Mnakarabati nini kutumia bilioni 60 kwa shule za Ihungo na Nyakaho?

Keyboard Warrior

JF-Expert Member
Aug 5, 2014
985
2,884
Jamani hii ni sawa kweli?

Yaani kutoka 30m mpaka 60 billion ni parefu, hata kama wali underestimate mwanzoni, bado hiyo figure mpya ni too much.

That is 30 billion per school.Shule gani ishawai jengwa kwa kiasi hicho? Hata the best private schools in Tz zenye kila aina ya amenities hazikujengwa kwa bei hiyo.

================================

Bukoba. Serikali imesema gharama za kujenga upya wa shule za sekondari za Ihungo na Nyakato ni Sh 60 bilioni hadi kukamilika kwa miundombinu yake ambayo itakayoruhusu wanafunzi kupata elimu kama kawaida.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu leo mjini Bukoba alipokuwa akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu hatua zilizochukuliwa na Serikali katika kukabiliana na athari zilizosababishwa na tetemeko la ardhi lililoukumba mkoa huo.

Katika kukamilisha ujenzi wa shule hizo, mkuu wa mkoa amesema kuwa hatua ya kuvunja wa majengo yote imeshaanza ambapo tayari Kampuni ya CHICO ya Wachina inaendelea na uvunjaji wa majengo yote ili kazi ya ujenzi uanze.

“Wataalam wote wa ujenzi kutoka idara mbalimbali za Serikali wanaendelea na uchambuzi yakinifu wa majengo mapya ya shule hizo utakaozingatia viwango vya ujenzi ambapo gharama za awali kwa tathmini iliyotolewa na wataalamu hao ni Sh 30 milioni kwa shule za Ihungo na Nyakato,” alisema Kijuu.

Uamuzi wa kuzijenga shule hizo upya zilizoharibiwa na tetemeko la ardhi, ulipelekea Serikali kuzifunga na kuwahamisha wanafunzi waliokuwa wanasomea katika shule za Sekondari Ihungo na Nyakato ili waweze kuendelea na masomo wakati shule zao zinajengwa upya.

Chanzo: Mwananchi
 
Bil60……? Tunajenga trump tower au uchumi ?anyway kwani michango wamekusanya ngapi? Alafu kuna waliojitolea kuzijenga hizo shule
 
Ebu ngoja nichukue kalam, karatasi na kikokotozi.
Kisha nitarejea na mifano halisi
 
Bukoba. Serikali imesema gharama za kujenga upya wa shule za sekondari za Ihungo na Nyakato ni Sh 60 bilioni hadi kukamilika kwa miundombinu yake ambayo itakayoruhusu wanafunzi kupata elimu kama kawaida.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu leo mjini Bukoba alipokuwa akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu hatua zilizochukuliwa na Serikali katika kukabiliana na athari zilizosababishwa na tetemeko la ardhi lililoukumba mkoa huo.

Katika kukamilisha ujenzi wa shule hizo, mkuu wa mkoa amesema kuwa hatua ya kuvunja wa majengo yote imeshaanza ambapo tayari Kampuni ya CHICO ya Wachina inaendelea na uvunjaji wa majengo yote ili kazi ya ujenzi uanze.

“Wataalam wote wa ujenzi kutoka idara mbalimbali za Serikali wanaendelea na uchambuzi yakinifu wa majengo mapya ya shule hizo utakaozingatia viwango vya ujenzi ambapo gharama za awali kwa tathmini iliyotolewa na wataalamu hao ni Sh 30 milioni kwa shule za Ihungo na Nyakato,” alisema Kijuu.

Uamuzi wa kuzijenga shule hizo upya zilizoharibiwa na tetemeko la ardhi, ulipelekea Serikali kuzifunga na kuwahamisha wanafunzi waliokuwa wanasomea katika shule za Sekondari Ihungo na Nyakato ili waweze kuendelea na masomo wakati shule zao zinajengwa upya.

Chanzo: Mwananchi

Jamani hii ni sawa kweli?
Yaani kutoka 30m mpaka 60 billion ni parefu, hata kama wali underestimate mwanzoni, bado hiyo figure mpya ni too much!
That is 30 billion per school!! Shule gani ishawai jengwa kwa kiasi hicho? Hata the best private schools in tz zenye kila aina ya amenities hazikujengwa kwa bei hiyo.
Duu bilion 60 tushapigwa inakuwa na kiwanda ndani yake ama
 
Jumla ya majengo 20 yenye ghorofa nne kila moja pale Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na yatakapokamilika tarehe 31 Desemba, 2016 yatakuwa na uwezo wa kuchukua wanachuo 3,840
Haya yalielezwa na Mtendaji mkuu wa TBA ndugu Elias Mwakalinga kua TBA ikitumia wataalamu na Vijana wa Kitanzania itatumia Shilingi Bilioni 10 kukamilisha ujenzi huo.
Sasa iweje hapa kwa ujenzi wa shule hizi 2 zigharimu 60 Bilion..
 
Nimeiona hii taarifa muda kidogo nikasema mwandishi atakuwa amekosea maana haingii akilini kabisa!
Mimi nilipoiona hii taarifa hapa, nilijihisi hata bwii lote likiniyeyuka kichwani
Tanzania kwa sasa hivi inatumia Zimbwabe Dollar? au mimi ndiyo sielewi?

Naona sasa hivi kila hela inayotajwa na serikali lazma iwe kuanzia bilioni!

Kuna kitu hapa si bure. Naamini hapa hapa Jf tunao wakadiria majengo hebu waje watusaidie katika hili
 
Back
Top Bottom