Mkurugenzi wa LATRA anapata wapi nguvu ya kupingana na Rais? Serikali inakataza kufunga biashara, yeye anafungia mabasi 35 yasitoe huduma

Kabla basi au Kampuni haijafungiwa kuna hatua mbalimbali zinafanyika kabla ya kufikia hatua hii mfano;
Kuonywa kwa maandishi
Makosa kujirudia mara kwa mara licha ya kuonywa
Pia kuna masharti ya leseni kama yalivyoainishwa ktk leseni.

Zipo kanuni mbalimbali ambazo zipo zikionyesha adhabu zinazotakiwa kuchukuliwa.
Ni vyema mleta hoja (kilimanjaro) ukazingatia matakwa ya leseni yako badala ya kupayuka mtandaoni!
 
Ukisoma wachangiaji wengi humu hata tangazo awajasoma......tunachojadili hapa kikiendelea kupewa kipaombele ipo siku watafunga biashara yako na hakuna atakayeweza kuhoji.....

Jaribuni kuondoka kwenye fikra za kijamaa.....nchi zilizopiga hatua hazikujikita kufunga biashara zilijikita kuweka mazingira wezeshi ya kutoa huduma

Mfano mimi ungeniambia nisimamie mfumo wa tiketi nisingeangaika na mwenye gari ningeweka masharti ya kuwasilisha mfumo wa tiketi nikague na kuupitisha ndipo nitoe tiketi......leo hii hawa LATRA hata mifumo ya kukata tiketi sidhani kama wanajua ubora wao.

Mifumo ya kukata tiketi online yenye viwango kwa Tanzania labda mfumo wa BM na Shabiby ila mifumo mingine yote haina ufanisi uliokusudiwa.

Mimi nipo mwanza , hadi naandika hapa nimejaribu kupitia sample ya mifumo kumi na tano ya watoa huduma ila Mifumo inayokupa matokeo chanya kwa online ticketing ni miwili tu ambayo ni BM na SHabiby....unaweza ukajaribu kwenye simu yako.

Hivyo tunapojadili hizi hoja hatupaswi kuweka roho zetu za wivu tunapaswa kuangalia waliofanikiwa wanafanya vipi? Hakuna nchi serious inayofungia vyombo vya usafiri, wanapenalize kampuni kupitia vipimo vya ufanisi.

Lakini pia tujiulize, lini tumesikia wananchi wakilalamikia kampuni iliyofungiwa? Hakuna siku wamewahi kulalamikiwa ; hizi ni issue za ushindani wa biashara kwamba sasa hivi biashara ni kubwa basi tupunguze watoa huduma.

Lastly sina uhakikia na root za Kilimanjaro ila lazima kuna maasimu wa kibiashara .....nikisearch hapa nakutana na malalamiko ya abiria desemba kuchelewa kufika ....so let us fighting this fungia mentality kwa sababu zilifanikiwa kwenye mabasi zitahamia kwenye vibanda vyetu
Hivi umefatilia maelezo ya LATRA na umeweza kuyaelewa hayo maelezo yao.
Je hiyo kampuni ya KILIMANJARO kuna sehemu wanasema kuwa wanavyo tuhumiwa navyo ni propaganda za kibiashara?.
Vipi wewe na kampuni ni nani haswa mwenye uchungu wa kufungiwa kwa kampuni?
Mwisho kwa maelezo ya LATRA wa kishilikiana na askari wa usalama barabarani kampuni ya KILIMANJARO inastahiki kufungiwa kutoa huduma mpaka hapo watakapo toka hadharani na kuomba radhi na kuahidi kutorudi tena hayo wanayo fanya
 
Mwambieni mmiliki wa Kilimanjaro bus service afuate sheria.

Hizi mada za humu hazitamsaidia.

Atoe tiketi za kieletroniki, asizdishe nauli, asikwepe kodi, afuateratiba ya mabasi iliyowekwa.
Kilimanjaro wanaendesha kampuni kihuni sana kwa kweli
 
Unaendeleaje kumsimamia mkaidi!? Mtu anayetamba wazi wazi kwamba yeye atafanya anavyotaka na kama faini ataendelea kulipa!?

Huyo mkaidi acha afaidi ukaidi wake na wala usimjumuishe Rais kwenye hilo.
Kama analipa faini shida Nini si aendelee tu huku akidakwa analipa anaingiza Mapato serikalini
 
Ajira zenyewe unazosemea hazifiki hata 200 kama anajiona yupo juu ya Sheria jawabu awajibishwe tu ...usitake kuchonganisha watu na raisi wao maana kusema kweli awamu hii serikali imekuwa fair sana kwa wafanyabiashara
 
Nimelipishwa sh 55,000 moshi to Dsm, ticket ya kuandika mkononi basi sasa limeletwa scania namba A, limechoka kwa kweli haiendani na hiyo bei kabisa..
Wahudumu wamenuna balaa..

Mara 100 basi za boss wamaokoto nauli nzuri , basi mpya na wahudumu wapo safi sana ila siyo hawa klm kabisa.
Mimi nilipogiwa sim eti niongeze nauli kuwa luxury ndo zinapatikana baada ya zile za kwanza kupotea
 
Ukisoma wachangiaji wengi humu hata tangazo awajasoma......tunachojadili hapa kikiendelea kupewa kipaombele ipo siku watafunga biashara yako na hakuna atakayeweza kuhoji.....

Jaribuni kuondoka kwenye fikra za kijamaa.....nchi zilizopiga hatua hazikujikita kufunga biashara zilijikita kuweka mazingira wezeshi ya kutoa huduma

Mfano mimi ungeniambia nisimamie mfumo wa tiketi nisingeangaika na mwenye gari ningeweka masharti ya kuwasilisha mfumo wa tiketi nikague na kuupitisha ndipo nitoe tiketi......leo hii hawa LATRA hata mifumo ya kukata tiketi sidhani kama wanajua ubora wao.

Mifumo ya kukata tiketi online yenye viwango kwa Tanzania labda mfumo wa BM na Shabiby ila mifumo mingine yote haina ufanisi uliokusudiwa.

Mimi nipo mwanza , hadi naandika hapa nimejaribu kupitia sample ya mifumo kumi na tano ya watoa huduma ila Mifumo inayokupa matokeo chanya kwa online ticketing ni miwili tu ambayo ni BM na SHabiby....unaweza ukajaribu kwenye simu yako.

Hivyo tunapojadili hizi hoja hatupaswi kuweka roho zetu za wivu tunapaswa kuangalia waliofanikiwa wanafanya vipi? Hakuna nchi serious inayofungia vyombo vya usafiri, wanapenalize kampuni kupitia vipimo vya ufanisi.

Lakini pia tujiulize, lini tumesikia wananchi wakilalamikia kampuni iliyofungiwa? Hakuna siku wamewahi kulalamikiwa ; hizi ni issue za ushindani wa biashara kwamba sasa hivi biashara ni kubwa basi tupunguze watoa huduma.

Lastly sina uhakikia na root za Kilimanjaro ila lazima kuna maasimu wa kibiashara .....nikisearch hapa nakutana na malalamiko ya abiria desemba kuchelewa kufika ....so let us fighting this fungia mentality kwa sababu zilifanikiwa kwenye mabasi zitahamia kwenye vibanda vyetu
Mkuu ukiachana na Mifumo ya ki eletronic.
Basi za Kilimanjaro nilizopanda 2011(BVN)Lipo barabarani mpaka leo ni bovu sio kwa kusimuliwa.Yapo mengi hasa haya yaa AQN,ACN.e.tc Hao ndio nauli ni 37,000-44,000/=

Mimi ni mdau sana wa usafiri wao tokana na mwendo ,nje na zile Polo G7 naanza na DMH series,DHY,DPT na hizi EAU (zipo nne)
Kama tu hizi EAU zimeanza kuwa chafu ndani basi KLM ana mengi ya kuamua.

Na hizo EAU series ndizo nauli 55,000/= VIP ambayo mkifika mbelembele huko wanapakia abiria wanakaa pale kwa Dereve kwa kigodoro.Achana na hayo charging system baadhi ya seat ni hazifanyi kazi.
 
Watumishi wa umma wanapaswa kuwa watu wanaotumia akili na busara kubwa sana. Wanalipwa mishahara kwa kodi za wananchi , wanalipwa kwa sababu kuna watu waliamua kufanya biashara. Lakini wao ni kama wanalipwa kwenda kuua biashara nchini.

Nasema haya baada ya kuona LATRA ikitoa tangazo kwa umma lakufungia mabasi 35 ya kampuni ya Kilimanjaro yasitoe huduma. Ukisoma tangazo lao hakuna Sehemu popote walipoeleza kwa ushahidi kampuni husika imetenda kosa gani, wameandika general statement ambayo inaonyesha wao wana mamlaka yakutuhumu na kutoa hukumu bila kusikiliza.

Hakuna Sehemu kwenye barua wanaonyesha wamechukua juhudi gani kushauriana na Kampuni ya Kilimanjaro. Hakuna Sehemu wanasema lini wahusika walikiuka haya masharti. Hakuna Sehemu wanasema mfumo wa kampuni hiyo unawaathiri vipi wananchi? Hii ingesaidia wananchi kutambua mapungufu na kuripoti endapo yapo kwa makampuni mengine.

Nirudi kwenye hoja, mhe. Rais anapotoa tamko ni amri na ndio mtizamo wa Utawala wake. Mhe Rais wakati anakataza kufungwa biashara alikuwa anaeleWa madhara yatokanayo na kufungia biashara na namna yalivyotishia uhai wa uchumi wetu.

Unapotafakari mtizamo wa Mhe. Rais ambao umekuwa unasisitizwa sana na Mh. Waziri wa fedha unajiuliza hawa wakurugenzi huwa wanawasikiliza mabosi zao?

Kupitia tangozi hili wapo watu wanakwenda kuathirika moja kwa moja

1. Kuendesha magari 35 maana yake madereva na makondakta wote hawana kazi ya kufanya na hivyo awatalipwa mishahara kwa kipindi chote.

2. Wahudumu wa kampuni hii wote wanakwenda kubaki nyumbani wakisubiri LATRA wakubali kufungulia au wakatae

3. Kodi ya serikali haitakusanywa kwa magari haya 35 ambayo yamefungiwa

4. Wasafiri waliokata tiketi kwa tarehe hizi maana yake watalazimika kutafuta utaratibu mwingine na may hakuna refund itakayofanyika. Kumbuka hiki ni kipindi ambacho watoto wanarudi shule.

Huu ni uchambuzi mdogo tu kuhusu athari za tamko hili. Lakini tujiulize makampuni mangapi mifumo ya tiketi inasumbua? Leo tujiulize mifumo ya serikali ikiwa na kasoro tunafunga hizo ofisi za umma? Ofisi gani ya umma imewahi kufungwa kupisha matengenezo ya mfumo?

Inawezekana Mh. Rais anawaza vingine na watendaji wanawaza kivingine.

Nilitegemea kwenye tangazo hili iwepo kauli kwamba LATRA wamefanya ukaguzi wa mfumo wa Kilimanjaro nakubaini kasoro 1,2,3.....wamewaelekeza kuzitatua na kufikia tarehe .......zisipotatuliwa kampuni itafungiwa kutoa huduma........kupitia tangazo la aina hi means kampuni inajua, wasafiri wanajua na hivyo unawaandaa kisaikolojia kuzikwepa hizi athari.

Sory to say, NI TANZANIA PEKEE NDIPO MAMLAKA ZINAKAZANA KUUA BIASHARA BADALA YA KUSIMAMIA UFANISI. NA HII INATOKANA NA MAMLAKA HIZI NYINGI KUPEWA JUKUMU LA KUDHIBITI. MDHIBITI SIKU ZOTE NI MTU WAKUKWAMISHA.
Kuna dhuluma na vita ya kibiashara hapa mahali. Sijawahi kusafiri bila ticket ya electronic kwenye hii kampuni. Na meseji napata kwenye simu yangu
 
Mkuu ukiachana na Mifumo ya ki eletronic.
Basi za Kilimanjaro nilizopanda 2011(BVN)Lipo barabarani mpaka leo ni bovu sio kwa kusimuliwa.Yapo mengi hasa haya yaa AQN,ACN.e.tc Hao ndio nauli ni 37,000-44,000/=

Mimi ni mdau sana wa usafiri wao tokana na mwendo ,nje na zile Polo G7 naanza na DMH series,DHY,DPT na hizi EAU (zipo nne)
Kama tu hizi EAU zimeanza kuwa chafu ndani basi KLM ana mengi ya kuamua.

Na hizo EAU series ndizo nauli 55,000/= VIP ambayo mkifika mbelembele huko wanapakia abiria wanakaa pale kwa Dereve kwa kigodoro.Achana na hayo charging system baadhi ya seat ni hazifanyi kazi.
Ungekua poa kama ubovu upo kwenye kitu gani... Wabongo ni wavivu wa kufikiri sana
 
Ungekua poa kama ubovu upo kwenye kitu gani... Wabongo ni wavivu wa kufikiri sana
Upo VIP bus 55,000/=
Unataka kuchaji simu,inakulazimu uchaji kwa jirani,halafu tukio hilo sio mara moja.

Hizi bus za miaka ya nyuma alizonazo nyingi zina Mende ndani..uchakavu na kuana baadhi huwa zinaharibikia sana njiani.

Kibaya ziadi kuna mchezo unafanyika inaweza kuwa Boss wao hajui.Unakata VIP ukiwa unajua ni Bus tulivu na kama linavyojieleza.
Utaombwa msamaha kuwa lile haliji..utapanishwa kwenye Basi za zamani chakavu.

Kuna mambo ya Kuboresha kutoka KLM,otherwise wapo vyema kwenye mwendo.
 
Back
Top Bottom