Mliopo Dar es Salaam kuna kitu kinapita maeneo yenu angani

NI Satelite zinazoitwa star link za yule kijana wa South Africa( Elon) anayewekewa kauzibe na Nape Mnauye asirushe internet hadi kule kwa Mandonga kisa tu hajajenga ofisi yake hapo Tanzagiza.
 
Ni kama nyota zinazoongozana kwa mstari mnyoofu, zikiachana kwa nafasi ndogo, zinaonekana zikiwa mbili mbili zilizokaribiana zinaacha nafasi kidogo kisha zinafuata nyingine mbili na kuendelea,tazama picha chini,sijawahi kuona kitu cha namna hii maishani.View attachment 2917366
Isije kuwa Tumevamiwa na Intarahamwe.......wanasema they have no Means but Ways
 
Kuna kitu sijui naweza kusema ni nini, maana si ndege kwa muonekano wa taa ulivyokuwa mrefu, ila nimeshindwa kuelewa kwa sababu ya giza.

Kimetokea uelekeo wa Bagamoyo kwenda kigamboni, mliopo huko hadi mbagara mnaweza kutujuza au anayeweza kuelewa ni kitu cha aina gani.

Kwenye komenti No. #7 kuna picha mdau wa Arusha Capt Tamar aliwahi kupiga picha, vinatembea kwa mstari kama wale ndege weupe wanaoluka pamoja kwa mstari wakihama wanaopatikana dead lake njia ya Loliondo.

Nawasilisha.
Hizo ni constellation satellite za starlink Internet mkuuu
 
Hicho kilichoonekana kinajulikana kama kimondo kwa kiswahili. Ni kipande cha sayari kati ya sayari zilizopo kwenye mzunguko wa ki sola na hutokea mara nyingi kuingia katika anga ya Dunia na kutokana na mwendo kasi wake na msuguano wa hewa huungua/kushika moto na kuteketea bila ya madhara kwa dunia. Ila imeshatokea si mara nyingi vipande kidogo kufika duniani. Nafikiri ni Mbeya kuna kitu kama hicho, na pia imeshatokea Urusi kwa miaka ya karibuni ya 2013.


View: https://youtu.be/dpmXyJrs7iU?si=n5gfri_uF3rcff68
 
Back
Top Bottom