Mkurugenzi Mkuu wa Bandari asimamishwa kazi!

PigaKuraYako

Member
Oct 28, 2010
21
6
Waziri wa Uchukuzi Tanzania Dk. Harisson Mwakyembe amemsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa TPA Ephrahim Mgawe pamoja na wasaidizi wake wawili.

SOURCE: East Africa TV

Kwa Maelezo zaidi:-

Dkt. Mwakyembe amsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Bandari

1.jpg

Waziri wa Uchukuzi Dkt. Harisson Mwakyembe amemsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari-TPA-Ndugu Ephrahim Mgawe pamoja na wasaidizi wake wawili ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili.

Wengine waliosimamishwa ni Meneja wa Mafuta ya Ndege Kurasini, Meneja wa JET na Meneja wa Oil Terminal kutokana na tuhuma za kupotea kwa mafuta na kuidanganya serikali kuhusu mafuta masafi na machafu.

Kutokana na kuwasimamisha kazi Wakurugenzi hao Dkt. Harisson Mwakyembe amemteua Injinia Madeni Kipange kukaimu nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa TPA.

Kufuatia tuhuma hizo zinazofanywa Bandarini Dkt. Mwakyembe ameunda Tume wa ya watu saba kufanya uchunguzi kwa wiki mbili na kumpelekea taarifa ofisini kwake ili kubaini ukweli wa tuhuma hizo zikiwemo za wizi.

Pia ameagiaza kufikia Septemba Mosi mwaka huu malipo yote yafanyike benki ili kuondoa rushwa na wizi unaofanyika ndani ya Mamlaka hiyo.

Waziri Mwakyembe anachukua hatua hizo kutokana na wadau wengi sasa hawaitumii Bandari ya Dar es salaam kupitisha mizigo yao kutokana na kutokuwa na imani na watumishi wake kitu kinachoifanya serikali kukosa mapato.

Pia ameagiza kusimamishwa mara moja kwa Kampuni ya Singilimo ambayo inajihusisha na kazi ya kubeba mafuta machafu na badala yake itafutwe Kampuni nyingine.
 
This step was long overdue, baada ya Omar Nundu kuyaanika yale maroroso ya upanuzi wa bandari yaliyokuwa yakifanywa na Mfutakamba, kulikopelekea Nundu kupigwa chini, tulisema humu kuwa Mgawe sio salama na hata bodi ya TPA itavunjiliwa mbali soon!.

Ile kampuni yao tegemeo ya CCCC ya Uchina, iko kwenye black book ya WB kwa makampuni yanayoshinda tenda kwa rushwa!.
 
Ni kweli, sio tetesi, wana siku 14 wanafanyiwa uchunguzi kutokana na ufisadi uliokithiri TPA.

Ni Ephraim Mgawe - DG
Casian Ngamilo - PMCapt. Masalu

Hii tumeipata kwenye port meeting leo

Wacha waende, wanatusababishia hasara sana hii nchi, meli zinashindwa kufika tanzania sababu ya ufisadi wao . waende wana kwenda, am so happy kwa kuwa imenikera sana kila siku japo kazi nafanya.
 
Wakuu,

Muda si mrefu Mkurugenzi Mkuu wa Bandari Bw. Mgawe na wakurugenzi wengine watatu pamoja na Meneja wa Bandari ya Dar Es Salaam Bwana Cassian Ngamillo wamesimamishwa kazi na waziri wa Uchukuzi Mheshimiwa Mwakyembe.

Inasemekana, kama kawaida yake amewasimamisha vigogo hao mbele ya kikao cha wafanyakazi kilichofanyika leo muda si mrefu..

Source: Mfanyakazi wa TPA aliyekuwa kwenye kikao.

More updates to follow, stay tuned.
 
1.jpg

Waziri wa Uchukuzi Dkt. Harisson Mwakyembe amemsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari-TPA-Ndugu Ephrahim Mgawe pamoja na wasaidizi wake wawili ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili.

Wengine waliosimamishwa ni Meneja wa Mafuta ya Ndege Kurasini, Meneja wa JET na Meneja wa Oil Terminal kutokana na tuhuma za kupotea kwa mafuta na kuidanganya serikali kuhusu mafuta masafi na machafu.

Kutokana na kuwasimamisha kazi Wakurugenzi hao Dkt. Harisson Mwakyembe amemteua Injinia Madeni Kipange kukaimu nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa TPA.

Kufuatia tuhuma hizo zinazofanywa Bandarini Dkt. Mwakyembe ameunda Tume wa ya watu saba kufanya uchunguzi kwa wiki mbili na kumpelekea taarifa ofisini kwake ili kubaini ukweli wa tuhuma hizo zikiwemo za wizi.

Pia ameagiaza kufikia Septemba Mosi mwaka huu malipo yote yafanyike benki ili kuondoa rushwa na wizi unaofanyika ndani ya Mamlaka hiyo.

Waziri Mwakyembe anachukua hatua hizo kutokana na wadau wengi sasa hawaitumii Bandari ya Dar es salaam kupitisha mizigo yao kutokana na kutokuwa na imani na watumishi wake kitu kinachoifanya serikali kukosa mapato.

Pia ameagiza kusimamishwa mara moja kwa Kampuni ya Singilimo ambayo inajihusisha na kazi ya kubeba mafuta machafu na badala yake itafutwe Kampuni nyingine.
 
Waziri wa uchukuzi amemsimamisha mkurugenzi mkuu wa Bandari-TPA NDG Ephraim Mgawe pamoja na wasaidizi wake wawili kwa tuhuma mbalimbali zinazowakabili... wengine waliosimamishwa kazi ni meneja wa mafuta ya ndege kurasini,meneja wa JET NA meneja wa OIL TERMINAL Kutokana na kosa la kupotea mafuta na kuidanganya serikali mafuta safi na machafu...mwakyemebe amemteua inginia Madeni Kipange kukaimu nafasi ya mkurugenzi mkuu---

My take> Jembe linaendelea kusafisha taasisi zilizo chini ya waizara ya Uchukuzi.
 
Mgawe mie nilisema tangu Kikwete alipomteua kwamba si mtu wa kuiweza ile kazi.

Basically tatizo limeanza na uteuzi wa Kikwete.
 
Akimaliza wizara hiyo ahamishiwe wizara ingine akasafishe kabla hawajamuweka speed governor.lol
 
Back
Top Bottom