Congo
JF-Expert Member
- Mar 13, 2008
- 2,064
- 2,301
Kwanza, kama TAKUKURU inawachunguza kwa sababu ya kukutwa na magari tu basi itakuwa haijafanya kitu. Pili, naamini magari hayo ni tone tu katika bahari ya vitu walivyonavyo. Tatu, nawalaumu waandishi wetu wa Kitanzania kwa kutokuwa makini katika uchunguzi wao. Waandishi hawa wako wilayani, mikoani na nchi nzima kwa ujumla. Mtu anaiba, anajenga jumba kuuuuuuuuuuubwa lakini mwandishi anapita anachekelea, huenda anasuburi na yeye zamu yake ifike, aibe. Nyie waandishi investigative journalism mnayosema iko wapi? Mbona mnaweza kufanya investigative journalism hiyo kwa wacheza sinema na wanamiziki hapa Tanzania?