Wana JF Nakusalimieni
Kuna demu 1 niko naye kama miezi 5 sasa, ambaye nimepanga kufunga naye ndoa. Kabla sijachukua uamuzi wa kufunga ndoa nimekuja kwenu kupata nasaha zenu. Huyu mke mtarajiwa kuna kazi amepata sasa ni mwezi wa pili. Kitu kinachonipa wasiwasi sana ni kuwa wakati wa kwenda kazini huwa anajipodoa kupita kiasi, anajiweka marangi usoni (makeup) na nguo anazovaa kazini ni za mitego mitego. Nishawahi kumuuliza kwa nini anjiremba sana na kuvaa namna hiyo kazini, akanijibu kuwa sio peke yake anafanya hivyo, na kazini kwao anatakiwa avae vizuri na apendeze. Sasa wana JF nakuombeni mnijibu ni kweli haya majibu nilopewa? Huyu demu yuko serious na mimi?? Kabla sijachukua uamuzi wa kufunga ndoa. Mbarikiwe wana JF