Mkapa angewafaa zaidi Waislam Kuliko Kikwete

Status
Not open for further replies.
Kichuguu.
Acha kupanic tunaelimishana tu. Mawakili maarufu walikuwa Murtaza Lakha na ndugu yake Abbas Lakha,Kwikwima hawa walikuwa miaka ya 80.
Ndiyo nawafahamu hao, nimetaja baadhi yao tu na kumaliza kwa kusema na wengineo, wote walihusika sana na criminal law. Hizi taaluma nyingine hazikuwa na soko sana; Mkono pia hakuwa na soko katika taaluma yake ya Business Law.
MKONO alipewa tenda nyingi za serikali kwa nguvu za Nyerere, hilo halina ubishi.

Thibitisha maneno yako. Nyerere aliondoka madarakani mwaka 1985, ubinafasishaji ulianza kwa nguvu sana mwaka 1990, na ndipo Mkono alipoanza kupata utajiri, na kapata utajiri zaidi kwenye mikataba iliyosainiwa baada ya Nyerere kufariki. Nyerere aliingiaje pale.
Mzee JUMBE alikuwa na mtu wa sheria toka Ghana zaidi ya Dourado na hakuwa muislam jee udini unaingiaje hapo? huyo bwana alimuwekea wazi mapungufu ya katiba kisheria, alikuwa raia wa GHANA
Umesema mwanasheria mkuu wa kwanza wa Zanzibar alikuwa Mghana.
 
Safi sana tuendelee na mjadala.

Tido Mhando hajawahi kuongoza television wala kufanya kazi kwenye Television. hana uzoefu wala elimu full stop!
 
Kichuguu.

Mkono ana digrii moja sawa na Mabere Marando sikuelewi unasema ame specialize kwenye business law na wengine criminal.
kwenye kumbukumbu zangu sijawahi kuona specialization undergraduate.

ni sawa na daktari awe na digrii moja useme ni specailist.
 
Jitahidi kuwa unafanya utafiti kidogo kabla hujaanza malumbano. Kumbe unabisha vitu usivyo kuwa na uhakika navyo. Elimu ya Mkono ni kama ifuatavyo:

  • LL.B, University of East Africa, University College of Dar es Salaam, Tanzania, 1970.

  • MA (Bus. Law), Council for National Academic Awards, City of London Polytechnic , UK, 1976

Halafu ana certifications zihusuzo Business Law kama ifuatazo:

  • Fellow, Institute of Chartered Secretaries & Administrators, F.C.I.S., UK, 1986
  • Associate, Institute of Chartered Secretaries & Administrators, A.C.I.S., UK, 1976
  • Chartered Secretaryship Final Examination (C.I.S.), South West London College, UK, 1975

Kwa vile Criminal Law ni kama sheria ya msingi kabisa ambayo kila mwanasheria anaifahamau, ndiyo maana Mkono alimtetea Ditopile Mzuzuzuri. Lakini inapokuja kwenye kutetea serikali ya Tanzania dhidi ya City Water, hapo anatumia Business Law, na mteja makini hawezi kumpa kazi ya aina hiyo hiyo mwanasheria yeyote bila kujua umahiri wake kwenye Business Law.
 
Kichuguu.

Naona wewe ndio hufanyi utafiti wakutosha. huyo Mkono ana vyeti vya uongo. hakuna chuo kinaitwa South west London wala London city of Polytechnic. Naomba adress yao? nimefuatilia orodha ya vyuo vikuu UK hakuna chuo hicho.

South west London au unakusudia South Chelsea College chuo cha waNIGERIA cha kuongezea visa.
 
Kila mwanasiasa Tanzania ana vyeti vya uongo? Halafu walio wengi wanadai kuvipata nje ya Tanzania. Naanza kuingiwa na wasiwasi na baadhi ya "wataalamu" wetu waliosoma nje.
 
Kila mwanasiasa Tanzania ana vyeti vya uongo? Halafu walio wengi wanadai kuvipata nje ya Tanzania. Naanza kuingiwa na wasiwasi na baadhi ya "wataalamu" wetu waliosoma nje.

Ukitizama CV ya mkono utaona mashaka mengi sana. 1976 inaonesha alikuwa kwenye kozi mbili tofauti na taasisi mbili tofauti.
PIA M.A BUS LAW kitendawili kingine nilitarajia iwe L.L.M na hakuna sehemu inayosema ni specialist wa Business Law kama kichuguu anavyolazimisha watu tuamini.

mkono kama mwanasheria sio mkali ila kwa vile ana mtaji aliopewa na Nyerere ameeajiri mawakili wazuri kama dr.mapunda n.k
case ya city water hakuifanya yeye ali sub-contract kwa kampuni ya UK.
mkono hajui sheria. anakula na mahakimu.
 
South West London College of Law
Station House
11-13 Masons Avenue
Wealdstone, Harrow
Middlesex
HA3 5AH

Note: The name of South West London College of Law has been changed to Middlesex College of Law
Please click here to go to the new web site ....

http://www.middlesexcollegeoflaw.co.uk/

Thank you for visiting our website. Middlesex College of Law (formerly known as South West London College of Law) was established in 2000 to cater initially for students wishing to study in the United Kingdom with the aim of obtaining the LLB degree of University of London under the External Programme.

Since its inception, MCL has experienced a remarkable growth in its academic base, which is reflected in the extensive range of courses it now offers. These include not only courses in Law, but now covers Accounting, Business, Computing, Politics and International Relations, and Management. Given the additional space now available in our new premises in Harrow (north-west of London), MCL now caters for a wide range of pre-degree courses like GCE ‘A’ Levels and Diplomas as well as degree courses in law.

Our main objective is to equip students with the knowledge and skills required, not only to pass their examinations, but also to be able to deal effectively with the challenges expected of them when they start their working life.

It goes without saying that obtaining any of the degrees offered at MCL will open doors for you in various walks of life, which include executive and management positions where your peculiar skills will be in high demand. At MCL, we assist in organising visits to places of interest for our students throughout the country. This helps to ensure that everyone can gain maximum enjoyment from his or her stay at MCL.

Our lecturers are particularly committed to ensuring that our students are adequately prepared for their examinations, which takes place in June and December of every year (depending on your course).

Mission Statement
To create an educational environment, which meet the academic and intellectual needs of every student studying at MCL......

150 years of education provision
City of London Polytechnic’s new name is London Guildhall University. The Polytechnic of North London becomes the University of North London. 1996 University of North London celebrates its centenary.
 
Ukitizama CV ya mkono utaona mashaka mengi sana. 1976 inaonesha alikuwa kwenye kozi mbili tofauti na taasisi mbili tofauti.
PIA M.A BUS LAW kitendawili kingine nilitarajia iwe L.L.M na hakuna sehemu inayosema ni specialist wa Business Law kama kichuguu anavyolazimisha watu tuamini.

mkono kama mwanasheria sio mkali ila kwa vile ana mtaji aliopewa na Nyerere ameeajiri mawakili wazuri kama dr.mapunda n.k
case ya city water hakuifanya yeye ali sub-contract kwa kampuni ya UK.
mkono hajui sheria. anakula na mahakimu.

Kama mambo yataenda vizuri, mwaka 2010 utaona kwenye CV ya Mbowe kwamba katika kipindi kile kile amekuwa akifanya kozi mbili tofauti na vyuo viwili tofauti (vikiwa nchi tofauti). Huo ni mfano tu ambao ni hai kwa sasa hivi. Hii inaonyesha "ukali" wa ubongo wa mtu au siyo!!!!

Kilichonitua ni hiyo kwamba hivyo vyuo alivyovitaja kichuguu kwamba Mkono kasoma, wewe umesema kwamba havipo.
 
Kichuguu.

Naona wewe ndio hufanyi utafiti wakutosha. huyo Mkono ana vyeti vya uongo. hakuna chuo kinaitwa South west London wala London city of Polytechnic. Naomba adress yao? nimefuatilia orodha ya vyuo vikuu UK hakuna chuo hicho.

South west London au unakusudia South Chelsea College chuo cha waNIGERIA cha kuongezea visa.

Bado unamfuatilia Mzee Mkono? ngoja nikusaidie ufafanuzi ingawa kama wewe ni mtazannia na sasa unaishi London usingeshindwa kujua facts za vyuo alivyosomea mzee huyu kama ifuatavyo.

  1. Mwaka 1970, huyu mzee huyu alihitimu masomo yake "University of East Africa" kupitia "University College of Dar es Salaam." Leo hii University of East Africa haipo kwa vile ilivunjwa na kuwa university tatu za Makerere, Nairobi na Dar es Salaam. Na ile "University of College of Dar es Salaama" ndiyo leo inajulikana kama "University of Dar es Salaam".
  2. Mwaka 1976, alihitimu hapo "City of London Polytechnic", hata hivyo baada ya sheria mpya ya vyuo ya mwaka 1992, chuo hiki kilibadilisha jina na kuwa "London Guildhall University."
Nadhani umeelewa sasa; nakuomba kuwa unatafiti mambo kabla ya kuyaandika hasa kama yanahusu watu wengine kwa vile si vizuri kuchafua historia halali ya wenzio hata kama unawachukia.
 
Hao aika Tido ni watu wa maslahi,kwanza sifa kubwa ya Tido ni udini,pili ukabila.Alipokuwa BBC kawapa nafasi wa Tanga wenzie,pale alipoona hapa U Tanga peke yake hautoshi,ndio huvutia ktk dini,angalia TVT sasa hivi itakuwa ya wa Tanga,akina Said Yakub alipowaona hawa swahili akawabania,huyo ndio Tido.
Na ni kweli wakati wa nchi imetoka katika vita,nchi ina njaa huyu Tido alikuwa wapi?Tido jitu la MASLAH.
 
Bwana Kichuguu,

Chonde Chonde bwana!! Nadhani unafahamu huyu bwana kwa ukaribu sana!!!!!!
 
Ukitizama CV ya mkono utaona mashaka mengi sana. 1976 inaonesha alikuwa kwenye kozi mbili tofauti na taasisi mbili tofauti.
PIA M.A BUS LAW kitendawili kingine nilitarajia iwe L.L.M na hakuna sehemu inayosema ni specialist wa Business Law kama kichuguu anavyolazimisha watu tuamini.

Mtalii,

Tunarudi kule kule.
  1. CV ya Mzee Mkono inaonyesha kuwa akiwa London alisoma M.A (Business Law) mwaka 1976. Lakini kabla ya hapo alifanya mtihani wa C.I.S. hapo South West London College mwaka 1975 na kupasi kabla hajajiunga na City of London Polytechnic mwaka 1976: digrii ya masters ilikuwa kozi ya mwaka mmoja tu. Hakuhitaji kwenda chuoni kupata admission ya kuwa fellow au associate wa professional society yoyote. Kwa hiyo huo utata wa kusoma vyuo viwili mimi siuoni.
  2. Usibabaishwe sana na jina la digrii, wewe angalia contents za digrii hiyo. Nakupa mifano ya majina ya digrii ya masters katika engineering: Master of Engineering, Master of Science, Master of Science in Engineering, Master of of Applied Science in Engineering, Master of Engineering Science. Yote hayo ni majina yanayoweza kumaanisha digrii ya aina moja tu.
  3. Masters ya mzee Mkono ilifocus katika Business Law tu, kwa hiyo ni specialist wa business law; je unataka awe na mapembe ndipo ujue hivyo.
  4. Mojawapo ya fani ambazo huwa hazina ukihiyo ni uwakili. Huwezi kupewa uwakili na mahakama kabla haijathibitisha qualifications zako. Sasa kama wewe unahoji qualifications za mzee huyu ni afadhali uulize mahakama zote ambazo zinamruhuru kufanya shughuli za uwakili, na ni nyingi sana.
  5. Kama unakiri kuwa anaajiri wanasheria wazuri basi lazima ukiri kuwa yeye mwenyewe pia ni mwanasheria mzuri. Hakuna mwanasheria mzuri ambaye atakwenda kuajiriwa na mtu asiyejua sheria, badala yake ataanzisha kampuni yake mwenyewe.

Hata kama namchukia mtu, huwa naendelea kuheshimu qualifications zake halali. Ni kweli ningepiga kelele sana kama mzee huyu angekuwa na qualifications uchwara, lakini mzee wa watu anazo halali kabisa labda useme jingine.
 
Bwana Kichuguu,

Chonde Chonde bwana!! Nadhani unafahamu huyu bwana kwa ukaribu sana!!!!!!
Hapana simfahamu kwa karibu kiasi hicho, ila ninafahamu rekodi yake tu; ufahamu wangu kwake ni kama ninavyomfahamu Rais Kikwete au rais Bill Clinton.
 
Nungwi ni wa Mzumbe ipi - IDM au MU?

Was then IDM equivalent to Institute of Dev. Studies of UDSM?

Stands 2 b corrected.
 
Bado unamfuatilia Mzee Mkono? ngoja nikusaidie ufafanuzi ingawa kama wewe ni mtazannia na sasa unaishi London usingeshindwa kujua facts za vyuo alivyosomea mzee huyu kama ifuatavyo.

  1. Mwaka 1970, huyu mzee huyu alihitimu masomo yake "University of East Africa" kupitia "University College of Dar es Salaam." Leo hii University of East Africa haipo kwa vile ilivunjwa na kuwa university tatu za Makerere, Nairobi na Dar es Salaam. Na ile "University of College of Dar es Salaama" ndiyo leo inajulikana kama "University of Dar es Salaam".
  2. Mwaka 1976, alihitimu hapo "City of London Polytechnic", hata hivyo baada ya sheria mpya ya vyuo ya mwaka 1992, chuo hiki kilibadilisha jina na kuwa "London Guildhall University."
Nadhani umeelewa sasa; nakuomba kuwa unatafiti mambo kabla ya kuyaandika hasa kama yanahusu watu wengine kwa vile si vizuri kuchafua historia halali ya wenzio hata kama unawachukia.

Uliambiwa mapema: "Tuelimishane." Sasa kama wewe umeamua kutoa 'tuition' ya bila malipo usianze kulalama. Unakumbuka? Mwanzo ilikuwa hivi: "kwanza huyu Mkono alipendelewa na Nyerere kwa ukabila na udini." Wakatajwa na watu wengine, akina Sinde Warioba, Opio, n.k.

It is a fishing expedition - tupa kokolo, linase kila aina ya samaki. Au tupa tope, litanasa litakapoangukia.

Bahati mbaya ni kwamba hata ufundishe vipi, mwanafunzi aliyekwishapindisha mawazo yake kivyake ni vigumu sana kuibadili. Jaribu kufundisha 'algebra' kwa mtu asiyependa aina hiyo ya hesabu uone kama utafika popote; hata kama mwalimu anasifiwa kuwa mzuri kiasi gani.
 
Wana JF,
Niliuliza huko nyuma, kuna sensa au utafiti wowote kuonyesha idadi ya Watanzania kwa dini zao? Ulifanyika lini na ulifanywa na asasi gani?

Hata hivyo, nimewahi kudokezwa kuwa baada ya Uhuru, Mwalimu alizuia karatasi za sensa ya watu kuwa na kipengele cha dini ya mhesabiwaji. Niliambiwa kuwa alifanya hivyo kuzuia baadhi ya wananchi, kudai (au kutamba) kwa takwimu, kuwa wafuasi wa dini fulani ni wengi kuliko wa dini nyingine; hiyo yote ikiwa ni kupunguza kasi ya hisia za udini.
 
Mwanagenzi,
Ninayo sensa ya mwaka 1967. Hii inaonyesha bayana makabila na dini. Kuna wakati akina Mwinyi walikuwa wanasema Waislamu ni 80%
ya raia wote wa Tanzania, Mwalimu akawambia watangaze matokeo ya sensa ya 1987. Wakakaa kimya.
P.S. Ukitaka nikutumie ile ya 67 kama attachment nibeep.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom