Kaboom
JF-Expert Member
- Nov 6, 2011
- 10,828
- 14,976
Mlinzi wa Rais wa Tanzania huwa anachaguliwa na rais mwenyewe au kuna utaratibu mwingine unatumika kumpata?
Je, Mlinzi huyu anakuwa na likizo? Kama hana likizo, Je, Anapataje muda wa kujamiiana (Socialize) na jamii inayomzunguka pamoja na masuala ya kifamilia?
Sijui unamananisha nini unaposema mlinzi wa Rais. Kama unamananisha yule Ofisa wa jeshi mwenye sare ambaye unamananisha siku zote huwa nyuma ya Rais basi yule siyo mlinzi.
Yule ni ADC ambaye shughuli yake ni kuwa karibu na Rais kwa mambo mbalimbali ya kijamii na kazi kwa Rais.
ADC anaweza kuwa kazi yake ni kubeba speech kwa Rais, kumsaidia kwa mambo mengine kama kuangalia kiti kimekaaje na kadhalika na kadhalika.
Kwa upande mwingine ADC ni symbolic gesture ya madaraka ya Rais. Na ukumbuke sio marais wote wana Ma-ADC. Ukichunguza kwa makini utaona si rais kumuona ADC kwa Rais wa Marekani.
Kwa upande wa walinzi wa kiukweli ni kuwa wao hawavai sare. Walinzi hao wako wengi ingawa ni kweli yuko mmoja au wawili ambao siku zote ndiye yuko karibu na Rais. Mlinzi huyo aliye karibu na Rais hawezi kuchaguliwa na Rais.
Kikosi cha ulinzi cha Rais ndicho kinamteua mlinzi huyo kutokana na vigezo mbalimbali of course vikiwemo vya ukakamavu, ujuzi wa mafunzo ya mapambano kama karate, loyalty kwa system na kwa rais, muonekane wake na kadhalika na kadhalika.
Sidhani kama Rais anaweza kuwa na mkono katika uteuzi wake ingawa inawezekana pengine baada ya muda Rais anaweza akasema kuwa abadilishiwe mlinzi kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za majungu na kadhalika.
ADC huteuliwa na Jeshi lakini inawezekana pengine Rais akawa na 'ushawishi' katika uteuzi wake. Hapa neno 'ushawishi' liko kwenye mabano kwa makusudi.
Inamananisha vikundi mbalimbali katika jamii ambavyo viko karibu na Rais vinaweza vikapenyeza jina la ADC. Lakini kwa nchi zinazozingatia mfumo mzuri wa utendaji wa kazi na kuacha pembeni masuala ya ubabaishaji si rahisi kwa ADC kuteuliwa kiushikaji.Kuhusu hali ikoje kwa Tanzania mimi sijui. Tafuteni wenyewe uteuzi unakuwaje.