Mke wa mshikaji wangu aniduwaza!

Uchungu wa mke anaujua mume na uchungu wa mume anaujua mke. usithubutu kufanya kitu ambacho ukifanyiwa ww utaumia
 
Huyo mtu hawezi kukupenda kuliko mumewe aliyemfanya awaache wazazi wake walio mzaa na kumkuza kwa upendo na kwenda kuishi na huyo mume. Kwako anataka tu kulipiza kisasi au kumuumiza mumewe, na kama anataka mumewe aumie, ipo siku atafanya vyovyote vile ili mumewe ajue ili aumie sasa itakapotokea hivyo ndipo utakapojuta kuzaliwa. Asikudanganye hamna siri katika katika kisasi, tunza heshima ya rafiki yako na kulinda ndoa yake. Kuwa serious, acha kupokea simu yake wala kujibu sms, usiende nyumbani kwake, kutana na rafiki yako juu kwa ju.

ushauri wako umetulia auzingatie

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
unajua wanawake ni viumbe wa ajabu sana. na akikataa atamwambia mumewe kuwa jamaa alimtongoza akamkatalia ili amchonganishe kabisa na jamaa. hii dunia ngumu sana hasa unapokutana na masaibu kama haya na wewe sio firauni

mie ndio maana sipendi urafiki na opposite sex maana a simple platonic hug can trigger lust between the two. bora mwanamke anijue kuwa mie mgegedaji from the start so she knows wat she is getting sio urafiki wakati nataka kumgegeda
 
ha, ha,haaaa. tatizo ni kwamba mke wa jamaa yako unakuwa umesogezwa naye karibu na mshikaji wako
 
ha, ha,haaaa. tatizo ni kwamba mke wa jamaa yako unakuwa umesogezwa naye karibu na mshikaji wako

ata kama...wee weka distance tuu..mambo yakukumbatiana hamna mambo sijui kuzoea nyumbani kwa jamaa hapana...kuonana na shem ni katika need to see basis
 
dawa yake ndogo sana uyo..muignore usijibu chochote na nenda uso kwa uso mchane liveeeeee..that thing will demonize u.
 
Ndugu yangu. Usisikilize huyo Mwanamke hata akueleze mabaya 1000 ya mumewe fikiria kama anaweza kumsaliti mumewe wewe je? atashindwa kukusaliti? pia mapenzi kujificha ni mwanzoni lakin muda unavyozidi kwenda mtashtukiwa tu.
 
ahha dnt twist the story bwana...sasa mambo ya kabang umeyatoa wapi...plus this guy had it coming...u got to treat ir wife well bwana mpaka mwanamke atoke nje ndugu yangu mume kafanya kitu kibaya sana...wanawake wavumilivu sana na kwambia mpama mke atoke ujue in most cases mume amemtenda vibaya

ni ww kweli au kuna mtu kaiba id
 
Usije ukafanya hicho kitu katika maisha yako maana utakijutia siku zote ulizobakiza hapa duniani, epukana na huyo shemejio kwa gharama yeyote mkuu...! Ni hayo tu..
 
kama njiwa anajiita chinja unaogopa nn hata mm ilishanitokea mpaka leo ananiheshemu
 
Mie nakushauri achana nae kabisa,
Tena ikiwezekana mtamkie kwa ukali huyo mwanamke na uweke msisitizo kuwa kitu kama hicho hutafanya kamwe.
 
kama vp tokanae 2 maana utapo mwaacha hatakuona na ww kama mshikaji wako pia anaweza kufanya chochote kama utamkatalia
 
Jana nimeduwazwa sana baada ya mke wa rafiki yangu kunitamkia wazi kuwa ananipenda na anataka kutoka na mimi.
Tangu nifahamiane naye miaka takribani mitano sasa tumekuwa tukiheshimiana naye sana kama mashemeji. mwaka huu akaniambia kuwa mumewe ameanza kubadilika kwa kuzidisha ulevi, kuchelewa kurudi nyumbani na wakati mwingine kulala nje na pia alizifuma meseji za mapenzi kwenye simu ya mumewe kutoka kwa mtu aliyemsave kwa jina la kiume, hivyo nimsaidie kumshauri ili abadilke ila akanionya nisimwambie kama ni yeye ndiye kaniambia.

Nilimtia moyo kuhusu hali hiyo na kumwomba awe mvumilivu na asichoke kuongea na mumewe kuhusu hali hiyo ili abadilike. Binafsi nilipata wakati mgumu wa namna gani nitamshauri jamaa bila kumtajia makosa yake na wapi nimeyapata hivyo nikashindwa hiyo kazi.

Mke wa jamaa akaanza kunipigia simu usiku kulalamika kila mumewe anapochelewa kurudi na wakati mwingine akinipigia alfajiri kuniambia kuwa mumewe hajarudi hadi muda huo. Niliendelea kumtia moyo ingawa mambo hayo yalikuwa ni ya kweli.

Cha ajabu kuanzia wiki jana amekuwa akinitumia meseji za mapenzi, nikajua ni hizi meseji ambazo watu hutumiana hivyo sikujali sana hadi pale aliponiandikia akiniambia kuwa yuko serious anataka kutoka na mimi. Sikuamini nikampigia simu kusikia sauti yake kama ni yeye kweli, ndipo aliponithibitishia kuwa yuko serious na atatunza siri na kunitunzia heshima yangu kwa jamaa kwani tayari moyo wake umeangukia kwangu.

Sikuweza kumjibu kitu kwa namna nilivyopatwa na mshangao. hadi sasa anaendelea kunibembeleza na kunipa mbinu nyingi za kutimiza lengo lake bila kujulikana na watu.

Binafsi sina lengo la kumsaliti mshikaji wangu ila nimelileta kwenu ili mnishauri nimjibu vipi huyu mwanamke ili heshima yangu kwa familia hii iendelee kuwapo na pia kusitokee chuki yoyote kutokana na kadhia hii itakayopelekea urafiki wangu na familia hii kuyumba au kupotea.
[/QUOTJana nimeduwazwa sana baada ya mke wa rafiki yangu kunitamkia wazi kuwa ananipenda na anataka kutoka na mimi.
Tangu nifahamiane naye miaka takribani mitano sasa tumekuwa tukiheshimiana naye sana kama mashemeji. mwaka huu akaniambia kuwa mumewe ameanza kubadilika kwa kuzidisha ulevi, kuchelewa kurudi nyumbani na wakati mwingine kulala nje na pia alizifuma meseji za mapenzi kwenye simu ya mumewe kutoka kwa mtu aliyemsave kwa jina la kiume, hivyo nimsaidie kumshauri ili abadilke ila akanionya nisimwambie kama ni yeye ndiye kaniambia.

Nilimtia moyo kuhusu hali hiyo na kumwomba awe mvumilivu na asichoke kuongea na mumewe kuhusu hali hiyo ili abadilike. Binafsi nilipata wakati mgumu wa namna gani nitamshauri jamaa bila kumtajia makosa yake na wapi nimeyapata hivyo nikashindwa hiyo kazi.

Mke wa jamaa akaanza kunipigia simu usiku kulalamika kila mumewe anapochelewa kurudi na wakati mwingine akinipigia alfajiri kuniambia kuwa mumewe hajarudi hadi muda huo. Niliendelea kumtia moyo ingawa mambo hayo yalikuwa ni ya kweli.

Cha ajabu kuanzia wiki jana amekuwa akinitumia meseji za mapenzi, nikajua ni hizi meseji ambazo watu hutumiana hivyo sikujali sana hadi pale aliponiandikia akiniambia kuwa yuko serious anataka kutoka na mimi. Sikuamini nikampigia simu kusikia sauti yake kama ni yeye kweli, ndipo aliponithibitishia kuwa yuko serious na atatunza siri na kunitunzia heshima yangu kwa jamaa kwani tayari moyo wake umeangukia kwangu.

Sikuweza kumjibu kitu kwa namna nilivyopatwa na mshangao. hadi sasa anaendelea kunibembeleza na kunipa mbinu nyingi za kutimiza lengo lake bila kujulikana na watu.

Binafsi sina lengo la kumsaliti mshikaji wangu ila nimelileta kwenu ili mnishauri nimjibu vipi huyu mwanamke ili heshima yangu kwa familia hii iendelee kuwapo na pia kusitokee chuki yoyote kutokana na kadhia hii itakayopelekea urafiki wangu na familia hii kuyumba au kupotea.[:yell::yell::yell::yell::yell:E] chagua moja kama kusuka au kunyoa
 
Usijaribu maana utajutia for the rest of your life. Cheza na chochote si mke wa mtu. Unaweza kujiona shujaa kwa kumpigia mwenzio lakini ukikamatwa utatamani uffffeee
 
acha tamaa na ulafi wa kimapenzi ebu mshinde shetani katika hilo tafuta movie ya jetli ya the defender uone jinsi jetli alivyomshinda shetani katika suala kama hilo la kwako.

what you hates to be done to you by others dont do it to others.
 
Pamoja kwamba jamaa anachepuka, ukweli hayuko tayari 'kupigiwa' mke wake: sikushauri ujiingize katika 'uhusiano feki' huo kwani vita ake ni mbaya!
 
Back
Top Bottom