Mke wangu kaniletea shoga yake nitembee naye!

yani unashindwa ona wazi kwamba mkeo na shoga yako wako pamoja. mkeo ana mtu wake tena nadhani kakuchoka. hebu kuna kichwa kidogo utaelewa mpango mzima
 
Kwa taarifa yako mkeo ana mwanaume bora na mwenye akili kuliko wewe.
 
kaka unapoteza muda na huyo rafii wa mkeo, mkeo atakuwa na bwana nnje hana semina hana chochote kakolea na dushelele la nje,,jiulize kwanini hataki ujue NGO yao ikowapi, kwanini hataki mwende wote..hebu umiza akili acha kuwa ----, unless kama na wewe umekolea kwa hicho kimeo
 
Hii nayo ni akili ya kianalogia mkuu hukuizima na mitambo yake tare1/1/2013 ass sita kamili usiku?? Pole sana kama umeingia nayo mwaka huu.UNAKWENDA NAYE PEKU AU NA KINGA? NA JE UMEPIMA???? MKEO KUNA JAMBO ANAKUFICHA KESHAOLEWA HUYO NDUGU YANGU BADILI AKILI YAKO IFIKIRI KIDIGITAL ZAIDI NDUGU ACHANA NA NANLOGIA .

Bravoooooooo, imetulia
 
Mke wangu amejiunga na VICOBA na pia NGO moja ya mambo ya kuwawezesha wanawake kibisahara. Amekuwa akisafiri mara kwa mara kwenda mikoani kwenye semina za hiyo NGO yao. Nimekuwa nikilalamika sana kuhusu hiyo tabia yake mpaka tukapelekana kwa wazazi na akaahidi hatosafiri tena.

Miezi miwili iliyopita amenijulisha kwamba amepewa cheo kwenye NGO yao na atalazimika kusafiri sana hivyo kuna shoga yake ndiye atakuja kunipikia na kulala hapo nyumbani kila akisafiri ili kunihudumia mimi na watoto. Nilipinga sana wazo lake lakini akasema hawezi kuacha kusafiri kwa sababu anapata marupurupu kwa ustawi wa familia jambo ambalo si kweli maana tangu ajiunge na hiyo NGO sijaona lolote la maana zaidi ya mavazi ya gharama anayojinunulia.

Tatizo hataki hata siku moja nitembelee NGO yao wala nisafiri naye, mie ni mtumishi serikalini, lakini siwezi kunyimwa hata ruhusa ya wiki moja ili nisafiri naye.
Mabishano yetu hayakupata muafaka na matokeo yake siku aliposafiri, shoga yake akaja pale nyumbani na kufanya shughuli zote zipaswazo kufanyw ana mke na niliporudi usiku nilimkuta sebuleni akinisubiri. Aliniandalia maji ya kuoga na kisha chakula na wakati nakula alikuwa amekaa pale sebuleni akiangalia TV huku tukizungumza.

Tuliishi hivyo kwa wiki nzima hadi mke wangu akarudi na yule shoga yake aliondoka na kurudi kwake. (Huyu dada hajaolewa ila amezaa na jamaa flani huko kwao Songea na mtoto yuko kwa wazazi wake. Hapa mjini anaishi peke yake akijishughulisha na biashara ya kukopesha nguo za kike). Mke wangu aliniuliza kama shoga yake hakumuangusha, yaani alikuwa anaihudumia familia vizuri, nikamjibu kwamba hakuwa na tatizo.

Wiki mbili baadaye mke wangu akaaga anasafiri tena kwenda Dodoma kwenye semina na atakaa kule kwa wiki mbili, hivyo shoga yake atakuja tena kukaa pale nyumbani hadi atakaporudi. Sasa wiki moja tangu mke wangu aondoke tuliishi vizuri tu, lakini wiki ya pili huyu bibie kaanza kunitega na kama mjuavyo wanawake wako smart sana, nilijitahidi sana kukwepa mitego, lakini sikufua dafu, akanidaka tena ilikuwa sebuleni watoto wote walikuwa wamelala.

Naomba nikiri kwamba huyu mwanamke alikuwa ni hodari kweli kweli maana nadhani alikuwa anajua ninachokikosa kwa mke wangu. Tangu siku hiyo alikuwa analala chumbani kwangu mpaka alfajiri ndio anarudi chumbani kwake.
Mke wangu aliporudi nilisikitika sana, maana nilitamani asafiri tena, kutokana na kunogewa na penzi la shoga yake. Hivi sasa tumeendea kukutana mara kwa mara maeneo ya mbali na huyu shoga wa mke wangu na kwa kweli ameniteka kabisa yaani namuwaza wakati wote na nimejikuta nikiwa simtamani mke wangu kabisa.

Lakini cha kushangaza mke wangu wala hajanishitukia na amekuwa akimuamini sana shoga yake kupita kiasi na siku hizi huwa anasafiri mara kwa mara tena huwa anakaa wiki mbili kila akisafiri na huyo shoga yake ndio kawa kama mke wangu, yaani kama dini yangu ingekuwa inaniruhusu ningemuoa awe mke wa pili.

Hebu wana JF niambieni, hivi mke wangu akijua atanilaumu kweli?

.......Tooooooooooooooba! yakhe....ukila vya watu na vyako vyaliwa!
 
nakumbuka msemo wa mkuu wa kaya *ukitaka kula, lazma uliwe* sasa ww dalili zote za kuliwa zinaonekana, hvyo mi sion tatizo kama na wewe unakula, lkn mwishon lazma kitaeleweka.
 
yani unashindwa ona wazi kwamba mkeo na shoga yako wako pamoja. mkeo ana mtu wake tena nadhani kakuchoka. hebu kuna kichwa kidogo utaelewa mpango mzima

Nahisi kitu kama hicho.Kwa nini mke akatae kusafiri na mumewe? Kwa nini aruhusu shoga yake aje kutoa huduma kwa mumewe na na watoto alale hapo nyumbani?. Anajiamini nini?
 
mkeo kakupa shoga yake utembee nae wala sio kwa bahati mbaya bali hiyo ni planned. ukimbana vizuri huyo shoga wa mkeo atakupa siri zote za mkeo. inaonekana mkeo ana mwanaume mwingine na ndio maana hataki usafiri nae na pili kakupa huyo shoga yake. mimi nijuavyo wanawake wako makini kuchunga waume zao wasiibiwe. mimi mke wangu yuko makini sana na house girl asiwe karibu na mimi. kama hayupo karibu nami anampiga marufuku house girl asiangalie TV pamoja nami. sasa je wewe na huyo mkeo!!!
 
we ulishaachika siku nyingi, ila mkeo akamwambia shoga yake kama anakumaind amlengeshee ili yy awe huru na NGO yake , cha msingi mkeo wa zamani anakujali hakutaka huanguke kihoro ukisikia habari zake, we weka mambo hadharani uone, ataondoka na kurudi kama mpambe wa rafiki yake kwenye harusi yenu bomani kwa mkuu wa wilaya.
 
Angalia sana isije ikawa na mkeo pia nae anakokwenda kwenye hizo safari na ana mtu wake huko, aiwezi kuingia akilini kwa mwanamke mwenye kumjali na kumpenda mme wake akulete shoga yake akuhudumie wewe wkt yeye huko safarini. Yaani Fisi anapewa kulinda Bucha kweli, Karibu mwaka 2013. Hii kama yakutunga vile, ila samahani km ntakuwa nimekukwaza huo ni mtazamo tu .Mwisho achana na huyo shoga wa mkeo na boresha ndoa yako mkuu
 
mkeo kakupa shoga yake utembee nae wala sio kwa bahati mbaya bali hiyo ni planned. ukimbana vizuri huyo shoga wa mkeo atakupa siri zote za mkeo. inaonekana mkeo ana mwanaume mwingine na ndio maana hataki usafiri nae na pili kakupa huyo shoga yake. mimi nijuavyo wanawake wako makini kuchunga waume zao wasiibiwe. mimi mke wangu yuko makini sana na house girl asiwe karibu na mimi. kama hayupo karibu nami anampiga marufuku house girl asiangalie TV pamoja nami. sasa je wewe na huyo mkeo!!!

kweli kabisa mkuu " uchungu wa mme ajue ni mkwe na kinyume chake pia" mimi wa kwangu hataki hata ndugu zake kike niwe na nao karibu na kuwazoea kivile, sebuse wewe una sema shoga

dah asa mkuu kuajiriwa serikalini na story ya jamaa vinawiana vipi?
Hata mimi namshangaa huyu mkuu, serikalini wameajiliwa watu wa vyama vote ila hawana kadi tu, lkn wanapenzi na vyama vyao mbalimbali vya siasa mkuu

Mke wangu amejiunga na VICOBA na pia NGO moja ya mambo ya kuwawezesha wanawake kibisahara. Amekuwa akisafiri mara kwa mara kwenda mikoani kwenye semina za hiyo NGO yao. Nimekuwa nikilalamika sana kuhusu hiyo tabia yake mpaka tukapelekana kwa wazazi na akaahidi hatosafiri tena.

Miezi miwili iliyopita amenijulisha kwamba amepewa cheo kwenye NGO yao na atalazimika kusafiri sana hivyo kuna shoga yake ndiye atakuja kunipikia na kulala hapo nyumbani kila akisafiri ili kunihudumia mimi na watoto. Nilipinga sana wazo lake lakini akasema hawezi kuacha kusafiri kwa sababu anapata marupurupu kwa ustawi wa familia jambo ambalo si kweli maana tangu ajiunge na hiyo NGO sijaona lolote la maana zaidi ya mavazi ya gharama anayojinunulia.

Tatizo hataki hata siku moja nitembelee NGO yao wala nisafiri naye, mie ni mtumishi serikalini, lakini siwezi kunyimwa hata ruhusa ya wiki moja ili nisafiri naye.
Mabishano yetu hayakupata muafaka na matokeo yake siku aliposafiri, shoga yake akaja pale nyumbani na kufanya shughuli zote zipaswazo kufanyw ana mke na niliporudi usiku nilimkuta sebuleni akinisubiri. Aliniandalia maji ya kuoga na kisha chakula na wakati nakula alikuwa amekaa pale sebuleni akiangalia TV huku tukizungumza.

Tuliishi hivyo kwa wiki nzima hadi mke wangu akarudi na yule shoga yake aliondoka na kurudi kwake. (Huyu dada hajaolewa ila amezaa na jamaa flani huko kwao Songea na mtoto yuko kwa wazazi wake. Hapa mjini anaishi peke yake akijishughulisha na biashara ya kukopesha nguo za kike). Mke wangu aliniuliza kama shoga yake hakumuangusha, yaani alikuwa anaihudumia familia vizuri, nikamjibu kwamba hakuwa na tatizo.

Wiki mbili baadaye mke wangu akaaga anasafiri tena kwenda Dodoma kwenye semina na atakaa kule kwa wiki mbili, hivyo shoga yake atakuja tena kukaa pale nyumbani hadi atakaporudi. Sasa wiki moja tangu mke wangu aondoke tuliishi vizuri tu, lakini wiki ya pili huyu bibie kaanza kunitega na kama mjuavyo wanawake wako smart sana, nilijitahidi sana kukwepa mitego, lakini sikufua dafu, akanidaka tena ilikuwa sebuleni watoto wote walikuwa wamelala.

Naomba nikiri kwamba huyu mwanamke alikuwa ni hodari kweli kweli maana nadhani alikuwa anajua ninachokikosa kwa mke wangu. Tangu siku hiyo alikuwa analala chumbani kwangu mpaka alfajiri ndio anarudi chumbani kwake.
Mke wangu aliporudi nilisikitika sana, maana nilitamani asafiri tena, kutokana na kunogewa na penzi la shoga yake. Hivi sasa tumeendea kukutana mara kwa mara maeneo ya mbali na huyu shoga wa mke wangu na kwa kweli ameniteka kabisa yaani namuwaza wakati wote na nimejikuta nikiwa simtamani mke wangu kabisa.

Lakini cha kushangaza mke wangu wala hajanishitukia na amekuwa akimuamini sana shoga yake kupita kiasi na siku hizi huwa anasafiri mara kwa mara tena huwa anakaa wiki mbili kila akisafiri na huyo shoga yake ndio kawa kama mke wangu, yaani kama dini yangu ingekuwa inaniruhusu ningemuoa awe mke wa pili.

Hebu wana JF niambieni, hivi mke wangu akijua atanilaumu kweli?

Mkuu pole lakini hapo ukiona hivyo ujue hata mamsap aliaanza mapema hako kamchezo wako ndo mana hashughuliki yeye kusafiri na mavazi ya garama ujue kitu iliendelea long time . shtuka ufanye maamuzi NGO kuna mambo.
 
We endelea tu kumsifia mwanamke bogus kama huyo...usinifanye niamini mpo ndani ya meli moja.

utashaaaaaaaaaaa!
Kwani.mwanaume hapa sio bogus? Hivi mwanaume mzima na kengele zake analetewe mke wa kukaimu na mkewe anae anaona sawa? Ana ulemavu gani hadi wanae walale na shosti wa mkewe?
 
Back
Top Bottom