Mkullo kamdesa Kikwete?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,478
39,997
Hotuba ya Kikwete:

Jumla ya misaada na mikopo ya bajeti (GBS) katika kipindi cha Julai 2008 hadi Machi 2009 ilikuwa TSh milioni 869,563 ambazo ni asilimia 107 ya makadirio ya TSh milioni 812,113 zinazotegemewa kwenye bajeti ya mwaka 2008/09.

Hotuba ya Mkullo:

Mheshimiwa Spika, jumla ya misaada na mikopo ya bajeti
(General Budget Support - GBS) katika kipindi cha Julai 2008 hadi
Machi, 2009 ilikuwa shilingi milioni 869,563 ambazo ni sawa na
asilimia 115 ya makadirio ya shilingi milioni 757,722 katika kipindi
hicho.

Hotuba ya Kikwete:

Hii inatokana na baadhi ya wafadhili kutoa fedha zaidi ya walizoahidi kwenye bajeti na kushuka kwa thamani ya shilingi ya Tanzania dhidi ya dola ya Marekani.

Hotuba ya Mkullo:

Hii inatokana na baadhi ya Wahisani kutoa misaada na mikopo
zaidi ya makadirio ya awali, pamoja na kushuka kwa thamani ya
sarafu yetu dhidi ya Dola ya Kimarekani ikilinganishwa na makadirio
ya awali.

Hotuba ya Kikwete:

Hata hivyo, misaada na mikopo kwa ajili ya miradi ya maendeleo (ikijumuisha Mfuko wa Basket) kwa kipindi cha Julai 2008 hadi Machi 2009 ilifikia TSh milioni 866,412 sawa na asilimia 56 tu ya makadirio kwa mwaka 2008/09.

Hotuba ya Mkullo:

Aidha, misaada na mikopo kwa ajili ya miradi ya maendeleo
(ikijumuisha Mifuko ya Kisekta - Basket Funds) kwa kipindi cha Julai
2008 hadi Machi 2009 ilifikia shilingi milioni 867,564 sawa na asilimia
59 ya makadirio kwa mwaka 2008/09.


Hotuba ya Kikwete:

Tathmini ya mwelekeo wa bajeti kwa miezi tisa ya mwaka 2008/09 inaonyesha kuwa malengo ya sera za mapato hayatafikiwa kama ilivyopangwa.

Hotuba ya Mkullo:

Mheshimiwa Spika, tathmini ya mwenendo wa bajeti kwa
miezi tisa ya mwaka 2008/09 inaonesha kuwa malengo ya sera za
mapato hayatofikiwa kama ilivyopangwa.

Hotuba ya Kikwete:

Mapato ya ndani yanategemewa kufikia TSh milioni 4,248,858 ikiwa ni asilimia 10 chini ya lengo la TSh milioni 4,728,595.

Hotuba ya Mkullo:

Mapato ya ndani yanategemewa kufikia shilingi milioni 4,248,858 (trilioni 4.2) ikiwa ni asilimia 90 ya lengo la shilingi milioni 4,728,595 (trilioni 4.7).

Swali:

Mifano hiyo inatosha kusema mtu kadesa?

 
Kudesa ndo nini?

Na hiyo ya mwisho ni kitu kile kile kabisa. 10% chini ya lengo ni sawa na 90% ya lengo.
 
Hapa ndio nataka nijue walimu wetu wa chuo kikuu wanasemaje wakiona paper mbili zinavyolingana hivyo.
 
Huenda JK ndio alisoma bajeti kabla ya siku iliyopangwa! Au JK alikuwa na nia ya kumsafishia njia Mkullo.
 
Ahh kudesa ni plagiarism? Sasa hizo si facts, ulitake kila mmoja aje na zake? lol
 
Plagarism ni kujaribu kufanya kazi ya mtu mwengine ionekane kama kazi yako.
 
Sioni ajabu kushabihiana neno kwa neno kwa hizi hotuba mbili kwa maana uandishi wa hotuba serikalini uko hivi - Kiongozi akitaka kuzungumzia kitu, basi taasis husika huagizwa kuandika na kumpelekea huyo Mkuu.Kitakachokuwa kimetokea hapa ni kuwa aliyepewa jukumu kuandika kwa wote ni huyohuyo mtu mmoja/watu haohao.Kwa vile nao hawakufikiria kuwa itang'amuliwa kama alivyong'amua MKJJ, basi wakatoa ilivyo.
 
Sioni ajabu kushabihiana neno kwa neno kwa hizi hotuba mbili kwa maana uandishi wa hotuba serikalini uko hivi - Kiongozi akitaka kuzungumzia kitu, basi taasis husika huagizwa kuandika na kumpelekea huyo Mkuu.Kitakachokuwa kimetokea hapa ni kuwa aliyepewa jukumu kuandika kwa wote ni huyohuyo mtummoja/watu haohao.Kwa vile nao hawakufikiria kuwa inatang'amuliwa kama alivyong'amua MKJJ, basi wakatoa ilivyo.

Nafahamu hilo na ni wazi kuwa waandishi watakuwa ni wale wale:

a. Mkullo alipokuwa anatumia maneno yale yale yaliyotumiwa na Kikwete alikuwa anamnukuu kikwete au alitaka yajulikane kama ni maneno yake?

b. Mimi nikiamua kuyanukuu nitasema ni maneno hasa ya nani? Kwa sababu kwanza niliyasikia kwa Kikwete ambaye niliamini ni maneno yake.
 
Ingekuwa tatizo iwapo hizi hotuba zisingefanana. Kufanana kwake ni sawa na kulitarajiwa. Viongozi wa serikali hiyohiyo wanapozungumzia swala hilohilo hatutarajii taarifa tofauti.
Cha msingi ni kwamba pamoja na content kufanana hotuba haijachukuliwa word to word.
 
Wakati wew unamuuliza Kang, wikipedia na dictionary havikuwepo?
Mipasho mipasho mipasho, halafu?

Kumbe mmemshtukia wengi!! :) Hakuna kubeza hapa, labda alete definition yake anayoijua mwenyewe.
Sidhani kama kuna mtu anafikiri Kikwete anakaaga ikulu na calculator anaanza kuhesabu hizi asilimia, data zote zinatoka sahemu moja so lazima zifanane.
 
Kwakuwa Mkulo kama waziri wa fedha ndiye aliyetakiwa kusoma hiyo hotuba ya bajeti, NADHANI Kikwete ndiye aliyedesa hotuba ya Mkulo na kuwahi kuisoma.
 
Back
Top Bottom