Mnakarabati nini kutumia bilioni 60 kwa shule za Ihungo na Nyakaho?

Gazeti la Mwananchi linazidi kupoteza mwelekeo. Kwenye hiyo taarifa wameanza kwa kusema shule mbili zitagharimu shs 60 bilioni. Katikati kwenye andiko wanasema shule moja itagharimu sus 30 milioni! Hivi Editor hakuona kama kuna utata na hizo figures?
 
Bukoba. Serikali imesema gharama za kujenga upya wa shule za sekondari za Ihungo na Nyakato ni Sh 60 bilioni hadi kukamilika kwa miundombinu yake ambayo itakayoruhusu wanafunzi kupata elimu kama kawaida.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu leo mjini Bukoba alipokuwa akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu hatua zilizochukuliwa na Serikali katika kukabiliana na athari zilizosababishwa na tetemeko la ardhi lililoukumba mkoa huo.

Katika kukamilisha ujenzi wa shule hizo, mkuu wa mkoa amesema kuwa hatua ya kuvunja wa majengo yote imeshaanza ambapo tayari Kampuni ya CHICO ya Wachina inaendelea na uvunjaji wa majengo yote ili kazi ya ujenzi uanze.

“Wataalam wote wa ujenzi kutoka idara mbalimbali za Serikali wanaendelea na uchambuzi yakinifu wa majengo mapya ya shule hizo utakaozingatia viwango vya ujenzi ambapo gharama za awali kwa tathmini iliyotolewa na wataalamu hao ni Sh 30 milioni kwa shule za Ihungo na Nyakato,” alisema Kijuu.

Uamuzi wa kuzijenga shule hizo upya zilizoharibiwa na tetemeko la ardhi, ulipelekea Serikali kuzifunga na kuwahamisha wanafunzi waliokuwa wanasomea katika shule za Sekondari Ihungo na Nyakato ili waweze kuendelea na masomo wakati shule zao zinajengwa upya.

Chanzo: Mwananchi

Jamani hii ni sawa kweli?
Yaani kutoka 30m mpaka 60 billion ni parefu, hata kama wali underestimate mwanzoni, bado hiyo figure mpya ni too much!
That is 30 billion per school!! Shule gani ishawai jengwa kwa kiasi hicho? Hata the best private schools in tz zenye kila aina ya amenities hazikujengwa kwa bei hiyo.
Wewe na Ufipa mmekadiria shilingi ngapi?
 
Kuna kitu hapa si bure. Naamini hapa hapa Jf tunao wakadiria majengo hebu waje watusaidie katika hili
Hata kama wapo huwezi kupinga kitu ambacho serikali imesha pitisha! labla uwapeleka mahakamani walio kadidiria hzo hela
 
Sielewi hiki kitu, yaani bilioni 60 zitumike kukarabati shule mbili za sekondari? Shule ngapi TZ zinaweza jengwa kwa bilioni 30 kila moja?

=======

Serikali imesema gharama za kujenga upya wa shule za sekondari za Ihungo na Nyakato ni Sh 60 bilioni hadi kukamilika kwa miundombinu yake ambayo itakayoruhusu wanafunzi kupata elimu kama kawaida.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu leo mjini Bukoba alipokuwa akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu hatua zilizochukuliwa na Serikali katika kukabiliana na athari zilizosababishwa na tetemeko la ardhi lililoukumba mkoa huo.

Katika kukamilisha ujenzi wa shule hizo, mkuu wa mkoa amesema kuwa hatua ya kuvunja wa majengo yote imeshaanza ambapo tayari Kampuni ya CHICO ya Wachina inaendelea na uvunjaji wa majengo yote ili kazi ya ujenzi uanze.

“Wataalam wote wa ujenzi kutoka idara mbalimbali za Serikali wanaendelea na uchambuzi yakinifu wa majengo mapya ya shule hizo utakaozingatia viwango vya ujenzi ambapo gharama za awali kwa tathmini iliyotolewa na wataalamu hao ni Sh 30 milioni kwa shule za Ihungo na Nyakato,” alisema Kijuu.

Uamuzi wa kuzijenga shule hizo upya zilizoharibiwa na tetemeko la ardhi, ulipelekea Serikali kuzifunga na kuwahamisha wanafunzi waliokuwa wanasomea katika shule za Sekondari Ihungo na Nyakato ili waweze kuendelea na masomo wakati shule zao zinajengwa upya.

Chanzo: Mwananchi
 
Mkuu, lakini si wafanya biashara wawili waliwahaidi Watanzania kwamba watazijenga upya! Kama wamefanya tathimini ya kuzijenga kwa gharama ya Billioni sitini sawa tu, lakini siyo wanakuja wajanja hapa wanaigeuzia kibao Serikali kwamba ndiyo ihusike kuzijenga.
 
Serikali ya Ujapan kupitia Balozi wake hapa nchini ilitangaza kutengeneza shule zote zilizokumbwa na kadhia hiyo
Kwani imekuwaje tena?
 
Back
Top Bottom