saigilomagema
JF-Expert Member
- Jun 5, 2015
- 4,173
- 6,158
Kuna daladala zimepewa leseni za kusafirisha abiria kutokea maeneo yafuatayo;
1. Oldonyosambu, Monduli, Morombo, Intel, Kisongo kupitia stand ndogo kwenda Kiong'ori
2. Oldonyosambu, Monduli, Morombo, Intel, Kisongo kupitia stand ndogo kwenda Kikatiti
Haya magari kwanza hayaanzii safari sehemu husika km nilivyozitaja hapo juu, mengi km si yote huanzia safari zao stand ndogo. Pili hayafiki mwisho wa safari yaani Kikatiti na King'ori, King'ori ndiyo kabisa hakuna gari linaenda kule. LATRA mkoa wa Arusha mnayafahamu yote haya ila kwasababu ya rushwa iliyokithiri hapo ofisini kwenu hamjishushulishi na mateso ya wananchi. Polisi trafiki wanajua vizuri ila kwasababu ya rushwa na kuwa magari mengine ni ya kwao hawaoni shida kutosimamia sheria.
Kwanini mtu akate leseni ya usairishaji ruti aliyoichagua yeye mwenyewe bila kulazimishwa na akipewa ruti anakuja kujipangia anavyotaka. Ile ni huduma kwa wananchi, watu tunaishi ndani ya nchi yetu kwa wasiwasi huna uhakika wa kufika unakoenda ingawa gari ulilopanda hata kibao chake mbele kinaonesha kinakotakiwa kufika. Badala yake madereva na makondakta ni wababe, wana lugha chafu kuliko unavyoweza kufikiri, anaweza kukujibu kuwa nenda mkokote kashtaki. Wakifika maji ya chai dereva anashuka mtakaa hata nusu saa au zaidi wakisubiri gari ya kuwafaulisha wanavyoita wao, hivi watanzania tumekuwa mizigo mpaka tufaulishwe? na wana lugha yao nyingine ya kusema tunawawauzia gari nyingine, kwanza huu ni udhalishaji wanaofanyiwa wananchi ndani ya nchi yao huru
Mkurugenzi mkuu wa LATRA CPA Suluo nchi hii inajua we ni mchapakazi umeiheshimisha LATRA, ila LATRA mkoa wa Arusha imeoza. Tunaomba msaada wako. Weka maafisa wako pale kituo cha maji ya chai tena watoke Dsm siyo hawa wa Arusha ambao wameshaoza na rushwa, afisa wa LATRA siyo wa kukaa ofisini wantakiwa wazunguke mitaani kuangalia changamoto wanazopata washika dau wao ambao ni abiria, changamoto zingine zinapata majibu on the sport.
Basi lolote litakalokamatwa limeishia Maji ya Chai lifutiwe leseni ya kwenda King'ori au Kikatiti apewe ruti yake ya kuishia hapo hapo Maji ya Chai na abadilishe kibao kuwa gari lake linaishia Maji ya Chai.
Ni serikali tu ndio itatusaidia, hawa wenye mabasi hawaridhiki labda mpaka wale mioyo ya binadamu wenzao, ni majuzi tu nauli iliongezwa, mwezi uliofuata mafuta yalipuangua bei, leo mtu anakuambia mafuta haya ni mashetani manyanayasaji, CPA Suluo wasaidie watanzania wenzako wanaoteswa. Unakuta basi lina abiria hata 10, anageuza. Nafikiri kisheria hata km kuna abiria moja anatakiwa afikishwe mwisho wa safari, hata km hakuna abiria gari linatakiwa lifike mwisho wa safari maana kuna abiria watakuwa njiani wanasubiri usafiri, wengine watakuwa vituo vya mbele inakoelekea gari, wengine wanalisunbiria aidha Kikatiti au King'ori.
Km watu hawataki kustaarabika wenyewe walazimishwe na sheria kustaarabika, mbona mambo hayapo nchi jirani za wenzetu? Tanzania kuna nini, lini tutastaarabika? Ni aibu! Kenya wametuacha mbali sana kwa ustaarabu ktk usafiri, kwanza hukuti hata abiria anayesimama. Nchi za Zambia, Zimbabwe, Uswatini ndiyo km uzunguni, bado South, Namibia. Baadhi ya nchi nimefika ustaarabu wao ni wa hali ya juu sana. Ukija huku kwetu utafikiri sisi sijui ni watu wa aina gani. Siku hizi madereva na makondakta wao Arusha hawavai uniform wamekaa kihuni huni tu, na mamlaka zipo. Arusha inatakiwa isafishwe kuna uozo kuazia jeshi la polisi k,itengo cha usafiri barabarani na LATRA. RTO wa Arusha na map-DTO wake wanafikiri wapo pale kula rushwa na kufanya biashara zao. Ondoeni hawa watu Arusha pelekeni huko mikoa mingine tena ya pembezoni mwa nchi, peleka wilaya km za Tunduru.