeti za wizara,sekta kwanza kabla ya bajeti kuu ya serikali.Maana miaka yote inasomwa kwanza bajeti kuu kisha ndiyo wizara jambo ambalo mnyika alisema halina mamntiki kwa kuwa inakua wabunge wameshaipitisha kwa ushabiki,ikija bajeti ya wizara wabunge hao hao wanalalamika kuwa haitoshi
 
Ni habari njema, cha msingi wabunge wote waige mfano wa Mnyika, ya kwamba hoja hapa sio kuchangia mara nyingi, hoja ni kuchangia mara nyingi lakini hoja zenye mashiko. Na kwa kweli bila kuuma maneno Mnyika amefanikiwa kuwa na michango mingi tena zenye mashiko.Isije ikawa unachangia mara nyingi lakini unashusha *****.
 
Barabara za Kilungule ni dhoflihali! Bonyokwa hakuendeki, King'ong'o hakuna njia, Ubungo Kibangu shida!

Kimsingi jimbo la Ubungo kupewa mnyika kulikuwa ni kumdhoofisha kisiasa anake jimbo enzi ya keenja lilikuwa na shida lukuki. maji ndo kabisa bara bara usiseme hakuna hata moja so kutegemea Mnyika afanye kwa miaka 5 ni uongo, keenja alikaa miaka mingapi? maji yalikuwepo?

Kimara iko kabisa na ubungo maji msewe yote na golani wanatumia maji ya mto maboamba hayatoi maji. bora hata ujio wa mnyika ulileta na miradi ya tasaf maeneo ya kibwegere na kwembe barabara ndo mbovu hazipitiki lol!

Kwembe hakuna njia, bonyokwa king'ong'o, kibwegere ndio afadhali kidogo na makabe
 
kimsingi jimbo la ubungo kupewa mnyika kulikuwa ni kumdhoofisha kisiasa anake jimbo enzi ya keenja lilikuwa na shida lukuki. maji ndo kabisa bara bara usiseme hakuna hata moja so kutegemea mnyika afanye kwa miaka 5 ni uongo, keenja alikaa miaka mingapi? maji yalikuwepo? kimara iko kabisa na ubungo maji msewe yote na golani wanatumia maji ya mto maboamba hayatoi maji. bora hata ujio wa mnyika ulileta na miradi ya tasaf maeneo ya kibwegere na kwembe barabara ndo mbovu hazipitiki lol!kwembe hakuna njia, bonyokwa king'ong'o, kibwegere ndio afadhali kidogo na makabe

Anaonewa vipi wakati yeye kinara? Hivi vijisababu eti Keenja kakaa miaka mingapi ni vya kisengelema. Siku tukiwapa nchi CDM watakuja na majibu hayo hayo CCM imekaa miaka 50. Wakati anaomba kura Mnyika alisema ataondoa hizi kero na akirudi atapimwa kwa hilo sio idadi ya miongozo ya spika.
 
Anaonewa vipi wakati yeye kinara? Hivi vijisababu eti Keenja kakaa miaka mingapi ni vya kisengelema. Siku tukiwapa nchi CDM watakuja na majibu hayo hayo CCM imekaa miaka 50. Wakati anaomba kura Mnyika alisema ataondoa hizi kero na akirudi atapimwa kwa hilo sio idadi ya miongozo ya spika.

sasa kumbe watu mnapenda kuongopewa eeh! manake mimi ni miongoni mwa watu ambao niliwah kusema mnyika anataka kudumaa kisaisa kwa hli jimbo. na wakati nasema nilionekana niviroba lkn wachambuzi wa siasa walisema ni kweli.hatuwez kumtegemea amalize haya yote kwa mara mja ila kule alikofanya apewe hongera zake na siyo kuonekana kana kwamba hajatend kabisa.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom