JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,308
- 5,460
Wakizungumza mbele ya Meneja wa (TRA) Mkoa wa Katavi, Nicholaus Migera wamesema kuwa wamechoshwa na vitendo vya kukadiliwa kodi kubwa kinyume na mapato ya biashara zao, jambo ambalo limepelekea baadhi yao kufunga biashara.
Aidha, wameongeza kwa kusema kuwa kwa muda mrefu wakihoji kuhusu jambo hilo wamekuwa wakijibiwa kuwa ambaye haridhiki na makadirio hayo au faini zinazotozwa na mamlaka hiyo afunge biashara.
Migera amesema Mamlaka hiyo itaendelea na program ya elimu kwa mlipa kodi ili kukuza uelewa wa masuala ya kikodi kwa wafanyabishara pamoja na kuwajengea uwezo watumishi wake ili kujiepusha na ukiukwaji wa maadili wakati wa ukusanyaji wa kodi na tozo zingine kwa wananchi.