Mkulo, Maige, Ngeleja kikaangoni TAKUKURU

Ahsante robot kwa taarifa.

Kwa kifupi tu sitegemei kitu chochchote chanya hapa, ni zile zile sarakasi za takukuru na ccm.
Hapa tunazugwa ili tuwache kupiga kelele.
 
Takukuru is Toothless hata miba ya Samaki hawawezi kuivunja wataweza hiyo Mifupa ya Ng'ombe.

Takukuru wenyewe wala Rushwa hawana lolote hapo ni Changa la macho wa Watanzania
Hii kweli wenyewe wanahitaji kuchunguzwa sababu za kushindwa kukamata mafisadi wa EPA.
Mimi nadhani ili kweli TAKUKURU iweze kufanya kazi inabidi liwe shirika pekee litakaloongozwa na Vyama vya upinzani.
Hahahaaaa!
 
mkuu Invisible, kichwa cha habari kingesomeka "takukuru kuwasafisha Mkulo, Maige na Ngeleja"
habari ingenoga!!!!!!!
 
Last edited by a moderator:
Kati ya taasisi ninazopendekeza zifutwe hapa nchni ni hiyo takukuru. Inaongoza kwa rushwa. Hawana maana yoyote zaidi ya kula bure pesa za walipa kodi.

Ktk sakata hili wangeanza kushitakiwa hao takukuru kwa kushindwa kuwajibika. Kama wangekuwa wanawajibika wizi huo ungetokea wapi?????? Mpaka waambiwe ndio waanze uchunguzi kwani wao wamekuwa polisi?

Ni heri hiyo taasisi ifutwe kazi wanayoifanya polisi wanaimudu vizuri kuliko hata wao. Tena polisi wanakula rushwa ndogo hao jamaa wanakula rushwa kubwa mno. Ni kuifuta tu hiyo taasisi hakuna kitu hapo!
 
Hivi ni kwa nini siku zote Watanzania tulio wengi huwa hatugundui kuwa Serikali ya CCM inatudanganya kwa mambo mengi kwa nia ya kutuliza na kutupotezea agenda zetu.

Kinachoonekana hapa ni kiini macho tu ili kupoteza na kutusahaulisha fikra tulizonazo dhidi ya uongozi mbovu wa Serikali ya awamu ya nne.

Mkulo, Maige na Ngereja hawakuwa pekee yao katika deal hizi ni lazima nyumayo kulikuwa na wengine na hata TAKUKURU Watakuwa ni washirika na matokeo yake kinachofanyika usishangae jioni watu wanapigiana simu ili kupeana updates za reaction za mtaani.
 
mkuu Invisible, kichwa cha habari kingesomeka "takukuru kuwasafisha Mkulo, Maige na Ngeleja"
habari ingenoga!!!!!!!

Takukuru ni Washing Machine ya Mafisadi na Hapo hamna Kesi yoyote na hakuna mtu atakayepelekwa Mahakamani au Gerezani zaidi ya Takukuru kula Kodi zetu kwa uchunguzi wa kijinga na mwsiho watakuja na conclusion ya kusema hakuna wizi uliofanyika zaidi ya kelele za Wapinzani na hatufanyikazi kwa kusukumwa na Wapinzani. Dr. Hosea pia ni Janga la Taifa kama Kikwete. Help us GOD tutoke hapa tulipo
 
Nasubiri kwa hamu kuona mwisho wa hiyo sinema mpya in town kwa hisani ya CCM. Uliwahi kuona wapi mtuhumiwa wa wizi kwa mali za umma akiandikiwa tena hundi eti kwa kimombo cha GRATUITY?

NOOOOO kama kweli majarada yapo kwa Hosea watafikishwa mahakaman,na pia inategemea na uzito na ushahidi wa tuhuma dhidi yao.PCCB is strong enough,subirin mtaona
 
NOOOOO kama kweli majarada yapo kwa Hosea watafikishwa mahakaman,na pia inategemea na uzito na ushahidi wa tuhuma dhidi yao.PCCB is strong enough,subirin mtaona
PCCB hawana strength zaidi ya CAG. Inamaana CAG asingebaini madudu hela za walipa kodi si zilishaibwa na hao jamaa? Inawezekana kabisa hao wezi wanakula mchongo na PCCB.

Waburuzwe wote hao mahakamani na wote wawe chini ya uchunguzi. PCCB haina kazi hapa nchini. Ifutwe tu! Wao walitakiwa wajikite zaidi kwenye kuzuia siyo mpaka rushwa ibainike wao wende kuprosecute, kwani state attorneys wote waliopo hiyo kazi hawaiwezi?

PCCB wanakera na wanasaidia mafisadi kutokamatwa kwani wanawasaidia jamaa kupoteza ushahidi tu. Wasiwe wanahusishwa ktk corruption ambazo zimeshagundulika na vyombo vingine.
 
Takukuru ni Washing Machine ya Mafisadi na Hapo hamna Kesi yoyote na hakuna mtu atakayepelekwa Mahakamani au Gerezani zaidi ya Takukuru kula Kodi zetu kwa uchunguzi wa kijinga na mwsiho watakuja na conclusion ya kusema hakuna wizi uliofanyika zaidi ya kelele za Wapinzani na hatufanyikazi kwa kusukumwa na Wapinzani. Dr. Hosea pia ni Janga la Taifa kama Kikwete. Help us GOD tutoke hapa tulipo

Kwa kuwa hawa akina maige hawatuhumiwi kupewa rushwa wazi wazi, bali matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia serikali hasara kubwa, hapa dpp angewasweka ndani wote kwa shitaka la kuhujumu uchumi!!!!!!! na mashitaka mengine yangewafuata huko huko gerezani, kama takukurupuka nao wangeanzisha uchunguzi wao wa kirushwa rushwa haingekuwa mbaya. kwa sasa Feleshi anasubiri naye akumbushwe majukumu yake!
 
Kweli hawa jamaa waliingiwa na shetani mpaka mtu una airfreight gari? Wanastahili kifungo kwakweli la sivyo wafilisiwe kabisa..
 
Watanzania hasa vijana, kwa ufahamu wangu na udadisi juu ya Politics, Power Strugle and Economy naomba nisimame kuhesabiwa miongoni mwa watakao dumu daima upande wa utetezi kwa Ezekiel Maige.

Mzimu mkubwa unaomwandama huyu Mtanzania si nyumba aliyonunua $0.7M cash au njia aliyotumia kupata hiyo pesa bali ujasiri wake kuvuluga syndicate ya waporaji wa maliasili zetu waliodumu kwenye sekta tangu miaka ya mwanzo wa 1960.

Na kubwa la pili ni malengo makubwa na dhamira ya dhati iliyokuwa ikijidhihirisha katika mafanikio yaliyokuwa yameanza kupatikana katika sekta ya Maliasili na Utalii. Maize asingeweza kuyafanya haya bila kuyagusa na kuyabatilisha maslahi makubwa na ya toka enzi ya wakubwa wa nchi hii. Wakubwa hao wengi wako nje ya serikali na hata nje ya nchi. Wananguvu za kubadilisha uongo kuwa ukweli na kinyume chake vilevile. Mwiko aliouvunja Maize ndo Ngeleja alidhani kwa kuuenzi nao watamuenzi kumbe haikuwa hivyo. Ngeleja hajavuluga maslahi ya mkubwa yeyote ila pale wao walipokula yeye kakomba mboga hadi kulamba mwiko.

Rai yangu kwa vijana wasimeze habari kama zinavyowekwa kwenye vyombo vya habari. Na katika yanayoitwa kashfa kuu kupitia kamati za Bunge msichukulie wajumbe kama Malaika na kudhani kila wanalotaarifu ndo ukweli. Hata marefa wana timu zao! Ukitaka kunielewa rejea mswada wa kuondoa kodi kwenye mafuta ya taa uone jinsi Bunge na Kamati zinavyotumika ki-udalali hata katika masuala nyeti.

Nikipata muda nitajitahidi nifumbue mafumbo zaidi labda vijana wenzangu mtanielewa. Hapa mimi si mjumbe wa Maige bali ni muathirika wa ukweli uliopindishwa. Kwa jinsi hii taifa litaendelea kuwakosa watu wenye maamuzi yenye manufaa kwa wananchi. Mbaya zaidi sijazisikia sauti za Wazawa ambao kwa hakika kabisa walipewa vitalu kwa mara ya kwanza toka Tanganyika huru. Simameni jamani, jitokezeni muuweke ukweli huu wazi na Watanzania wasiojua waelewe pumba na mchele.

Ni dhambi kubwa kumuacha Maige kujitetea mwenyewe kwa jambo alilolifanya kwa nia safi kuwanufaisha ninyi Wazawa.
Ericus Kimasha,

Nadhani humjui huyu Maige vizuri,Data zipo,na hata madudu aliyo yafanya yako wazi, achana na nyumba ni kwa manufaa yake, unadhani kampuni zilizo nyimwa vitalu ndani kuna watanzania wangapi wanao tegemewa na familia zao? Unatoa kwa mtu ambaye hata hajuio wageni anapata lini je ni kuijenga nchi au. Usikurupuke, nyumba ni ya kwake na maisha kama aliipata kwa njia anazo jua yeye sawa, si tuanalilia maslahi ya watanzania wenzetu ambao wanapunguzwa kazi.
 
Last edited by a moderator:
Watanzania hasa vijana, kwa ufahamu wangu na udadisi juu ya Politics, Power Strugle and Economy naomba nisimame kuhesabiwa miongoni mwa watakao dumu daima upande wa utetezi kwa Ezekiel Maige.

Mzimu mkubwa unaomwandama huyu Mtanzania si nyumba aliyonunua $0.7M cash au njia aliyotumia kupata hiyo pesa bali ujasiri wake kuvuluga syndicate ya waporaji wa maliasili zetu waliodumu kwenye sekta tangu miaka ya mwanzo wa 1960.

Na kubwa la pili ni malengo makubwa na dhamira ya dhati iliyokuwa ikijidhihirisha katika mafanikio yaliyokuwa yameanza kupatikana katika sekta ya Maliasili na Utalii. Maize asingeweza kuyafanya haya bila kuyagusa na kuyabatilisha maslahi makubwa na ya toka enzi ya wakubwa wa nchi hii. Wakubwa hao wengi wako nje ya serikali na hata nje ya nchi. Wananguvu za kubadilisha uongo kuwa ukweli na kinyume chake vilevile. Mwiko aliouvunja Maize ndo Ngeleja alidhani kwa kuuenzi nao watamuenzi kumbe haikuwa hivyo. Ngeleja hajavuluga maslahi ya mkubwa yeyote ila pale wao walipokula yeye kakomba mboga hadi kulamba mwiko.

Rai yangu kwa vijana wasimeze habari kama zinavyowekwa kwenye vyombo vya habari. Na katika yanayoitwa kashfa kuu kupitia kamati za Bunge msichukulie wajumbe kama Malaika na kudhani kila wanalotaarifu ndo ukweli. Hata marefa wana timu zao! Ukitaka kunielewa rejea mswada wa kuondoa kodi kwenye mafuta ya taa uone jinsi Bunge na Kamati zinavyotumika ki-udalali hata katika masuala nyeti.

Nikipata muda nitajitahidi nifumbue mafumbo zaidi labda vijana wenzangu mtanielewa. Hapa mimi si mjumbe wa Maige bali ni muathirika wa ukweli uliopindishwa. Kwa jinsi hii taifa litaendelea kuwakosa watu wenye maamuzi yenye manufaa kwa wananchi. Mbaya zaidi sijazisikia sauti za Wazawa ambao kwa hakika kabisa walipewa vitalu kwa mara ya kwanza toka Tanganyika huru. Simameni jamani, jitokezeni muuweke ukweli huu wazi na Watanzania wasiojua waelewe pumba na mchele.

Ni dhambi kubwa kumuacha Maige kujitetea mwenyewe kwa jambo alilolifanya kwa nia safi kuwanufaisha ninyi Wazawa.

Sio maige kweli wwewe? Mbona maelezo yako yanafanana na ya maige? Mna mkataba na uwaziri? Mkiukosa inakua nogwa?
 
Mbona mambo yatakuwa kama yale yale ya Basil Mramba na Daniel Yona?

Mahakamani Kisutu kila wiki na hakuna lolote. Sasa kwa hawa itakuwa ni TAKUKURU kila siku until doomsday!
 
Kuna umuhimu wa kutumia adhabu za wachina hapa tz ili tuwe na kumbukumbu juu ya utiifu wa sheria za nchi yetu.
 
Eti, haiwezekani wakatolewa hadharani kwa wananchi wenye hasira kali wakamaliza game? mbona vibaka wa simu na kuku huwa wanakutana na wananchi wenye hasira kali? hawa vipi hawaingii kwene category hii? laiti wezi wa kuku nao na wale wa simu wangekuwa wanachunguzwa na Takokuru haki ingepatikana bila ya ncha ya upanga
Elli,

Kwani ni nani anaowaleta hadharani haoo vibaka?! Wanaletwa na polisi, mahakama, au?!

TAKUKURU hawawezi kufanya hivyo, ila mimi na wewe tunaweza! TAKUKURU ni kansa, ni kansa isiyotibika iwe kwa mionzi ya X-Ray wala Gamma rays. Tiba dhidi ya TAKUKURU ni kukata kiungo kizima kilichoathirika! Kansa nyingine ni DPP, nae ni kansa mbaya na hatari kabisa kwa mustakabali wa taifa hili. Nayo ni kansa ambayo tiba yake ni kuondolewa kwa kiungo kizima! Kama kweli mtu amekutwa na Vogue 2 na mwingine amesafirisha benz kwa air cargo, yanini basi hadi leo hawajafikishwa mahakamani?! Mwizi akikamatwa tu, jambo la kwanza ni polisi ni siku chache baadae mahakamani ndipo anapotolewa kwa dhamana! Hawa tayari wana sifa zote za kufikishwa mahakamani......wapewe dhamana huko wakati uchunguzi zaidi ukiendelea! Lakini kwa HOssea huyu na mwenzake Feleshi yule yule, basi hamna lolote hapo la maana! Kesi sita kubwa za ufisadi ambazo Hossea alikuwa anazihubiri sijui zimeishia wapi!

Edward Hossea ni kansa. DPP ni kansa. DCI ni kansa pia! Madubashwa haya hayapo tayari kulinda maslahi ya walio wengi kwavile tu wamekata shauri la kujipendekeza kwa mabwana zao. Kama Al-Qaeda wangeweza kulipua TAKUKURU, Idara Ya Mashitaka ya Umma (chini ya DPP) na kisha kuwazuru watendaji wao wakuu; basi wala nisingeumizwa na shambulio hilo nchini mwetu.

Mbaya zaidi, wakina Mkulo wenyewe wanalindwa vizuri na dubwana na chinja chinja lingine linaloitwa Utawala Bora!! Utawala BOra ndani ya jamii yenye ukosefu mkubwa wa maadili....jamiii iliyojaa wezi, mafisadi, wala rushwa, wazinzi, wafiraji, wakosefu wa uwajibikaji! Utawala bora ndani ya jamii ambayo hata viongozi wake wa kiroho nao ni wezi, wazinzi, wala rushwa, mafisadi, wafiraji, wauza mihadarati na uchafu mwingine wote!

Siwezi kutarajia lolote la maana toka hapo!! Wenye uchungu na nchi hii tupiganie KATIBA YA KIDIKTETA. Katiba ya Kidikteta ambayo itafuta WESTERN GOOD GOVERNANCE na kuingiza APPROVED DICTATORSHIP GOVERNANCE. Ni katiba ya aina hiyo inayopaswa kuongoza jamii ya kifedhuli kama yetu. Tuwenayo angalau kwa miaka 20 ili iweze kuwarudisha mafedhuli kwenye mstari wa uungwana.
 
Last edited by a moderator:
Hivi hawa mawaziri na huwa wana kinga wawapo madarakani?

Inakuwaje nyendo zao hazichunguzwi kipindi wapo madarakani? Sababu hii taarifa zinaonyesha haya mambo hawakuyafanya baada ya kuondoka wizarani bali ni sehemu ya maisha yao walipokuwa pale.

Nashindwa kuelewa hii nchi ipo salama kwa kiwango gani... Hawa PCCB wanapswa wajiulize wanamsaidiaje rais na nchi.

Utata mwingine ni kitendo cha rais kutoa speech inayotafsirika kama vile anawalilia mawaziri wake kwa kusema wanaponzwa na watendaji wao na kuahidi safari hii ku deal na hao watendaji.

Nazidi kujiuliza kama hawa ndiyo rais alikuwa anawalilia au tumpe nafasi atuonyeshe wengine!

Majibu yapo kwenye mjadala wako
PCCB wanamsaidia raisi kwa kuwalinda hao jamaa na ndio maana wabunge walipomlazimisha awafukuze amewalilia
Sina hakika sana na usafi na udhati wa raisi wa kupambana na ufisadi
 
Baada ya kukutwa na tuhuma kama hizo ilibidi waende tu mahakamani. Takukuru ilikuwa wapi kugundua kama hawa jamaa wameihujumu taifa hili? Wanachunguza nin wakati ushahidi upo??? Ni ubadhilifu tu wa hela huo.kwani Takukuru ndio mahakama???
 
Back
Top Bottom