Mlipuko huu wa Rooters za WIFI kwa kampuni za Simu ipi ni nzuri Kwa matumizi nyumbani?

Chief-Mkwawa Hebu nieleze kuhusu hivi vidubwana maana kuna jamaa anataka kuniuzia jinsi vinavyofanya kazi na ni vizuri kwa matumizi ya ofisi na nyumbani na vipi kuhusu ufanyaji kazi wake
IMG-20240217-WA0000.jpg

Nafkiri ni 4G microwave hio kabla ya 5G kuja zilitumika na Voda/Airtel na wengine.

Kama Eneo lako kuna 5G vyema ukakomaa upate 5G, ina faida zaidi kuliko 4G.
Na ufanyaji kazi wake ukoje..
Hiyo ya kuwekwa nje kama Ungo wa Starlinks
Na hiyo ya ndani...
Na kingine Hivi star links ni bei gani na malipo yake kwa mwz
 
Ufanyaji kazi ni mmoja, Microwave inasaidia kupunguza ping, 5G yenyewe by nature ina ping ndogo, uzuri wa 5G ni capacity hata kama mtakua wengi mtaani ngumu speed kudrop.

Starlink around 1.5m installation na kwa mwezi around 120,000 huku kwetu.
 
Kwa maeneo niliyopo Vigumu sana kwa 5G kushika
Starlink around 1.5m installation na kwa mwezi around 120,000 huku kwetu.
so Hapa Tz kuna wakala? na nikienda kununua Kenya (Maana naona wengi wanafanya hivyo) nalipaje k8furushi cha Mwezi
 
Hii mimi mwenyewe ndio naisikia hapa sijawahi ku experience changamoto hiyo.

Kuna miezi huwa napiga hadi terabyte mbili bila speed kushuka.

Na sometimes kwenye torrent napata download speed hadi ya 9MB per sec.

Hapa nimepiga 650GB na bado speed iko kasi ile ile.

View attachment 2910940
mkuu hicho ni kifurushi cha shi ngapi kwa mwezi.
 
Kwa matumizi karibia yote ya kawaida hauhitaji 5G so usitoe hela bila sababu, jaribu mwenyewe kwenye simu yako weka hotspot kisha weka mtandao HSDPA/HSPA+/4G uone kama spidi inakutosha. Labda kama unacheza realtime games kunaweza kukawa na umuhimu zaidi katika latency.
 
Kwa mitandao ya simu Airtel wapo friendly zaidi, Gharama ndogo za kujisajili ambayo ni laki 2, wanakupa router na powerbank incase umeme unakatika ama upo nje ya nyumba. Vifurushi vyao vinaanzia 70,000 kwa mwezi

Voda pia wapo vizuri ila wame target zaidi wafanyabiashara, usajili bure ila utahitaji ka kila mwezi kulipa, vifurushi vinaanzia 120,000

Tigo wao gharama ghali sana kujiunga 650,000 ila kwa mwezi ni 70,000

Angalia kwako mambo haya
1. Unapata 5G? Kama unapata ni mtandao upi?
2. Pima speed zote za 4G na 5G angalia mtandao upi unazidi speed husika unayotaka kununua...

Then chagua mtandao kutokana na quality ya mtandao ya eneo lako, u naweza toa hela nyingi ukaishia kupata speed mbovu.
Wiki hii nimenunua Voda ile router yenye masikio inayotunza chaji kidogo, maana zile nyingine kubwa hazitunzi chaji kabisa. Sio kweli kwamba ni bure, nimeilipia 145,000 na kwa mwezi 115,000 unlimited unapata 10mbps. Tatizo lake ni 50m coverage alafu nikiiweka ghorofani wa chini hawapati vizuri na nikiweka chini wa ghorofani hawapati vizuri.

Nataka kuchukua router yenye nguvu zaidi iwe kama 150m na iwe strong. Hakuna haja ya kuwa na router eti ikiwa sebuleni juu, uko mbele getini chini mtandao hamna.

Nichukue aina gani, au niwatafute TTCL wafunge fiber? Naogopa watakuwa wababaishaji, na Zuku wana tabia ya kuuza signal sijui zinaitwaje hizo. Kesi zao nimesizikia.
 
Hio ya Voda 115,000 ni unlimited ya zamani, ya 4G, ya sasa ni 120,000 na unapata 30mbps. Pia ni bure kuunga kama umetimiza masharti.

Hio wifi unaweza ukafanya mesh, tafuta router nyengine weka mahala, tumia ethernet kuziconect router ili upate signal zaidi.

Fiber ni bora zaidi, ila angalia coverage kwako, signal ya Zuku sijaelewa bado ina maanisha nini. Ttcl inataka moyo, kama una option nyengine achana nao.
 
Wifi haipiti vizuri katika cementi/concrete jaribu kuweka sehemu kama kwenye ngazi labda ili signal ifike kote pia unaweza kununua extender/booster/repeater hiki ni kifaa kinachokamata wifi na kuirusha na nguvu mpya sio nzuri kama wifi kila ghorofa ua mesh ila ni cheap na inatosha mara nyingi. So unaiweka somewhere btwn router na ghorofa ya pili.
Screenshot_20240221-173116_Firefox.jpg
 
Hio ya Voda 115,000 ni unlimited ya zamani, ya 4G, ya sasa ni 120,000 na unapata 30mbps. Pia ni bure kuunga kama umetimiza masharti.

Hio wifi unaweza ukafanya mesh, tafuta router nyengine weka mahala, tumia ethernet kuziconect router ili upate signal zaidi.

Fiber ni bora zaidi, ila angalia coverage kwako, signal ya Zuku sijaelewa bado ina maanisha nini. Ttcl inataka moyo, kama una option nyengine achana nao.
Masharti gani Vodacom wanataka kuunga hiyo 30mbps
 
Hii mimi mwenyewe ndio naisikia hapa sijawahi ku experience changamoto hiyo.

Kuna miezi huwa napiga hadi terabyte mbili bila speed kushuka.

Na sometimes kwenye torrent napata download speed hadi ya 9MB per sec.

Hapa nimepiga 650GB na bado speed iko kasi ile ile.

View attachment 2910940
Msaada mkuu namna ya kudownload movie kweny torrent natanguliza shukrani
 
Mimi natumia vodacom nyumbani ambayo ni ya 4G 20Mbps,na ofisini natumia airtel 5G ambayo ni 30Mbps..
Kiukweli zote zipo vizuri sana,ingawa nimeipenda Airtel kwakua ina powerbank umeme ukikata unaweza tumia mpka 7hrs bila kuzima.
 
Back
Top Bottom