Mnawakumbuka watuma salamu maarufu redioni wa enzi hizo? Tujikumbushe kwa kuwataja...

Una umri gani?
Umewahi kuwasikia watu hawa?
1. Bokoman Mkongoman
2. Limonga Justin Limonga
3. Chidi chidi Chitenda
3. Wajadi Fundi
4. Mwalimu Mashaka Sabuni
5. Alafa Kapilima
6. Thomas Mushi Kimboka
Na Zakaria Ndemfoo wakiwa safarini kuelekea Mahuta Newala?
Binadamu Mashaka
 
sasa hivi tuna madereva bajaji na kina migebuka ... kuna hawa wakina ustaadh sabasaba wa rukwa yaani kila zama ina kiki zake
 
Una umri gani?
Umewahi kuwasikia watu hawa?
1. Bokoman Mkongoman
2. Limonga Justin Limonga
3. Chidi chidi Chitenda
3. Wajadi Fundi
4. Mwalimu Mashaka Sabuni
5. Alafa Kapilima
6. Thomas Mushi Kimboka
Na Zakaria Ndemfoo wakiwa safarini kuelekea Mahuta Newala?
Enzi hizo radio ni RTD pekee na watangazaji kama Malima Ndelema, Hendrick Michael Libuda, Edna Rajabu Ni. Vipindi Mchana mwema, wakati wa kazi, jioni njema, club raha leo nk.

Nilikua nikiishi Mwananyamala B kwa mama Zakaria Jirani na bar yake Lumpa Bar. Daaah umenikumbusha mbali sana!
 
Huyo Limonga na chidi chidi chitenda WaPo tegeta kule Dar hao wasambaa,, mmoja yupo kwenye maroli yetu ya mchanga ni fundi, ,,,na Rafiki yao mzee Litumbi wa mtaa wa msichoke, ,, kipindi iko 1997 Simu za kiganjani hamna kivile zaidi ya TTCL tu
Mhm labda ni watu tofauti!Limonga ninayemjua ni mtangazaji wa Uhuru fm.
 
Mbona wa mwanza hamuwataji


Mfano
Muhili obale

Pagija

Hangaya

Aaron Makulilo Dr

Beka wa Bengali

Sita tuma Kubanda

Basu basanga Basu

Emannuel Barnabas Masagida
 
Wale jamaa wa chabela camp wako wapi? Pia kuna mtangazaji wa RFA anaitwa Roy Mlaliki Maganga sijui yuko wapi huyu jamaa
 
Usimwache Papaa Osama kanda ya kati Dodoma.Pia ni dhambi kubwa kumsahau Ima kulaya na ndugu yake
Kama ni mbwembwe basi hakuna aliyewahi wafikia wazee wa niambriiiiieeee ...wazee wa koma koma sela sela nukta nuta

Story kidogo kuhusu hawa jamaa ni siku walipomchezee mtu mzima Charles Hilary akiwa redio one
Alipiga simu Muhiru Obare na kuweka kikorombwezo Niambriiiiiiieeeeee ,Charles Hilary akakasirika sana akamkandia kiaina na akaweka wazi kuwa hapendi hiyo tabia ya watu kutamka hivyo (Niambriiiieee!). Akapiga simu Mkaudi Mkaudo Tingisha naye akaweka vikorombwezo hivyo hivyo Charles akamkatia cm akachukia sana . Mtu wa tatu kupiga simu ni Ima Kulaya, akatuma salama kama kawaida ila mwisho akamwambia Charles ;

IMA KULAYA: Brother Charles eeh!
CHARLES HILARY: Ndio Ima kulaya
IMA KULAYA: Watu wengine sio wastaarabu kabisa
CHARLES HILARY: Kweli kabisa Ima kulaya,kwa nini wasiige watu wastaarabu kama wewe!
IMA KULAYA: Huwa nawachukia sana hawa jamaa wanaosema Niambriiiiiiiiiiiiiiiiieeeeeeiii
Charles Hilary alicheka sana mwenyewe kwani Imma naye alifanya yale yale ila kwa style nyingine kwani naye aliivuta zaidi kuzidi wale wa mwanzo. Tokea hapo ikabidi awe anawaacha wazee wa niambriiiieeee koma koma sela sela nukta nukta.

Mkasa mwingine ulikuwa ule wa kutuma salamu kwa zaidi ya watu 3, Charles Hilary aliwashindwa kabisa jamaa kwani kitendo cha kupokea simu tu, mtu kama Papaa Osama alikuwa ameshataja watu kama 6. Walikwa na swaga za aina yake

Charles Hilary : Karibu Papaa Osama ,tuma salaam
Papaa Osama : Charles Hilary! Nipo na Mwiri Obare,Mamka Mushi,Chesco Mzee wa Matunda wakusalimu sana.Chidi Chitenda anamuuguza Maalim Litumbi hivyo hatafika . Kaka Charles Natuma Salaam kwa watu watatu kama ifuatavyo moja Chivalavala akiwa pale kwa Makabureta Pili kwa David Bekham Onana na Mwisho kwa Mohamed Kiyai yai ambaye ametapeliwa saa na Baba Dula 1.
Charles Hilary : Haya bwana..!
Kuwadhibiti ilikuwa inashindikana kwani walikuwa wanaspeed kali sana hawa jamaa katika kutaja majina haswa Muhiri Obare na Limonga J. Limonga

cc ChescoMatunda
Walikua wa asound sana
 
Mbona wa mwanza hamuwataji


Mfano
Muhili obale

Pagija

Hangaya

Aaron Makulilo Dr

Beka wa Bengali

Sita tuma Kubanda

Basu basanga Basu

Emannuel Barnabas Masagida
Muhiri obare...utasikia Naaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaammmmmm
Dah jamaa alikuwa na pumzi...miaka ya 2002 kuja juu
 
Watangazaji Radio one wakati huo ni Misanya Bingi,Rehema Saleh ,Mr Dullah,Mikidadi Mahmoud,Abdallah Majura,Sos B,DjJd ,Bwana Nkwanga,Uncle J Nyaisanga,
 
Majogo ya shamba hayo,
Walizibahatisha za msimu , au za madili au utapeli nk. Mifereji imefungwaa kifo cha Mende.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom