Makonda: Stendi mpya Iringa ipewe jina la Chongolo

Mjanja M1

JF-Expert Member
Oct 7, 2018
3,660
12,304
Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, Paul Makonda amesema ataishawishi Serikali na Uongozi wa juu mara baada ya kukamilika kwa stendi mpya Iringa ili ipewe jina la aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo kwakuwa ameacha alama ndani ya CCM.

Makonda amenukuliwa akisema “Hapa kuna Kaka yangu Chongolo, nilikuwa nae yeye akiwa Mkuu wa Wilaya MimI nikiwa wa Mkoa Dar es salaam, yeye akiwa Katibu Mkuu wa CCM na mimi nikiwa Mwenezi wake sasa nilivyoambiwa kuna hitajika stendi nami nikasema kwa heshima ya Chongolo basi nami nitalibeba ili tuongeze sauti kuhakikisha tunajenga stendi angalau Mwana Mafinga Chongolo awe sehemu ya kumbukumbu na nitawashawishi Viongozi waweke jina la Chongolo kwenye stendi ikiwa sehemu ya kumbukumbu"

Makonda ameyasema hayo wakati akiongea na Wananchi wa Mafinga Mjini mkoani Iringa katika muendelezo wa ziara yake ya mikoa 20.

Credit - MillardAyo
 
Makonda mnafiq sana,yeye ndiye alimtengenezea Chongolo ajali ya kisiasa halafu anajaribu kumpaka mafuta kwa mgongo wa chupa.
 
Hawa Washenzi wanakula mali zetu na wanataka kuzipa mali zetu majina yao .... yaani mitaa haijawatosha!!?
Hii ni dharau sana kwa watanzania. watu wanaotoka nchi zenye watu wenye akili wakishuka hapa wakasikia mjinga mmoja anapambana jina la stand liwe fulani, badala ya kuchambua sera za uchumi na kubadilisha uchumi wa nchi, wanatuona hata sisi tunaomsikiliza mtu kama huyu na kuchekelea au kumfurahia ni mambumbumbu. nchi zingine watu walitakiwa wewe mtaani sasaivi kuandamana kwa dharau, anatuona Watanzania mambumbumbu tunaweza kudanganyika kwa siasa za kitoto namna hiyo, huu upuuzi sijui utaisha lini.
 
Cheap politics. Leo ni mwaka 2024 lakini utasema tuko miaka ya 1960's. Tuna safari ndefu sana kama hiki ndo chama tawala
Mtaji ni hawa stupid arogant uneducated majority wasio sikia, unaambiwa kusikia kwa kenge mpaka damu itoke maskioni.
 
Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, Paul Makonda amesema ataishawishi Serikali na Uongozi wa juu mara baada ya kukamilika kwa stendi mpya Iringa ili ipewe jina la aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo kwakuwa ameacha alama ndani ya CCM.

Makonda amenukuliwa akisema “Hapa kuna Kaka yangu Chongolo, nilikuwa nae yeye akiwa Mkuu wa Wilaya MimI nikiwa wa Mkoa Dar es salaam, yeye akiwa Katibu Mkuu wa CCM na mimi nikiwa Mwenezi wake sasa nilivyoambiwa kuna hitajika stendi nami nikasema kwa heshima ya Chongolo basi nami nitalibeba ili tuongeze sauti kuhakikisha tunajenga stendi angalau Mwana Mafinga Chongolo awe sehemu ya kumbukumbu na nitawashawishi Viongozi waweke jina la Chongolo kwenye stendi ikiwa sehemu ya kumbukumbu"

Makonda ameyasema hayo wakati akiongea na Wananchi wa Mafinga Mjini mkoani Iringa katika muendelezo wa ziara yake ya mikoa 20.

Credit - MillardAyo
Wakati yeye na Wahuni wenzake ndio Wamemfanyia FITINA za kumzalilisha MITANDAONI mpaka akajiuzulu Makonda alikuwa na Bifu toka CHONGOLO akiwa DC KINONDONI Makonda akiwa RC DAR

Sent from my SM-A145R using JamiiForums mobile app
 
Hii ni dharau sana kwa watanzania. watu wanaotoka nchi zenye watu wenye akili wakishuka hapa wakasikia mjinga mmoja anapambana jina la stand liwe fulani, badala ya kuchambua sera za uchumi na kubadilisha uchumi wa nchi, wanatuona hata sisi tunaomsikiliza mtu kama huyu na kuchekelea au kumfurahia ni mambumbumbu. nchi zingine watu walitakiwa wewe mtaani sasaivi kuandamana kwa dharau, anatuona Watanzania mambumbumbu tunaweza kudanganyika kwa siasa za kitoto namna hiyo, huu upuuzi sijui utaisha lini.

Halafu huyo jamaa mwenyewe wanayetaka kumpa kaondoka madarakani kwa kashfa za ngono ... we are not serious!!
 
Hiyo ilikuwa Gia ya kuwadanganya wanaIringa ili wasikumbuke kuwa ndugu yao Chongolo alifitiniwa na yeye...ujinga ni kipaji.
 
Back
Top Bottom