Mnyika ashinda kesi dhidi yake; Hawa Nghumbi atakiwa kulipa gharama za kesi!

Mijitu mingine bwana nawahi mahakamani mtu kashapigwa chini safari hakuna posho wala mshahara
kudadeki kama zamani tuu full njaaa na ilemela tumekata rufaa nahbari zilizopo Hihness atapigwa chini
chezea cc
 
Kwa watanzania wanaopenda maendeleo ya taifa hili john ameonesha ana upeo mkubwa sana bungeni, kusingekuwepo siasa mbovu za kuangaria uchama kwa pamoja tumeona bungeni john aliomba miongozo mingi pia aliomba marekebisho kwenye miswada mbalimbali kuliko mbunge yeyote.
 
Mijitu mingine bwana nawahi mahakamani mtu kashapigwa chini safari hakuna posho wala mshahara
kudadeki kama zamani tuu full njaaa na ilemela tumekata rufaa nahbari zilizopo Hihness atapigwa chini
chezea cc

Ndoto nyingine very interesting maana zimekaa kitamthilia
 
Hali ya mambo ni nzuri watu hawana munkari kama ilivyotarajiwa hasa wale wa Chadema ndio wengi na wanaonyesha wana matumaini ya Ushindi,

Hukumui haijaanza kusomwa tunaelezwa itaanza mida ya saa 3 hivi,

Polisi kwa mida hii sio wengi sana kwa hesabu hawafiki 50. Kwa ujumla hali ni ya amani kabisa!

Tutawajuza hatua kwa hatua moja kwa moja toka ukumbini!

Updates:

- Basi aina ya coaster lililobeba mashabiki wa chadema ndio linaingia huku likishangiliwa na watu kwa alama ya vidole viwili alimaarufu Amani na Upendo!

- Naaaaam vijana wakazi (FFU) ndio wanaingia kwenye eneo la tukio wakiwa wamevalia kikazi yani kama Baghdad lakini wapo kwa usalama tu hakuna dalili ya vurugu yoyote hali ni yaamani tu!

- Kuna mabishano ya hapa na pale kati ya wananchi na wahudumu wa mahakama, watu wanalalamika kuwa mbona mda unakwenda na hawaruhusiwi kuingia mahakamani! Lakini wamefanikiwa kuwasihii na wananchi wametuliza munkali

- Tunaendelea kusubiri mda ufike tuanze kufuatilia kesi hii!

- Naaaaam tumeshaingia ukumbini tayari kuanza usikilizaji wa kesi hii uendelee! Tumeambiwa tuzime simu lakini MIMI sitazima mwanzo mwisho!

- Tunasubiri jaji aingie na jopo la mawakili wa pande zote wapo tayari!

UPDATES:
Kuna kichekesho kimejitokeza hapa, yani wakati wakuingia ukumbini kuna mbinu iliyotumika na mashabiki wa CDM kuwabana mlangoni wale wa Magamba na wakashindwa kupata siti kilichofuata ni afande kuwatoa nje, wakati wakitolewa nje kuna kuna mwanachadema mashuhuri akaingia ukumbini afande akataka kumuunganisha na wanachadema kutoka nje, unaambiwa ukumbi umelipuka na kusema huyo siti ipoo!

Naaaaaaaaaaam Mh Mnyika ndio anaingia ukumbini anashangiliwa kwa makofi na Pipooooooozi Pawaaaaaaaaaaaaaa!

Updates:
Wakili wa Mnyika ndugu Mbogolo ndio anaingia anasalimiana na mnyika waapiga picha wanaendelea kupiga picha!
Sasa kilichobaki ni kumsubiri jaji tu aingie ukumbini!

Updates:
Jambo la kufurahisha ktk kesi hii nikuwa Mh Mnyika na Hawa Ng'umbi wamekaa pamoja na wanapiga stori kweli, hata alipotokea afisa usalama akataka kuwatenganisha mnyika amemwambia haina tatizo watu pipoooooooooooz!

UPDATES:

M/Kiti wa CHADEMA na Kiongozi wa Upinzani Bungeni Mh Freeman Mbowe aka Sauti ya Zege ndio anaingia anashangiliwa ile mbaya pipooooooozi


UPDATES: Mpaka dakika hii saa nne kamili bado Jaji haja ingia ukumbini, tunaendelea kumsubiri!

UPDATES:
Naaaam jaji ameingia na hukumu inaanza rasmi,

sitosoma maoni ya wadau, nafuatilia tu update zako. kuwa makini sana kutupa update
 
Kwa watanzania wanaopenda maendeleo ya taifa hili john ameonesha ana upeo mkubwa sana bungeni, kusingekuwepo siasa mbovu za kuangaria uchama kwa pamoja tumeona bungeni john aliomba miongozo mingi pia aliomba marekebisho kwenye miswada mbalimbali kuliko mbunge yeyote.

Kwa hilo nampa big up John Mnyika
 
Tusubili uamuzi wa mahakama ingawaje hukumu wanaijua kabla ata kesi kuanza
 
ohhh thanks kwa updates na i hope to get more updates from you...pipoooooooz....poweeeer!!!
 
Duh hapo sasa. Hiyo lugha tutapata updates kweli. Kwa nini hasomi kwa kimatumbi? kwani kesi ilikuwa inaendeshwa kwa lugha gani?
 
kwamba idadi ya polisi si wengi sana hadi sasa ni ishara mbaya kwa CCM
 
Najivisha ushekhe Mnyika atashinda kesi hii na jimbo hilo kuendelea kubaki mikononi mwa magwanda, magamba labda mjaribu kuchumbia tena 2015.
 
Falsafa ya CCM anayefanya kazi asile asiyefanya kazi ale sasa hapa kwa CDM ni tofauti, hizi kesi ni za kutengenezwa(artificial) kwa makusudi fulani sasa hapa mnyika anaondoka
 
Back
Top Bottom