Mnakarabati nini kutumia bilioni 60 kwa shule za Ihungo na Nyakaho?

Jamani hii ni sawa kweli?

Yaani kutoka 30m mpaka 60 billion ni parefu, hata kama wali underestimate mwanzoni, bado hiyo figure mpya ni too much.

That is 30 billion per school.Shule gani ishawai jengwa kwa kiasi hicho? Hata the best private schools in Tz zenye kila aina ya amenities hazikujengwa kwa bei hiyo.

================================

Bukoba. Serikali imesema gharama za kujenga upya wa shule za sekondari za Ihungo na Nyakato ni Sh 60 bilioni hadi kukamilika kwa miundombinu yake ambayo itakayoruhusu wanafunzi kupata elimu kama kawaida.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu leo mjini Bukoba alipokuwa akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu hatua zilizochukuliwa na Serikali katika kukabiliana na athari zilizosababishwa na tetemeko la ardhi lililoukumba mkoa huo.
I saw this coming the rest still loading.................

Katika kukamilisha ujenzi wa shule hizo, mkuu wa mkoa amesema kuwa hatua ya kuvunja wa majengo yote imeshaanza ambapo tayari Kampuni ya CHICO ya Wachina inaendelea na uvunjaji wa majengo yote ili kazi ya ujenzi uanze.

“Wataalam wote wa ujenzi kutoka idara mbalimbali za Serikali wanaendelea na uchambuzi yakinifu wa majengo mapya ya shule hizo utakaozingatia viwango vya ujenzi ambapo gharama za awali kwa tathmini iliyotolewa na wataalamu hao ni Sh 30 milioni kwa shule za Ihungo na Nyakato,” alisema Kijuu.

Uamuzi wa kuzijenga shule hizo upya zilizoharibiwa na tetemeko la ardhi, ulipelekea Serikali kuzifunga na kuwahamisha wanafunzi waliokuwa wanasomea katika shule za Sekondari Ihungo na Nyakato ili waweze kuendelea na masomo wakati shule zao zinajengwa upya.


Chanzo: Mwananchi
 
Ni sawa kabisa wajenge majengo ya kisasa na miundo mbinu bora yenye zana bora za kufundishia pamoja na maabara.

Bila shaka wewe unayepinga ni mchagga ingekuwa moshi ungeona sawa.
 
Kama zitajengwa upya zote mbili haziwezi kuzidi 15bil, hizo ni hesabu za kitaalam
 
Jumla ya majengo 20 yenye ghorofa nne kila moja pale Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na yatakapokamilika tarehe 31 Desemba, 2016 yatakuwa na uwezo wa kuchukua wanachuo 3,840
Haya yalielezwa na Mtendaji mkuu wa TBA ndugu Elias Mwakalinga kua TBA ikitumia wataalamu na Vijana wa Kitanzania itatumia Shilingi Bilioni 10 kukamilisha ujenzi huo.
Sasa iweje hapa kwa ujenzi wa shule hizi 2 zigharimu 60 Bilion..
Wahaya bhana wanapenda sifa...60 billion poleni sana kina nshomile
 
Hawa wameshaona watu wanachangia wameona pa kulia kufanyia ufisadi, ukisikia kufa kufaana
 
Kwa figure hiyo ya mwendokasi (bilioni 60) soon atatumbuliwa mtu we subiri maana...
 
Omba tu majengo yawe na thamani ya pesa tajwa,usijali wingi wa pesa,shule ni miundombinu kamanda
Mzee, kwa billioni 6 sawa. Lakini bilioni 60,hapana. Hayo ni matusi ya nguoni na kuudhalilisha umma.
Je na hao matajiri wa mafuta, sikuile ya harambee, waliahidi mbele ya Waziri mkuu kuzijenga upya shule mbili zilizoharibika kabisa.
Hivi ni shule zipi hizo kweli!

Sent from my itel it1507 using JamiiForums mobile app
 
Wewe ndio hujaelewa zinajengwa shele mbili mbili yani mbili hizo unazoziona hapo na mbili kama hizo hizo matumboni mwa viongozi wa serekali wanaosimamia na kuratibu zoezi hilo
Usisahau ni kama hizo hizo



Hapa kazi tu kaa kimya
 
Maafa Haya Watu Ndiyo Wanapiga Pesa Hadharani
Tazama Sasa Hivi Michango Inavyomwagika
Halafu Unaambiwa Secondary Mbili Zinajengwa Kwa Bei Hiyo Hapo Huhitaji CAG Ila Mahakama Itoe Hukumu
 
Serikali yake inapesa aise! Usishangae kabisa. Tukiambiwa tubadilishe chama japo awamu moja mnatoa povu kila tu.n.du. Tuingie barabarani, mnakuwa kama Kobe! Acheni wazitafune tu hakuna jinsi, hakuna namna.
 
Back
Top Bottom