Mnada wa Jezi Tano za Simba Sport Club umefanyika. Jezi ya Rais Samia yauzwa milioni 10

Shark

JF-Expert Member
Jan 25, 2010
29,462
29,163
Jezi ya Rais wa Heshima wa klabu, Mohamed Dewji 'Mo' imeuzwa Sh. 2,000,000 na Duka la Vifaa la Michezo la
1690837582211.png
Romario Sports katika mnada unaoendelea katika Ofisi za Azam TV ikiwa ni ahadi tuliyoitoa kabla ya kupelewa kilele cha Mlima Kilimanjaro Julai 21, 2023.

Jezi ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Mwinyi imeuzwa Tsh. 5,000,000 kwa Hasa Clearing and Forwarding katika mnada unaoendelea katika ofisi za Azam TV

Jezi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Philip Mpango imeuzwa kwa Sh. 3,000,000 kwa Sanda Omary 'Sandaland The Only One.

Jezi ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Kassim Majaliwa imeuzwa kwa Sh. 4,000,000 kwa S & Sons LTD.

Kibegi kilichokuwa na jezi zetu na kupelekwa juu ya kilele cha Mlima Kilimanjaro imeuzwa kwa Sh. 2,500,000 kwa Saleh Majapa

Jezi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan imeuzwa kwa Sh. 10,000,000 kwa Benki ya CRDB CRDB.

Kibegi kilichokuwa na jezi zetu na kupelekwa juu ya kilele cha Mlima Kilimanjaro imeuzwa kwa Sh. 2,500,000 kwa Saleh Majapa.
 
simba bana mnafraisha ngao ya jamii mkidundwa, mwamedi anaaanza vijembe mnaanza kutafutana.

wenzenu yanga wako bize kujifua nyie mnapiga kampeni za ccm.

hakuna waasisi ambao walipambania simba au soka la Tanzania?
 
Back
Top Bottom