Halafu sauti yake nyororo Sana.Umenikumbusha mbali mpaka nimemkumbuka Catherine Chomago mtangazaji matata wa RTD aliyependa nyimbo za Vata Mombasa Juju man wa Le Orchestra Lipua lipua!
Wajadi fundi wajadi binadam mashaka kutoka mahuta shimoni kipindi hicho mwaka 1996 rtd kipindi cha jambo na malima nderema kuanzia saa 1.20 asbhNamkumbuka fundi nani sijui
Hapo kwenye "Mghani" nadhani ni kipindi kile cha mashairi nilikuaa nakipenda saaana mtangazaji alikua Bwana Said NyokaDuu, umenikumbusha mbali,
Enzi hizo miaka ya mwanzo ya 90, nilikuwa na rafiki wa karibu, mtangazaji RTD, alinihadithia mambo mengi.
Siku hizo mshahara wa Mtangazaji RTD akianza kazi ilikuwa ni Shilingi,
3,660.65.
Kikombe cha chai ya maziwa canteen yao pale Pugu Rd. ilikuwa Sh. 20, chapati, 20, andazi 10, mayai mawili ya kukaanga 40. Kipande cha kuku wa kukaanga ni sh.60.
Hao mabingwa wa salamu, walikuwa kila ukisoma kadi yake, kuna mahali unapita, anakupiga na Sh. 100. ukimaliza kipindi cha salaam, ukishuka canteen, hiyo 100, unapata chai, chapati 2 na mayai mawili ya kukaanga, kipande cha kuku na soda juu.
Jioni ukipita maeneo fulani, sio vi offer vinafululuza, akina dada ndio usiseme, enzi hizo redio yenyewe ilikuwa moja.
Hawa mabingwa wa salamu, ndio walikuwa wakiongoza kumwaga hizo 100, wakifuatiwa na wanamuziki wanaotaka nyimbo zao zipigwe, hawa walikata fungu kubwa zaidi,
Enzi hizo, Mghanii wetu akiwa 'Mzee Athumani Khalfani' akilipwa Sh.100 kughani kipindi cha nusu saa.
Jameni watu wametoka mbali!. Wee acha tuu!.
Mungu awarehemu watangazaji wote waliotangulia, na walibakia mpaka sasa, wapewe pongezi nyingi, na hata wazuri waliochipukia na wanaoendelea kuchipukia pia pongezi, ukiondoa wale wachache wana vamia fani.
Chivalavala S. ChivalavalaKulikuwa na "mabingwa wa salamu" ambao walikuwa hawakosekani aidha kutuma salamu au kutumiwa salamu kwenye vipindi mbalimbali vya radio. Unayakumbuka majina yao?
Alianza kutuma salam anzia late 1960's/1970s...kwenye idhaa za kiswahili ziliokuwepo.Huyu alikua bingwa kweli kweliThobias Mnyani wa uhuru na msimbazi. Rashid nguruwe wa korogwe.Bingwa wa salam tanzania alikuwa Zakaria Ndemfoo,radio zote za kiswahili kuanzia germany,south africa nk lazima utamsikia- Aliwahi kusema asiposikia jina lake redioni hupungua nusu kilo