Mkurugenzi Mkuu wa Bandari asimamishwa kazi!

Kazi nzuri,ila huko TPA ni moja kati ya sehemu nyingi zenye uozo katika uwajibikaji,yaani ni ubabaishaji mtupu,just imagine tulikua tunategemewa na majirani katika kuingiza na kutoa mizigo lakini kutokana na uzembe hawa jamaa tumekimbiwa! Ngoja tuone mwisho wa picha!
 
mkurugenzi wa TPA asimamishwa kazi kupisha uchunguzi....
source issa michuzi.....
 
fukuza wte kisha simamisha kizimbani si mnawafukuza af wanakaa mtaani wanatumbua raha na mkwanja wetu malabuku zao
 
Nina hamu na watu wa TPA walikwiba mziki wa gari yangu tena walinyofoa kwa kuvunja nyangau sana hawa
inatulazimu kupitishia magari mombasa kwa ajili ya washenzi wachache pale bandari
mbaya zaidi ukitaka uipate iyo stolen item faster wanakuletea ila lazima utoe mkwanja yaani ni kama legalised business vile
 
Jaribuni kuangalia threads kabla ya kupost, hii issue ina threads kama tano tayari hapa.
 
Waziri wa uchukuzi amemsimamisha mkurugenzi mkuu wa Bandari-TPA NDG Ephraim Mgawe pamoja na wasaidizi wake wawili kwa tuhuma mbalimbali zinazowakabili... wengine waliosimamishwa kazi ni meneja wa mafuta ya ndege kurasini,meneja wa JET NA meneja wa OIL TERMINAL Kutokana na kosa la kupotea mafuta na kuidanganya serikali mafuta safi na machafu...mwakyemebe amemteua inginia Madeni Kipange kukaimu nafasi ya mkurugenzi mkuu---

My take> Jembe linaendelea kusafisha taasisi zilizo chini ya waizara ya Uchukuzi.

JAMANI NAOMBENI MAJINA YA HAWA

1) Meneja wa Jeti
2)Meneja wa Oil terminal
3)Meneja wa Mafuta ya ndege kurasini
 
..Hivi kuwasimamisha hawa Wakurugenzi Wakuu ni solution?!!, ATCL nako lilifanyika hili mwisho wa siku shirika limesimamisha safari za ndege zake..

Kiongozi vipi tena nawe mbona hueleweki! Unataka kupunguza kasi ya mpiganaji katika kuchapa kazi na maamuzi ya busara anayoyafanya? Manake hamchelewi kusema oooh hafai. Leo anatumia fagio lake,tayari mmeishaanza kuhoji! Mbona wanadamu haturiziki? Toa ushauri basi unataka afanye nini ili iwe ndiyo solution ya matatizo. BIG UP MWAKYEMBE.
 
jama huyu wa shirika landege mapka sasa hajapelekwa kwa pilato,leo makida makida hapo bandari pata fanyika km atcl msipige kelele ,hongera mwakyembe endelea kuwanyoa mpaka ngozi zitoke
 
..Hivi kuwasimamisha hawa Wakurugenzi Wakuu ni solution?!!, ATCL nako lilifanyika hili mwisho wa siku shirika limesimamisha safari za ndege zake..

Ingekuwa ni wewe ungefanyaje? Toa ushauri. Mpiganaji anatumia fagio la chuma alilopewa kusafisha na kukwangua kutu na mazagazaga mengine machafu. Hataki mambo ya ushikaji. Eti sijui leo umeharibu hapa unahamishiwa sehemu nyingine, hiyo hakuna. Fagio la chuma linapitishwa kisha msasa na mwisho inapakwa vanishi. BIG UP MWAKYEMBE.
 
ingekuwa ni wewe ungefanyaje? Toa ushauri. Mpiganaji anatumia fagio la chuma alilopewa kusafisha na kukwangua kutu na mazagazaga mengine machafu. Hataki mambo ya ushikaji. Eti sijui leo umeharibu hapa unahamishiwa sehemu nyingine, hiyo hakuna. Fagio la chuma linapitishwa kisha msasa na mwisho inapakwa vanishi. Big up mwakyembe.

ange waacha wale vyao na kustahafu kwa usalama
 
Huyu jamaa mpuuzi hata kwao hajajenga nyumba nilionyeshwa msingi wa nyumba toka 1983.shame on him
 
Back
Top Bottom