The Evil Genius
JF-Expert Member
- Mar 21, 2014
- 5,466
- 17,308
Juzi hapa Rais alipofanya mahojiano na Tido Mhando alisema Magufuli alikua anaendesha miradi kwa mikopo na mikopo mingine ya gharama sana.
Wanasiasa uchwara kama Zito wamewahi kumsema Magufuli kwamba amekua akichukua mikopo kwenye taasisi za fedha za kibiashara kama Benki za Suisse Credits, Standard Chartered Bank nk kwamba hiyo mikopo ni ya gharama sana kwani ina riba kubwa kwa sababu ni ya kibiashara.
Watu hao wakashauri kwamba mikopo ilitakiwa ichukuliwe kwenye taasisi za kimataifa kama IMF ana WB ama AfDB nk kwani wao hutoa concessional loans ama mikopo ya gharama nafuu.
Mimi binafsi nakubaliana na hoja zao kwamba IMF ama WB wana mikopo ya gharama nafuu na pia credit/grace period yao hua ni kubwa sana kuanzia miaka 5 na kuendelea kutegemeana na mazungumzo yenu.
Naomba kuuliza, je huu mkopo kutoka EXIM Bank ya India ambao umechukuliwa kwenye bank ya biashara mbona sisikii ukisemwa au wenyewe ni mkopo wa bei rahisi?
Tusisahau serikali ya JK ilikopa kutoka EXIM Bank ya China kujenga bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Kinyerezi wenye gharama kubwa sana ambao tutaulipa kwa miaka zaidi ya 10 na bomba lenyewe linatumika kwa 6% na kuiacha TPDC na deni la zaidi ya Trilioni 2 ambazo iwe isiwe lazima sisi watanzania tutalipa tu.
Tukubaliane kwamba mikopo ya kibiashara ni mikopo ya hovyo haijalishi nani anaingia mikataba ila nashangaa sisikii wataalamu wetu uchwara wakiponda hii ya mama, ama kisa tu walikua na chuki na Magufuli? Sijui.
Je, ni kwanini tumekopa kwenye benki ya kibiashara na hatukukopa WB ma IMF ambao wana Gharama ndogo za mikopo ama wametugomea kutokana na kua na mzigo mkubwa wa madeni? Je deni letu sio sustainable tena?