Mlipuko ulisababishwa na kombora kutoka nje?

Dr.Mbura

Senior Member
Jun 30, 2009
193
122
Ni mara chache sana mimi kuchangia hapa JF ila nimesoma post zote za milipuko lakini sajaona post za kitu nilichokiona kabla ya milipuko.

MIMI naishi maeneo ya Segerea ni karibu sana na GOMS nilichokiona ambacho nakiita shambulizi ni kitu kama kimondo kutoka juu sana na kudondoka maeneo ya Goms baada ya hapo ndipo milipuko ilianza!
 
Inawezekana ulikona peke yako tu?
Kuna mtu ulimweleza kuwa ona kitu kinadondoka toka juu sana au ulikuwa peke yako.
Wikileaks watatupatia taarifa hata kama ni baada ya miaka 5
 
Du hii kali, ingawa pale tuna Rader kibao na za uwanja wa ndege sijui watasema, kwanihakuna watakaoficha huku wmefiwa na ndugu zao.
Nnachokukubalia tofauti na waandishi wa haari na viongozi wetu ile milipuko sio ya mabomu ila ni ya makombora na TNT maana Bomu huwezi lificha Dar karibu na watu.
Wataalamu watanisahihisha mm nimeona kwenye picha zao BM (Ballistic Missile) makombora ya mizinga, makombora ya vifaru lakini Bomu hasa lingechukua kilomita kadhaa na kweli makamnda wangewajiishwa.
Yale jamani ni makombora likigongwa pini nyuma linaondoka masafa yale yamepasuka kwa ajili ya joto la moto wa mwengine chanzo tunakisuiri. Mooja katuambia ni kimondo
 
Je ulisikia sauti kabla ya kuona kitu hicho ? kombora huwa halitokei juu sana ,nakumbuka yale yaliyotumwa Sudani tulikuwa tukiyaona hayakupita juu sana ,tomahawk cruise missile huwa zinaonekana zikipita kimo cha minazi ,nilikuwepo Sudani siku zile ,tuliziona ila hatukujua ni kitu gani, mpaka tuliposikia ,nilijua ni maroketi ya kivita lakini sijawahi kuiona hizo cruise missile,ndo ilikuwa mara ya mwanzo.
 
Lolote linaweza kusemwa lakini mimi naamini hile haikuwa ajali tu, ni kitu kilichopangwa.
 
Ni mara chache sana mimi kuchangia hapa JF ila nimesoma post zote za milipuko lakini sajaona post za kitu nilichokiona kabla ya milipuko. MIMI naishi maeneo ya segerea ni karibu sana na GOMS nilichokiona ambacho nakiita shambulizi ni kitu kama kimondo kutoka juu sana na kudondoka maeneo ya goms baada ya hapo ndipo milipuko ilianza

Ni bora huwa huchangii, kwa style hii wote tungeonekana ni wehu aiseeee !
 
Kwa upande mmoja nasadiki kile alichokisema mtoa hoja kabla ya mlipuko wa kwanza kuna kitu kilioneka hewani kwa muda,mimi nakaa tabata relini hapa magengeni watu walikuwa wanabishana kusema ndege wangine wakisema kimondo na baada kama ya dk.5-10 tulisikia mlipuko mkubwa na wengi walikimbilia uwanja wa ndege wakiamini ndege imeanguka.

Pendekezo:Baada ya kumshambulia mtoa hoja tupinge hoja yake na sio kumchambua yeye na kumtolea maneno ya kashfa hatutakuwa tofauti na bunge la mipasho,tuwe kweli thinkers.
 
Mtalaumu bure huyu mshikaji anasomaga hapa...abovetopsecret.com
ndo wana mambo hayo ya vimondo
 
Kwa upande mmoja nasadiki kile alichokisema mtoa hoja kabla ya mlipuko wa kwanza kuna kitu kilioneka hewani kwa muda,mimi nakaa tabata relini hapa magengeni watu walikuwa wanabishana kusema ndege wangine wakisema kimondo na baada kama ya dk.5-10 tulisikia mlipuko mkubwa na wengi walikimbilia uwanja wa ndege wakiamini ndege imeanguka.

Pendekezo:Baada ya kumshambulia mtoa hoja tupinge hoja yake na sio kumchambua yeye na kumtolea maneno ya kashfa hatutakuwa tofauti na bunge la mipasho,tuwe kweli thinkers.

unasadiki ...... hahaaaaa ...... lete vivid evidence bana
 
Inawezekana ulikona peke yako tu?
Kuna mtu ulimweleza kuwa ona kitu kinadondoka toka juu sana au ulikuwa peke yako.
Wikileaks watatupatia taarifa hata kama ni baada ya miaka 5

Ni kweli kabisa, sie tupo Ubungo Msewe na tulikiona hicho kitu ila kilikuwa na mkia tofauti na pia kiasi fulani ulikuwa siyo wa kawaida. Baada ya hapo tukaanza kusikia milio tukajua ni Radi, kama dkk 5 bdae ndio tukajua kuna mabomu yanalipuka.
Ila labda lilikuwa ni bomu la mwanzo mwanzo kulipuka, nahisi hivyo,cjui
 
asante kwa kutolea majibui mawazo yako mwenyewe....
 
Ni mara chache sana mimi kuchangia hapa JF ila nimesoma post zote za milipuko lakini sajaona post za kitu nilichokiona kabla ya milipuko. MIMI naishi maeneo ya segerea ni karibu sana na GOMS nilichokiona ambacho nakiita shambulizi ni kitu kama kimondo kutoka juu sana na kudondoka maeneo ya goms baada ya hapo ndipo milipuko ilianza

we can call it crap? so unamaanisha kambi ilivamiwa? na kina nani? rostam au lowassa au kenya au marekani au iran? au alqaeda? na kama ni hivyo rada wamenunua ya nini? pambo au?
 
Japo mnamvamia mwanzisha hoja nadhani ni kwakuwa kasema 'Ni mara chache yeye kuchangia JF' ila nikiri kuwa huyu si raia wa kwanza kutoa kauli hii...

Ni mtu wa nne nasikia anatoa kauli hii, wa kwanza si member wa JF na nadhani hata haijui JF, alinifahamisha kuwa aliona kitu kama kimondo kikionekana kuelekea maeneo ya Tabata (yeye yupo Ubungo) na baadae kikafuatiwa na mshindo mzito, dakika kama 10 baadae ndo akasikia kuwa kuna milipuko ya mabomu. Mwingine yupo Njia Panda ya Segerea, raia mwenye kuuza genge maeneo hayo alisema almost kitu kilekile.

Hii kitu si ya kupuuza, vyombo vyetu vya usalama vijaribu kuangalia kama kulikuwa na shambulizi toka nje, inawezekana sana japo wengi mnapinga...

Bull, acha kueneza udini kwenye sensitive issues kama hizi mkuu
 
then it could be a falling star (meteorite). Lakini what are the odds of that? Kitu kimeanguka kutoka angani na kwenda moja kwa moja kwenye ghala ya silaha. lakini all in all, its all plausible! Maana wakati zinaanguka huwa na moto na uwezo wa kuvunja nyumba moja kwa moja.
Angalia hii website inatoa incidents mbalimbali za meteorites zilizoangukia vitu:
Interesting meteorite falls
Please note...this is Harvard University Page. Ivyo ina credibility kubwa in itself. Unaweza pia ku-google cases za watu, nyumba na vingine kuwa hit na hizi meteorite. Sio kitu kipya kabisa. Inabidi serikali iongee na wana sayansi walio na vyombo vya ku-monitor anga.
 
Back
Top Bottom