“Mke Anajipodoa sana wakati wa kwenda kazini”

Boflo

JF-Expert Member
Jan 20, 2010
4,384
4,408
Wana JF Nakusalimieni

Kuna demu 1 niko naye kama miezi 5 sasa, ambaye nimepanga kufunga naye ndoa. Kabla sijachukua uamuzi wa kufunga ndoa nimekuja kwenu kupata nasaha zenu. Huyu mke mtarajiwa kuna kazi amepata sasa ni mwezi wa pili. Kitu kinachonipa wasiwasi sana ni kuwa wakati wa kwenda kazini huwa anajipodoa kupita kiasi, anajiweka marangi usoni (makeup) na nguo anazovaa kazini ni za mitego mitego. Nishawahi kumuuliza kwa nini anjiremba sana na kuvaa namna hivyo kazini, akanijibu kuwa sio peke yake anafanya hivyo, na kazini kwao anatakiwa avae vizuri na apendeze. Sasa wana JF nakuombeni mnijibu ni kweli haya majibu nilopewa? Huyu demu yuko serious na mimi?? Kabla sijachukua uamuzi wa kufunga ndoa. Mbarikiwe wana JF
 
Haha.....mbavu sina Boflo
Hapo mimi naona kama unaibiwa, kazi gani hiyo ya kuvaa kimtego tego?
 
Yaani mnafanya uasherati cna ushauri zaidi ya kwenda kuokoka haraka kabla cku mbaya hazijafika
 
Haha.....mbavu sina Boflo
Hapo mimi naona kama unaibiwa, kazi gani hiyo ya kuvaa kimtego tego?

Asante, na mimi hapo ndipo napatwa na wasiwasi, Mke wangu wa kwanza niliachana naye baada ya kugundua ninagongewa. Sasa hivi nataka niwe makini sana
 
Kujipodoa wakati wa kwenda kazini siyo tatizo sana, ni tabia ya akina dada walio wengi. Haiwezekani aende kazini akute wenzake wamependeza halafu yeye awe mchafu mchafu, si jambo zuri.

Ila kama kujipodoa huku kumezidi sana na akaendelea kupiga vimini vilivyozidi kiasi, hapo ni muhimu ukae naye chini na kumueleza kuwa wewe kama husband wake mtarajiwa, haupendelei yeye avae mavazi yasiyo ya heshima na kujipodoa kupita kiasi. Kama kweli ni mwanamke mzuri atakutii, ila kama bado yako wangu wangu anaweza kuku-ignore.

Pia angalia namna alivyopata hiyo kazi na mahusiano yake na hao wafanyakazi wenzake. Uwe makini na mwenye busara kwenye maamuzi yako isije ikawa ni wivu unakusumbua! :A S embarassed:
 
Wana JF Nakusalimieni

Kuna demu 1 niko naye kama miezi 5 sasa, ambaye nimepanga kufunga naye ndoa. Kabla sijachukua uamuzi wa kufunga ndoa nimekuja kwenu kupata nasaha zenu. Huyu mke mtarajiwa kuna kazi amepata sasa ni mwezi wa pili. Kitu kinachonipa wasiwasi sana ni kuwa wakati wa kwenda kazini huwa anajipodoa kupita kiasi, anajiweka marangi usoni (makeup) na nguo anazovaa kazini ni za mitego mitego. Nishawahi kumuuliza kwa nini anjiremba sana na kuvaa namna hiyo kazini, akanijibu kuwa sio peke yake anafanya hivyo, na kazini kwao anatakiwa avae vizuri na apendeze. Sasa wana JF nakuombeni mnijibu ni kweli haya majibu nilopewa? Huyu demu yuko serious na mimi?? Kabla sijachukua uamuzi wa kufunga ndoa. Mbarikiwe wana JF

Umeshasema ni DEMU wako basically huwezi
kumuoa na ndo maana unaona kupendeza kwake ni kasoro kwako.
Tafta mchumba bana achana na MADEMU.
 
Wewe si ulipenda hizo hizo gear sasa walialia nini...waache wenzako pia watoe taka za macho kama si za mwili
 
Wana JF Nakusalimieni

Kuna demu 1 niko naye kama miezi 5 sasa, ambaye nimepanga kufunga naye ndoa. Kabla sijachukua uamuzi wa kufunga ndoa nimekuja kwenu kupata nasaha zenu. Huyu mke mtarajiwa kuna kazi amepata sasa ni mwezi wa pili. Kitu kinachonipa wasiwasi sana ni kuwa wakati wa kwenda kazini huwa anajipodoa kupita kiasi, anajiweka marangi usoni (makeup) na nguo anazovaa kazini ni za mitego mitego. Nishawahi kumuuliza kwa nini anjiremba sana na kuvaa namna hiyo kazini, akanijibu kuwa sio peke yake anafanya hivyo, na kazini kwao anatakiwa avae vizuri na apendeze. Sasa wana JF nakuombeni mnijibu ni kweli haya majibu nilopewa? Huyu demu yuko serious na mimi?? Kabla sijachukua uamuzi wa kufunga ndoa. Mbarikiwe wana JF

Atakuwa anafanya kazi mapokezi lazima ajipodoe awe kiburudisho kwa watu wanao fika katika afisi
 
Kujipodoa wakati wa kwenda kazini siyo tatizo sana, ni tabia ya akina dada walio wengi. Haiwezekani aende kazini akute wenzake wamependeza halafu yeye awe mchafu mchafu, si jambo zuri.

Ila kama kujipodoa huku kumezidi sana na akaendelea kupiga vimini vilivyozidi kiasi, hapo ni muhimu ukae naye chini na kumueleza kuwa wewe kama husband wake mtarajiwa, haupendelei yeye avae mavazi yasiyo ya heshima na kujipodoa kupita kiasi. Kama kweli ni mwanamke mzuri atakutii, ila kama bado yako wangu wangu anaweza kuku-ignore.

Pia angalia namna alivyopata hiyo kazi na mahusiano yake na hao wafanyakazi wenzake. Uwe makini na mwenye busara kwenye maamuzi yake isije ikawa ni wivu unakusumbua! :A S embarassed:

Well said!
 
Yaani mnafanya uasherati cna ushauri zaidi ya kwenda kuokoka haraka kabla cku mbaya hazijafika

Kasema wanafanya uasherati? Au kasema anademu(msichana kabla ya ndoa) wake anajipodoa sana? Kuwa muelewa wewe...
 
Kasema wanafanya uasherati? Au kasema anademu(msichana kabla ya ndoa) wake anajipodoa sana? Kuwa muelewa wewe...

Asante sana mkuu, Tungekuwa wana Jf wa aina yako, hapa jamvini kweli pangekuwa raha mustarehe!
 
Wivu unahusika kwenye mapenzi yakweli, lakni ukizidi sana ni soo mkuu... Tumia busara kumrekebisha...
 
Hakuna sehemu unayoambiwa uvae nguo za mitego zaidi ya kua mcheza show nadhani, kuvaa vizuri kazini ni sawa lakini sio hivyo anavyo vaa yeye, hao marangi yakiwa mengi nayo pia yanachusha usoni. kaanae chini mueleze avae nguo za heshima
kwani akivaa nguo za ajabu ajabu ndio ataongezwa cheo? sema nae kama hakusiki ujue ukioa atakupa shida sana na kuishi na mke ni raha sio karaha huyo anatakiwa awe mfano kwa watoto wenu sasa kama yeye ndio hivyo watoto watakuwaje?
 
Umeshasema ni DEMU wako basically huwezi
kumuoa na ndo maana unaona kupendeza kwake ni kasoro kwako.
Tafta mchumba bana achana na MADEMU.

Unaweza kunitajia stage ya mwanzo mpaka yamwisho kufikia mwanamke kumwita mkeo?? Na ukanipa tafsiri ya neno DEMU...?
 
Hakuna sehemu unayoambiwa uvae nguo za mitego zaidi ya kua mcheza show nadhani, kuvaa vizuri kazini ni sawa lakini sio hivyo anavyo vaa yeye, hao marangi yakiwa mengi nayo pia yanachusha usoni. kaanae chini mueleze avae nguo za heshima
kwani akivaa nguo za ajabu ajabu ndio ataongezwa cheo? sema nae kama hakusiki ujue ukioa atakupa shida sana na kuishi na mke ni raha sio karaha huyo anatakiwa awe mfano kwa watoto wenu sasa kama yeye ndio hivyo watoto watakuwaje?

Aante sana mkuu, I appreciate jibu lako mwanana
 
Me sioni shida mkuu, ni kawaida ya dada zetu wengi kupenda kurembaremba ili wapendeze na kweli wanapendeza. So Nitamshangaa mwanamke asiyetaka kupendeza!!!!!! Ujue kule kazini kwake wapo kinadada wengi nadhani ndo maana kasema "siyo peke yake" hii inaleta ushindani usio rasmi kazini. Mwache apendeze wewe. Kwanza hajawa wa kwako, mnasheratiana tu!!!!
 
Sema naye tu kwan huu ndio wakati wako wa kumshepu kwa namna ile unayotaka mkeo awe,
Naami kujipodoa sio ishu sn ila si kwa kiwango hicho km anaenda kichenpati,iwe simle tu,
Naamini km anakupenda na yuko sirias nawe atakusikiliza na kufuata kile kikupendezacho ww mume mtarajiwa,
Inawezekama bado hajaelewa na ww ndio unahusika kumweka sawa,tumia busara na kuwa muwazi kwake mapema ili akujue na kuamua kufanya maamuzi sahihi,

Nadhan kwa vile tayari ni mke mtarajiwa mpe heshima yake kwani jina ulilotumia sidhan km linamstahili mke mtarajiwa!
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom