Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,476
- 39,995
Mara baada ya tukio la Gongo la Mboto kutokea maelezo ya kwanza (kina Kova na wenzake) walianza kutuambia ni "ajali". Baadaye taarifa zilitoka kwamba siku tatu kabla yake ulifanyika ukaguzi na kuhakikisha maghala yale yako salama na hakukuwa na dalili lolote la tatizo. Hivyo, tunakabiliwa na maelezo yafuatayo:
a. Ukaguzi haukuwa makini ilivyotakiwa (yaani wa kubabaisha) - uzembe!
b. Ukaguzi haukufanyika kama ilivyotakiwa (wa kuharakisha) - uzembe
c. Ukaguzi ulifanyika kwa kiwango kinachotakiwa na hakukuwa na tatizo lolote - JWTZ linasafishwa
d. Mtu/Watu wa ndani ambao walikuwa wanajua hali ilivyo waliamua kusabotage maghala kwa sababu zao - ughaidi
e. Mtu/watu wa nje ambao wanajua uwepo wa hiyo ghala na waliamua kusabotage kwa kutumia silaha - ughaidi.
Ninajiuliza maswali hayo kwanza kutokana na upekee wa tukio lenyewe lakini vile vile tukiangalia hali ya kisaikolojia miaka hii michache ambapo tumeona wanajeshi wetu (Polisi na Jeshi, na hata magereza) wakipatwa na msongo wa mawazo kiasi cha kutumia silaha kujidhuru wao wenyewe. Pendekezo kuwa hili laweza kufanywa na mwanajeshi linakuwa ngumu hasa baada ya taarifa kuwa hakuna mwanajeshi aliyekufa (japo hawasemi hakuna aliyedhurika).
Hivyo, njia pekee ya kuwaaminisha wananchi kuwa tukio hili halikuwa ughaidi ni muhimu (kama ilivyoamuriwa) kuleta chombo cha nje na huru kuchunguza na kutoa taarifa. Haiwezekani na taarifa ya Gongo la Mboto kuwa kificho tena. Tunahitaji kujua kiilichotokea, tunastahili kujua kilichotokea.
Lakini katika upande wa kusababisha madhara makubwa kwa wananchi hili halina mjadala - ni uzembe uliokubuhu wa viongozi walioko madarakani. Naungana na wale wanaotaka Dr. Mwinyi ajiuzulu na pamoja naye Katibu Mkuu MoDNS Bw. Andrew Nyamuso???