Elections 2010 Mkombozi Slaa apokelewa kwa kishindo Kahama

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
233

Wadau;

Habari nilizopata kutoka rafiki yangu aliye Kahama anasema Dr mkombozi wetu amepata mapokezi makubwa mjini humo jana (Jumapili) ambayo hayapata kutokea hapo.

Anasema ingawa alichelewa kidogo na kutinga saa 11.15 jioni umati mkubwa ulikuwa bado unamsubiri katika uwanja huo na alikwenda moja kwa moja jukwaani. Vifijo, vigelegele na vifijo, vikiambatana na kelele za BYE BYE KIKWETE, BYE BYE CCM zilisikika wakati anaingia.

Akihutubia alisikitishwa na manyumba duni (ya tembe) ambayo wananchi wengi bado wanayo baada ya miaka hamsini ya ‘maendeleo’ yanayodaiwa kuletwa na CCM.

Alisema watu ni masikini sana wilaya hiyo pamoja na kwamba wanakalia eneo la migodi miwili mikubwa ya dhahabu – Bulyanhulu na Buzwagi. Alishangaa kwa nini kila mgodi katika hiyo inachangia sh milioni 200 tu kila mwaka kwa hakmashauri ingawa kila mmoja unapishana katika uzalishaji.

Alisema tofali moja (gold bullion) la tofali la dhahabu lingeweza kusomesha watoto wa wilaya hiyo bure kuanzia shule za msingi hadi chuo kikuu.

Alimshambulia JK kwa kutoa ahadi za uongo zisizokuwa na mantiki. Alisema JK anapotoa ahadi kwamba atatengeneza barabara anadanganya tu, kwani kazi ya serikali ni kutengeneza barabara kwa sababu ndiyo inakusanya kodi. Alishangaa kuona kwamba JK anaifanya hiyo kuwa ahadi ya kampeni. Slaa alisema hivyo huku wananchi wakimshangilia kwa nguvu.

Awali alipokuwa maeneo ya vijijini, wananchi walikuwa wanamzuia barabarani ili awaslimie na awahutubie na alikuwa anafanya hivyo, ndiyo maana ya kuchelewa mkutanoni.

Kuhusu mgombea wa ubunge, rafiki yangu huyo alisema mgombea wa CCM, James lembeli yuko katika hali mbaya sana na dalili kubwa ni kwamba atapoteza kiti hicho kwa yule wa Chadema.

Rafiki yangu anasema Lembeli amekonda sana shauri ya mawazo ya kushindwa ingawa yeye anasema atashinda tu kwani kukonda kwake siyo sababu.

Hali kadhalika mgombea wa CUF katika jimbi jirani la Msalala naye amemkalia vibya mgombea wa CCM – Maige na dalili ni kwamba atakipoteza kiti hicho.

====
UPDATES - PICHA

slaa_in_kahama.jpg

bango_nzega.jpg

bango_salma.jpg

slaa_nzega_kahama.jpg

Lembeli aliacha kazi TANAPA akakimbilia ufisadini na sasa unamrudi tartiibu. Doctor the Presida come 1/11/2010
 
.... hakuna haja ya kutembea na wasanii na wengine wanaume wamevaa gauni ili kupata watu wa kuhutubia. Wananchi wanahaja ya kujua mustakabali wa nchi yao na sio mbwembwe za wasanii. Huko ni kufirisika kifikra. Hata Mwalimu Nyerere wakati anadai ukombozi wa nchi hii hakuwa na wasanii bali hoja za msingi kwa Watanganyika.

CHAGUA CHADEMA!!!!
 
Asante kwa taarifa nimeambiwa pia leo anaunguruma shinyanga mjini Mbele ya MWASISI wa CHadema Bob Nyanga Makani.
 
Ahadi za Kikwete za ajabu sana. Ni kama mwalimu aseme mkinipa kazi ya ualimu nitafundisha, daktari atatibu watu, etc etc.
 
Lembeli aliacha kazi TANAPA akakimbilia ufisadini na sasa unamrudi tartiibu. Doctor the Presida come 1/11/2010

Mwenzake Dk Mlingwa yamemfika. Alikuwa Mkurugenzi wa TAWIRI,akakimbilia siasa, miaka mitano katemwa (Shinyanga mjini). Sasa hivi sijui yuko wapi?
Mambo ya siasa bwana, we acha tu!
 
Fantastic. Nakwambia hata watu wa vijijini si wale wa mwaka 2005. Pamoja na vitisho vya CCM wameshatambua ya kuwa wameonewa sana, wameibiwa sana, wamedanganywa sana, wamefanywa kuwa maskini sana na sasa ni wakati wao wa kusema hapana kwa mafisadi CCM.

Kikwete awe fair tu na watu wake akubali haki itendeke awe rais mstaafu ataheshimika sana na si kutaka kurudi ikulu kwa mabavu.
 
Mwenzake Dk Mlingwa yamemfika. Alikuwa Mkurugenzi wa TAWIRI,akakimbilia siasa, miaka mitano katemwa (Shinyanga mjini). Sasa hivi sijui yuko wapi?
Mambo ya siasa bwana, we acha tu!

Labda amerudi kufundisha pala UDSM, Zoology walioko pale wanaweza kutupa taarifa kama yupo hapo au la.
 
Alisema watu ni masikini sana wilaya hiyo pamoja na kwamba wanakalia eneo la migodi miwili mikubwa ya dhahabu – Bulyanhulu na Buzwagi. Alishangaa kwa nini kila mgodi katika hiyo inachangia sh milioni 200 tu kila mwaka kwa hakmashauri ingawa kila mmoja unapishana katika uzalishaji.

Alisema tofali moja (gold bullion) la tofali la dhahabu lingeweza kusomesha watoto wa wilaya hiyo bure kuanzia shule za msingi hadi chuo kikuu.

Alimshambulia JK kwa kutoa ahadi za uongo zisizokuwa na mantiki. Alisema JK anapotoa ahadi kwamba atatengeneza barabara anadanganya tu, kwani kazi ya serikali ni kutengeneza barabara kwa sababu ndiyo inakusanya kodi. Alishangaa kuona kwamba JK anaifanya hiyo kuwa ahadi ya kampeni. Slaa alisema hivyo huku wananchi wakimshangilia kwa nguvu.

Asante sana Dr. Slaa kwa kuja kutukomboa kwenye minyororo ya utumwa wa CCM
 
Hakuna kisicho na mwisho. Amekuja yule aliyeibua uozo wa viongozi wa CCM bungeni. Huyu ndiye rais wetu kwani anatujali na alikubali kukejeliwa na mafisadi kwa sababu ya watanzania. DR Peter Slaa KARIBU IKULU UTUONGOZE baada ya kupelekwa vichochoroni na kutelekezwa na CCM. Ahadi za JK zinaonyesha Kuchanganyikiwa na kukosa la kusema kwani naye anajua hawezi kufanya yoote.

CCM na MAFISADI wanainuka wanainama wanaona haya haooooo:dance::dance::dance:
 
safiii,natamani watanzania wafumbue macho waone wanavo danganywa na huyu mutu
 
Asante kwa taarifa nimeambiwa pia leo anaunguruma shinyanga mjini Mbele ya MWASISI wa CHadema Bob Nyanga Makani.

Ndo maana jana wachakachuaji wa WA KIKWETE wamekimbilia huko shinyanga, CCM TUNAWAFUATILIA MGUU KWA MGUU, JICHO KWA JICHO, SIKIO KWA SIKIO, JARIBUNI MWAKA MWINGINE.....

TUTA APPEAL MPAKA MBINGUNI KWANI USHAHIDI UTAKUWEPO LOL

TRUST ME.... MIMI NI MWANA CCM ILA KIKWETE BASI

NACHAGUA MTU SIO CHAMA
 
Dr. Slaa ndiye dawa ya umaskini wa Watanzania, na ndiye dawa ya mafisadi. Tuhamasishe vijana na wazee vijijini wasiache kumpigia kura Dr. Slaa siku ya uchaguzi 31 Oktoba, 2010.
 
Mwenzake Dk Mlingwa yamemfika. Alikuwa Mkurugenzi wa TAWIRI,akakimbilia siasa, miaka mitano katemwa (Shinyanga mjini). Sasa hivi sijui yuko wapi?
Mambo ya siasa bwana, we acha tu!

Heshima kwako Nyumbu,

Mkuu Mlingwa ni rafiki yangu wa karibu sana tangu akiwa mkurugenzi TAWIRI.Kwasasa Mlingwa yuko Njiro[Msolla] nyumbani kwake anasoma magazeti tangu asubuhi mpaka jioni mambo yake si mabaya sana ana Landrover moja anaitumia kwa shughuli za utalii si unajua tena Arusha watalii wengi kipindi hiki.

Mlingwa anategemea kujiunga Sokoine University kama mwalimu mwakani uongo mbaya elimu yake nzuri hawezi kulala njaa lakini inataka moyo from deputy minister hadi mwalimu !,siasa wakati mwingine inaweza kukuangusha vibaya hadi mbwa unaowafuga wakakudharau.
 
Hili la mbwa ni hatari......yule Mattaka aliposimamishwa kazi na Mkapa alikuwa na majibwa 3 makubwa...waya ukawasababisha kuhama nyumba na kuhamia jirani...jamaa alipoendakujaribu kuyarudisha nusura yamtoe roho
 
Je kama Slaa angekuwa anaambatana na vikundi vya Bongo Fleva na watumbuizaji wengine plus usafiri wa bure, UMATI wa watu ungekuwaje?? Ingebidi waweke vikosi vya uokoaji kila anapopita kuepusha madhara ya kuumizana kwa kukanyagana.
 
1st post updated with photos from Kahama/Nzega

Mkuu;

Niko hapa kwa watani wa jadi. Umati huo kwenye Picha umenipa matumaini makubwa sana. narudi tarehe 30-11 kupiga kura yangu isipotee.

Kama noma na iwe noma!
 
Nimependa hilo Bango Kampuni ya Mama Salma inataka ubunge Nzega ha ha wananchi safari hii ni Kiboko
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom