Taarifa za uhakika kutoka Dodoma ndani ya Wabunge wa CCM ni kuwa kesho Ijumaa tarehe 09/6/2023 wametumiwa ujumbe wa wito wa kushiriki kikao cha Wabunge wa CCM - Party caucus Kwa ajili ya kuweka msimamo juu ya kupitisha azimio la mkataba wa Serikali na Dubai.
Kikao hiki kimeitwa siku moja kabla ya siku ya kupitishwa Kwa azimio la Bunge la kuridhia Mkataba huo ambao umesababisha sintofahamu kubwa katika jamii ya watanzania na hata jamii ya kimataifa.
Taarifa za ndani ya Wabunge wa CCM ni kuwa kuna mgawanyiko mkubwa miongoni mwao huku kundi moja likiweka bayana kuwa mkataba hauna Maslahi Kwa Taifa na lingine likisemwa kuwa kukataa kupitisha itatia aibu Chama chao hivyo Bora funika kombe Mwanaharamu apite!
Wabunge wanaopinga hoja zao ni zilezile za watanzania wazalendo kuhusu ubovu wa mkataba huo na umilele wake. Kundi hili linaongozwa na wabunge wawili kutoka majimbo ya DSM na kinara wao anatoka Mkoa wa Manyara! ( Majina kapuni ).
Watanzania kama kweli ni wazalendo wanashauriwa kuanzisha kampeni ya kuwapigia simu na jumbe (SMS) Kwa wabunge na kuwataka wakatae kupitisha azimio hilo kwani ni la hatari Kwa Taifa na usalama wa nchi.
Nitawajuza zaidi kwani Kwa sasa vikao viko kila sehemu Dodoma.
TIP: Kuna kundi la wabunge wanaopinga kuwa wabunge kutoka Zanzibar wasiwe sehemu ya kupitisha azimio hilo kwani rasilimali za Tanganyika ndio zinaenda kutolewa na hivyo kama wanataka kushiriki basi Bandari za Zanzibar ziwe sehemu ya mkataba huo.
More to follow, stay tuned!