Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 234
Wadau;
Habari nilizopata kutoka rafiki yangu aliye Kahama anasema Dr mkombozi wetu amepata mapokezi makubwa mjini humo jana (Jumapili) ambayo hayapata kutokea hapo.
Anasema ingawa alichelewa kidogo na kutinga saa 11.15 jioni umati mkubwa ulikuwa bado unamsubiri katika uwanja huo na alikwenda moja kwa moja jukwaani. Vifijo, vigelegele na vifijo, vikiambatana na kelele za BYE BYE KIKWETE, BYE BYE CCM zilisikika wakati anaingia.
Akihutubia alisikitishwa na manyumba duni (ya tembe) ambayo wananchi wengi bado wanayo baada ya miaka hamsini ya maendeleo yanayodaiwa kuletwa na CCM.
Alisema watu ni masikini sana wilaya hiyo pamoja na kwamba wanakalia eneo la migodi miwili mikubwa ya dhahabu Bulyanhulu na Buzwagi. Alishangaa kwa nini kila mgodi katika hiyo inachangia sh milioni 200 tu kila mwaka kwa hakmashauri ingawa kila mmoja unapishana katika uzalishaji.
Alisema tofali moja (gold bullion) la tofali la dhahabu lingeweza kusomesha watoto wa wilaya hiyo bure kuanzia shule za msingi hadi chuo kikuu.
Alimshambulia JK kwa kutoa ahadi za uongo zisizokuwa na mantiki. Alisema JK anapotoa ahadi kwamba atatengeneza barabara anadanganya tu, kwani kazi ya serikali ni kutengeneza barabara kwa sababu ndiyo inakusanya kodi. Alishangaa kuona kwamba JK anaifanya hiyo kuwa ahadi ya kampeni. Slaa alisema hivyo huku wananchi wakimshangilia kwa nguvu.
Awali alipokuwa maeneo ya vijijini, wananchi walikuwa wanamzuia barabarani ili awaslimie na awahutubie na alikuwa anafanya hivyo, ndiyo maana ya kuchelewa mkutanoni.
Kuhusu mgombea wa ubunge, rafiki yangu huyo alisema mgombea wa CCM, James lembeli yuko katika hali mbaya sana na dalili kubwa ni kwamba atapoteza kiti hicho kwa yule wa Chadema.
Rafiki yangu anasema Lembeli amekonda sana shauri ya mawazo ya kushindwa ingawa yeye anasema atashinda tu kwani kukonda kwake siyo sababu.
Hali kadhalika mgombea wa CUF katika jimbi jirani la Msalala naye amemkalia vibya mgombea wa CCM Maige na dalili ni kwamba atakipoteza kiti hicho.
====
UPDATES - PICHA