Mke wangu kaniletea shoga yake nitembee naye!

Tegelezeni

JF-Expert Member
Dec 31, 2009
268
124
Mke wangu amejiunga na VICOBA na pia NGO moja ya mambo ya kuwawezesha wanawake kibisahara. Amekuwa akisafiri mara kwa mara kwenda mikoani kwenye semina za hiyo NGO yao. Nimekuwa nikilalamika sana kuhusu hiyo tabia yake mpaka tukapelekana kwa wazazi na akaahidi hatosafiri tena.

Miezi miwili iliyopita amenijulisha kwamba amepewa cheo kwenye NGO yao na atalazimika kusafiri sana hivyo kuna shoga yake ndiye atakuja kunipikia na kulala hapo nyumbani kila akisafiri ili kunihudumia mimi na watoto. Nilipinga sana wazo lake lakini akasema hawezi kuacha kusafiri kwa sababu anapata marupurupu kwa ustawi wa familia jambo ambalo si kweli maana tangu ajiunge na hiyo NGO sijaona lolote la maana zaidi ya mavazi ya gharama anayojinunulia.

Tatizo hataki hata siku moja nitembelee NGO yao wala nisafiri naye, mie ni mtumishi serikalini, lakini siwezi kunyimwa hata ruhusa ya wiki moja ili nisafiri naye.
Mabishano yetu hayakupata muafaka na matokeo yake siku aliposafiri, shoga yake akaja pale nyumbani na kufanya shughuli zote zipaswazo kufanyw ana mke na niliporudi usiku nilimkuta sebuleni akinisubiri. Aliniandalia maji ya kuoga na kisha chakula na wakati nakula alikuwa amekaa pale sebuleni akiangalia TV huku tukizungumza.

Tuliishi hivyo kwa wiki nzima hadi mke wangu akarudi na yule shoga yake aliondoka na kurudi kwake. (Huyu dada hajaolewa ila amezaa na jamaa flani huko kwao Songea na mtoto yuko kwa wazazi wake. Hapa mjini anaishi peke yake akijishughulisha na biashara ya kukopesha nguo za kike). Mke wangu aliniuliza kama shoga yake hakumuangusha, yaani alikuwa anaihudumia familia vizuri, nikamjibu kwamba hakuwa na tatizo.

Wiki mbili baadaye mke wangu akaaga anasafiri tena kwenda Dodoma kwenye semina na atakaa kule kwa wiki mbili, hivyo shoga yake atakuja tena kukaa pale nyumbani hadi atakaporudi. Sasa wiki moja tangu mke wangu aondoke tuliishi vizuri tu, lakini wiki ya pili huyu bibie kaanza kunitega na kama mjuavyo wanawake wako smart sana, nilijitahidi sana kukwepa mitego, lakini sikufua dafu, akanidaka tena ilikuwa sebuleni watoto wote walikuwa wamelala.

Naomba nikiri kwamba huyu mwanamke alikuwa ni hodari kweli kweli maana nadhani alikuwa anajua ninachokikosa kwa mke wangu. Tangu siku hiyo alikuwa analala chumbani kwangu mpaka alfajiri ndio anarudi chumbani kwake.
Mke wangu aliporudi nilisikitika sana, maana nilitamani asafiri tena, kutokana na kunogewa na penzi la shoga yake. Hivi sasa tumeendea kukutana mara kwa mara maeneo ya mbali na huyu shoga wa mke wangu na kwa kweli ameniteka kabisa yaani namuwaza wakati wote na nimejikuta nikiwa simtamani mke wangu kabisa.

Lakini cha kushangaza mke wangu wala hajanishitukia na amekuwa akimuamini sana shoga yake kupita kiasi na siku hizi huwa anasafiri mara kwa mara tena huwa anakaa wiki mbili kila akisafiri na huyo shoga yake ndio kawa kama mke wangu, yaani kama dini yangu ingekuwa inaniruhusu ningemuoa awe mke wa pili.

Hebu wana JF niambieni, hivi mke wangu akijua atanilaumu kweli?
 
Hii nayo ni akili ya kianalogia mkuu hukuizima na mitambo yake tare1/1/2013 ass sita kamili usiku?? Pole sana kama umeingia nayo mwaka huu.UNAKWENDA NAYE PEKU AU NA KINGA? NA JE UMEPIMA???? MKEO KUNA JAMBO ANAKUFICHA KESHAOLEWA HUYO NDUGU YANGU BADILI AKILI YAKO IFIKIRI KIDIGITAL ZAIDI NDUGU ACHANA NA NANLOGIA .
 
Tegelezeni kwanza ule jirani yako na wakeze waliishia wapi/?

hiii nayo nzuri kweli kuitungia kitabu.
 
Last edited by a moderator:
Yawezekana mkeo pia kakabidhiwa mwenza wa kusafiri naye ndiyo maana hashtuki.
Linda ndoa kaka,utamu huo upo mpaka utafikiwa kaburini...kuwa na msimamo,ila kama huijali ndoa basi endelea kula shoga.
 
Hivi bado tu unaongelea dini wakati hakuna dini inayo ruhusu kuzini nje ya ndoa.

Mgoni huyo mana hao kwa viuno, kama wamakonde.

Pole sana.

Wewe kweli unawafahamu, yaani kabinti kanayajua mambo kama nini.
Kaminifanya nisimtamani kabisa mke wangu.
 
Mh huyo mkeo anawezaje kumuamini shoga yake hivo,,we mwenyewe unajua
uyafanyayo si sawa,,mwambie mkeo kila kitu na umuombe msamaha mtafute suluhisho.
Hao watoto unawalea kwenye mazingira gani??
 
Du kweli,huoni kama ni hatari kwa afya yako na watoto pia,kwani ukivumilia kwa mda itakuwaje?huku ukitafuta solution ya kudumu,UNATUMIA KINGA ??
 
...unaweza ukadhani ni NGO kumbe ni "NGO"
...angalia mkuu, inawezekana kuna watu wanakula kiulaiiini. Mke gani asie na wivu.
Chunguza vizuri. Nahisi unaibiwa.
 
Kwanza inaonyesha wewe mwenyewe ni mume -----,hapo inatumika ile style ya(ng'ata na kupuliza)yani mkeo anagawa nje na wewe anakupoza kwa hilo shangingi,kwanza inaonyesha hilo shangingi,kwanza lina masirahi na 'uboho'wako.
 
Sioni swali hapo, ushauri wangu. kama wakati mwingine akirudi safarini mtume akasabahi mkoani akirudi mpe safari nyingine ilimradi awe busy na wewe uwe busy na huyo rafiki.... hahaaa
 
Kalagabao ujue na mkeo nae akienda seminar inakula kwako...na usikute semina zenyewe hazipo ni uzushi tu
 
Back
Top Bottom