Mkapa angewafaa zaidi Waislam Kuliko Kikwete

Status
Not open for further replies.
Nungwi,
Sielewi wasi2 wa watu ni nini kujadili usawa katika uteuzi. Nina wasi2 hili swala upendeleo wa kundi moja ktk dini Tanzania litakuja kututumbukiza katika matatizo/machafuko siku zijazo. Waislam wanaona- ila wananyamaza- na istoshe ndo wengi kwa idadi!
Tanzania Bara sii sawa na Kenya au Uganda ambapo idadi ya Waislamu ni ndogo ukilinhanisha na Wakristo!
Ni bora tujadili haya mambo -watu wazoee -sidhani jawabu kama ni kunyamaza!
 
seniority kwenye ngazi ya judiciary ni jambo la muhimu sana...pale referal court the most senior supreme judges ambao wangekuwa eligble kuwa cj ni big.gen [retired] augustino ramandani,judge mrosso,judge lubuva,judge eusebio munuo na jaji kiongozi manento...majaji wa rufaa na mahakama kuu wamepangwa kwa namba kutokana na seniority[mfano ramandani alikuwa akijulikana kama JR 1..namba mbili baada ya JM....na kuendelea.hadu JR 11..namba zao hupanda kadiri wanavyositaafu au vinginevyo...kwa kuzingatia seniority protocal ya kujoin supreme court au high court..
kule kwenye bench la mahakama kuu kuna dadi J 50...sasa nimeangalia cv ya judge othman inalipa...huyu jaji mkuu bada ya kama miaka minne atakuwa amefikia retirement at any cost kwani hadi sasa amebakisha miaka miwili ya kustaafu kwa lazima na yupo eligible kwa extention ya two years contract..sasa kama muungwana akitaka kumpa othman ujaji mkuu ..itabidi ampe ujaji kiongozi ndani ya hii miaka miwili[since any judge kwenye bench anaweza kuchaguliwa kuwa jaji kiongozi na jaji mkuu]...then ampe ujaji wa supreme [since jaji mkuu anaweza kutoka kwenye bench la supreme au jaji kiongozi....so kwa kuwa bado ni kujana he is still a material and let us give him minimum of another five years ..if we want to think of him as CHIEF JUSTICE..although hata kuwa jaji peke yake ni heshima kubwa sana.
HATA jeshini mkuu wa majeshi lazima achaguliwe kutoka kwenye rank ya brig general kuendelea although mara nyingi au zote hutoka kati ya kundi la ma MAJ GENERALS...hii ni kwa sababu nchi hii ina system nzuri na ina amani so ni vigumu rais kukosa imani na senior officers ambao wako eligble kwa uteuzi akakosa hata mmoja wa kumwamini hadi aanze kutafuta makanali wakuwapandisha kuwarusha ngazi nne kama wanavyoweza kufanya marais wa nchi zisizokuwa stable..
upande wa polisi naona mara nyingi makamishana wa makao makuu wamerukwa sana kwenye uteuzi..mara zote maris wame prefer ma RPC...KUANZIA mzee mwinyi alimrusha ngazi HAROUN MAHUNDI kutoka RPC ARUSHA hadi IGP..Akafuatia mzee mkapa akamrusha OMAR MAHITA kutoka RPC arusha hadi IGP....NA KUWAACHA makamishna wa makao makuu wanashangaa..MUUNGWANA kamrusha SAID MWEMA ambaye alikuwa RPC mbeya [then seconded to interpal ] kuwa IGP na kusababisha kizaazaa kwa kuingia na makamishana wapya kabisa even tibaigana was not commissioner before...

seniority...
 
Kichuguu.

Bob Makani unasema hakupewa kwa vile hakuwa na digrii ya uchumi. mbona Mtei alipewa akiwa na Literature? wakati Makani ana sheria ambayo kidogo inafanana.

Baada ya Nyirabu alikuja Rutihinda kuwa gavana, huyo alikuwa na Political Science na International Relations.

Nadhani Makani hakupewa kwa dini yake lazima tukubali Mwalimu alivyokuwa Mdini.

Back 2 Warioba kuwa alikuwa na Qualification ndio akapewa uwaziri mkuu,na Jaji Chande ana Qualification zaidi ya Warioba au Augustino Ramadhani.sasa unataka tuamini kuwa Qualification ni kigezo, wakati jana ulisema kuwa SENIORITY ndio kigezo. mkuu sikuelewi kabisa!Chande ana exposure kubwa sana ambayo hana Warioba wala Jaji mkuu mpya.

Nakurudisha UDSM nyumbani kwako. wakati anatafutwa Dean wa Faculty ya Commerce and Management- Assad Mussa akamshinda vibaya Chijoriga kwa qualification na Seniority, akapita kwenye interviews zote. lilipofika File kwa Luhanga-VC wenu akampa bibi Chijoriga kwa madai ya Gender. hili limelieleza sana kwenye Mada ya Mzumbe VS UDSM nenda kwenye elimu utaona.

U-TURN ya Luhanga kuwa ni Gender imetoka wapi? mtu akija na Qualfication kama Chande unasema unataka Seniority. ikija Seniority kama DR.Assad unasema GENDER ISSUE and Globalization.

Warioba alipewa uwaziri mkuu kwa upendeleo kigezo cha elimu hakihusu kwa cheo cha uwaziri mkuu. ndio maana unaona Sumaye alipewa madaraka hayo huku akiwa hana elimu. baada ya kumaliza Uwaziri mkuu ndio amekwenda kusomea Management skills, wakati alitakiwa awe na Knowledge hiyo kabla ili apply kwenye uwaziri mkuu wake.

Na kwa taarifa yenu Course work na Dissertation amefanyiwa na vijana wa kikenya.

Nawaomba WaTanzania tusibaguane wote wapewe vyeo. kama balance ya Muungano inatazamwa why not ya Dini?

Nungwi
Kuna kitu kingine kwenye sheria lazima Upractice zikae kichwani, ndugu yetu Chande alikwenda Nje ya Nchi, so utakuta ktk kipindi hicho atakuwa amepitwa na mabadiliko ya Sheria kadha wa kadha za Bongo, so alivyo pewa Ujaji wa Mahakama Kuu Mbeya alipewa ili apate nafasi ya kuzipitia na kuzitumia kwa kutoa hukumu, sasa hata tutakapo mpa huo Ujaji Mkuu atakuwa in a better position ya kuwa reference aidha kwa hukumu atakazo kuwa ametoa au hata ktk mazungumzo na wenzake. na hata yeye mwenyewe sio mjinga alivyo kata huo uteuzi un, na kuamua kubaki bongo, tena mbeya, maana wengine wangependa kuwa Dari salamu au Arusha au Mza..
Huyo Assad wa UDSM sio lazima tumpe hapo , tunaweza kumpa U commisssioner TRA, Capital Markets etc , kama sasa hivi ni one of the board member NSSf.So Nungwi vitu vingine tusiharakishe. Ndio Maana hata Kikwete Tulimpa Foreign Affairs for ten years ili apate exposure zaidi na kuondo tamaa ndogo ndogo za masurufu na safari za nje. Atleast alipokuwa Foreign Affairs alikuwa anapata wasaa wa kupanda Tube train, kupita mitaa amayo ukiwa Raisi huwezi kupita.
sasa just imagine angechaguliwa Uraisi wakati ule halafu anataka kuingia Casino au kupanda underground itakuwaje na msafara wa Protocol Officers wake?
 
Nungwi,

Huwezi kuwatetea waislam hadi uwe muislam? kwa hiyo mtazamo wako asiye kuwepo na lake halipo? tuwe tunajadili issue hata kama hatuzipendi ila zina maslahi ya Taifa. nilipopost mada hii niliomba tuchangie kuona weakness zetu. sasa nimebatizwa kuwa ni Talaban.kwa taarifa tu mimi ni Sabato.

Nakubaliana na wewe mia kwa mia kama tutaweza kuzijadili issues na kuona weakness za watu badala ya rangi za watu kutafuta weakness inayotokana na rangi hiyo!.. Hapo juu umesema kuwa ni mimi ninasema:- Asiyekuwepo na lake halipo!...
Laa hasha ni wewe unayesema hivyo kuwa kwa sababu waislaam wapo basi na lao lazima liwepo! hapa umejaribu kupindisha hoja yako.
Na pale niliposema mtu unafahamu maana ya Taliban ama kukuita wewe ustadhi ni lazima uwe muislaam hapana ndugu yangu hii ni lugha ya kiarabu ambayo hutumika kwa kizazi cha pwani. labda niombe samahani kwa kufikiria kuwa wewe ni mtu wa pwani!.. heee heee heee!
Hata hivyo umezungumzia kuwa Nyerere alikuwa mdini wakati waziri mkuu wa kwanza alikuwa muislaam na hakuwa na elimu zaidi ya hekima na busara. Tena basi mimi binafsi namheshimu sana Kawawa kwa sababu ya hizo Busara zake na sio kwa dini yake! Hata kama angekuwa mkristu sidhani kama angekuwa tofauti na Kawawa niliyemjua mimi miaka hiyo. Rais aliyefuatia alikuwa Muislaam na wengine wote waliokuwa ktk nafasi ya juu kuchukua Urais wakati Ule!.. ikiwa ni pamoja na Salim A Salim na Kighoma Malima. Na tazama basi baraza lake la mawaziri!.. kulikuwepo na kila rangi acha dini zao kama sio waislaam kuwa wengi zaidi. Usitake turudie mada ambazo tumeisha zizungumzia na hata Picha ya baraza lake la kwanza ilisha tolewa humu JF tukaona mseto ule wa kwanza.

Unajua Nungwi, hii mada imebeba kichwa cha habariu kibaya sana! ni kichwa kinacho dhihirisha Ubaguzi unaposema Mkapa angewafaa sana waislaam kuliko JK!.. Hii ina maana mategemeo yako yalikuwa JK awabebe waislaam zaidi ya wakristu. Kwamba JK alikuwa anatakiwa kutazama dini za wateule ili kuwapa nafasi zaidi waislaam ktk kuweka Uuwiano. sasa nachoshindwa kuelewa ni Uuwiano upi unaohesabika hapa maanake pamoja na kuwa waislaam ni wengi ama sawa na wakristu nadhani mvuvi huvua samaki ampendaye kumla na sio kila samaki ktk bahari kutafuta usawa! Hivi wewe ukiacha kumwoa mke wa kabila lako utaitwa wewe kuwa ni waste!... ama?

Tatizo moja kubwa uloshindwa kulitazama hapa ni kwamba nchi yetu haijengwi kwa sera za kidini na hakuna ujenzi wa maendeleo yetu yanayotazama dini za watu ktk utekelezaji wa baadhi ya taasisi za serikali. Na mimi binafsi sikubali kuwa kuna udhaifu fulani unatokana na imani ya mtu katika kulitumikia taifa ila nimeyaona mengi yakifanywa na waislaam nje ya imani zao za dini. NI mwinyi aliyefungua milango ya uhusiano wetu ya Israel, ni Mwinyi aliyeruhusu kamari nchini, ni chini ya uongozi wa Mwinyi nilipoona makanisa yakijengwa kwa nguvu huko Zanzibar na hata kukaribishwa kwa madhehebu ya Moman hasa kutoka Nigeria ambao nasikia kuna baadhi ya sala zao huzifanya wakiwa Uchi. Ni mwinyi aliyeruhusu hata dhehebu la Ahmadia kuwa na maskani yao Tanzania.

Kwa hiyo ktk demokrasia ya leo Mwinyi anastahili sifa nyingi kwa kuwa rais asiyekuwa na Ubaguzi wa kidini lakini wakati huo huo kuna watu wanamwona kama shetani aliyeuza ustaaarabu wa Mtanzania kwa kikombe cha kahawa! na pengine kumtoa ktk Uislaam kwani yote alofanya ni kufuru. Na mimi binafsi nitasema kwamba mwinyi ndiye rais aliyepoteza culture yetu kwa kutufungia hizi imani mpya ambazo leo hii imekuwa mzigo mkubwa kwetu wazazi. Na sidhani kama ni maendeleo hata kidogo kwa sababu ukitazama nchi hizi za sub sahara ambazo ndio maskini kuliko nchi nyingi za kiafrika tumekwisha poteza kabisa culture zetu kwa kuiga Uzungu, uarabu na Uhindi na hata elimu yetu imekuwa ya kunukuu. Tumebaki watupu bila mwongozo kama vile misahafu imefutika na kubaki karatasi nyeupe!..
Nungwi, Tanzania njaa tu ndio inatusumbua hata kuanza kutazama dini na makabila ya watu ili kuwachulia watu ambao kwa kawaida ni chaguo la uongozi wa CCM. Mimi nadhani kama unayaona makosa ktk chaguzi zote uloweza kuzitaja basi wa kumlaumu ni CCM kwani hao waliochaguliwa ndio viongozi wanao support uongozi na sera za CCM chini ya JK. Ikiwa Bunge letu haliko independent, Majaji na jeshi letu ni taasisi za chama tawala kwa hiyo sidhani kama unategemea teuzi za hawa watu ambao yawezekana ni wachapa kazi lakini sio matunda ya chama. Kumbuka tu Tanzania leo hii imefikia kwamba ukiwa against CCM basi wewe sii raia halali wa Tanzania, umeikataa nchi yako!. Hili ni tamko la viongozi wetu wenyewe!
CCM sio JK bali ni team nzima na kama kweli kuna makosa mengi basi ndugu yangu watupie CCM ambao ni kundi kubwa la mchanganyiko wa waislaam na wakristu!. Na hata siku moja usifikirie kwamba JK ndiye kinara wa CCM, utakuwa umejidanganya kwa sababu CCM ni kubwa kuliko JK na wanaweza mweka chini kwa kasi ya kufumba na kufunbua macho!
Hawa jamaa hawana dini wala kabila bali ni system ambayo mimi na wewe tunaitazama tamthiria hiyo ktk mchezo wa sinema tu!
 
Nungwi
Kuna kitu kingine kwenye sheria lazima Upractice zikae kichwani, ndugu yetu Chande alikwenda Nje ya Nchi, so utakuta ktk kipindi hicho atakuwa amepitwa na mabadiliko ya Sheria kadha wa kadha za Bongo, so alivyo pewa Ujaji wa Mahakama Kuu Mbeya alipewa ili apate nafasi ya kuzipitia na kuzitumia kwa kutoa hukumu, sasa hata tutakapo mpa huo Ujaji Mkuu atakuwa in a better position ya kuwa reference aidha kwa hukumu atakazo kuwa ametoa au hata ktk mazungumzo na wenzake. na hata yeye mwenyewe sio mjinga alivyo kata huo uteuzi un, na kuamua kubaki bongo, tena mbeya, maana wengine wangependa kuwa Dari salamu au Arusha au Mza..
Huyo Assad wa UDSM sio lazima tumpe hapo , tunaweza kumpa U commisssioner TRA, Capital Markets etc , kama sasa hivi ni one of the board member NSSf.So Nungwi vitu vingine tusiharakishe. Ndio Maana hata Kikwete Tulimpa Foreign Affairs for ten years ili apate exposure zaidi na kuondo tamaa ndogo ndogo za masurufu na safari za nje. Atleast alipokuwa Foreign Affairs alikuwa anapata wasaa wa kupanda Tube train, kupita mitaa amayo ukiwa Raisi huwezi kupita.
sasa just imagine angechaguliwa Uraisi wakati ule halafu anataka kuingia Casino au kupanda underground itakuwaje na msafara wa Protocol Officers wake?

Maneno mazima na yamekwenda shule,Lakini tuliambiwa kuwa TRA ni mali ya maeneo ya wachagga na DR.ASSAD ni mtu wa Tanga.
 
Mkandara.

AHMADIYYA wako Tanzania kabla ya miaka ya 80s. Msikiti wao uko opposite na Stendi ya mabasi ya zamani ya mikoani-Iringa na Mbeya Mnazi Mmoja. msikiti ule umejengwa wakati wa Mwinyi?

Uingereza ni nchi ya Kikristu lakini bado imetoa fursa ya kuona haki inatendeka kwa dini zingine bila ubaguzi.cheki hapa.
http://www.cre.gov.uk/legal/rights_religion.html au Religion Dicrimination Act 2003.

United Kingdom polisi wanaruhusiwa kuvaa hijab vipi sheria ya hijab ikiletwa Tanzania moto utakuwaje?
 
Kichuguu.

Bob Makani unasema hakupewa kwa vile hakuwa na digrii ya uchumi. mbona Mtei alipewa akiwa na Literature? wakati Makani ana sheria ambayo kidogo inafanana.

Baada ya Nyirabu alikuja Rutihinda kuwa gavana, huyo alikuwa na Political Science na International Relations.

Nadhani Makani hakupewa kwa dini yake lazima tukubali Mwalimu alivyokuwa Mdini.

Swala la Rutihinda na Nyirabu lisingie kulinganisha Bob Makani na Nyirabu. Wewe niambie Nyirabu alikuwa na taaluma ipi; halafu thibitisha kama kweli Bob Makani aliachwa kwa sababu alikuwa Mwislamu; una hakika kuwa Bob Makani ni mwislamu? mimi sijui dini yake.

Back 2 Warioba kuwa alikuwa na Qualification ndio akapewa uwaziri mkuu,na Jaji Chande ana Qualification zaidi ya Warioba au Augustino Ramadhani.sasa unataka tuamini kuwa Qualification ni kigezo, wakati jana ulisema kuwa SENIORITY ndio kigezo. mkuu sikuelewi kabisa!Chande ana exposure kubwa sana ambayo hana Warioba wala Jaji mkuu mpya.
Utahitaji kufanya kazi ya ziada kunielewa kama unasoma ukiwa na majibu tayari kichwani mwako.

(1) Waryoba alipanda pole pole kuanzia ngazi za chini za unasheria baada ya kutoka chuoni; alifikia kuwa mwanasheria mkuu baada ya miaka kumi tangu aanze kufanya kazi za uanasheria na kuhitimu masters in international law.

(2) Nyerere hakumfanya Waryoba kuwa waziri mkuu, aliteuliwa na Mwinyi.

(3)Sijasema kuwa jaji Chande hana uzoefu; hata hivyo, uzoefu wake katika judiciary system yetu ni mdogo kulinganisha na wa Jaji Ramadhani. Unataka uamabiwe vipi ndipo uelewe tofauti. Kufanya kazi kama mchunguzi wa migogoro mbalimbali kwa kwenye umaoja wa mataifa ndizo qualification kubwa kuliko kufanya kazi kama jaji wa mahakama ya rufaa kwa miaka 18?

(4) Sijui ulingansihaji wa Jaji Chande na Jaji Waryoba wewe umeutoa wapi. Au ndiyo nijue kuwa hii ndiyo tabia ya Nungwi ya kuzungumza lolote limjialo kichwani. Hata hivyo hujui kuwa Waryoba pia ni jaji wa umoja wa mataifa kwenye maswala ya bahari na pia ameshaondongoza tume za commonewalth?
Nakurudisha UDSM nyumbani kwako. wakati anatafutwa Dean wa Faculty ya Commerce and Management- Assad Mussa akamshinda vibaya Chijoriga kwa qualification na Seniority, akapita kwenye interviews zote. lilipofika File kwa Luhanga-VC wenu akampa bibi Chijoriga kwa madai ya Gender. hili limelieleza sana kwenye Mada ya Mzumbe VS UDSM nenda kwenye elimu utaona.

U-TURN ya Luhanga kuwa ni Gender imetoka wapi? mtu akija na Qualfication kama Chande unasema unataka Seniority. ikija Seniority kama DR.Assad unasema GENDER ISSUE and Globalization.

Wewe Nungwi kweli kweli, na umeanza sasa; is this crap really relevant here?

Warioba alipewa uwaziri mkuu kwa upendeleo kigezo cha elimu hakihusu kwa cheo cha uwaziri mkuu. ndio maana unaona Sumaye alipewa madaraka hayo huku akiwa hana elimu. baada ya kumaliza Uwaziri mkuu ndio amekwenda kusomea Management skills, wakati alitakiwa awe na Knowledge hiyo kabla ili apply kwenye uwaziri mkuu wake.

Hujui kuwa mtu aliyempa uwaziri mkuu Waryoba alikuwa Mwinyi. Kipindi hicho kulikuwa hakuna mgombea mwenza kwa hiyo Rais ndiye alikuwa akiteua makamu wa rais na waziri mkuu ampendaye, na kwa vile mwinyi alikuwa katokea Zanzibar, ilikuwa lazima waziri mkuu atoke bara kulingana na katiba ya wakati, ndiyo maana Salim aliyekuwa waziri mkuu wa Nyerere akafanywa naibu waziri mkuu. Mwinyi alikuwa na candidate wa kutosha kwa mfano akina Msuya, lakini yeye akamchagua Waryoba.

Na kwa taarifa yenu Course work na Dissertation amefanyiwa na vijana wa kikenya.
Wewe Nungwi kweli kweli; Kwa vile Mzumbe kila mtu anaweza kupata Ph.D kwa wiki moja mnachukulia kuwa kila chuo kinafanya hivyo; yaani watu wengine wasifanye kazi zao wakalie kufanya coursework na dissertation ya mtu mwingine. Hizi siyo dissertation za Mzumbe kuwa utaiandika siku mbili tu, ni kazi inayoweza kufanyika kuanzia miezi minne na kuendelea kulingana na digrii yenyewe. Je wasamalia wema hao wa kikenya walikwenda kumfanyia defense pia?

Nawaomba WaTanzania tusibaguane wote wapewe vyeo. kama balance ya Muungano inatazamwa why not ya Dini?

Hii ni sawa kabisa, ndilo jambo tunalozungumzia kuwa tusichochee tofauti zetu zinazoweza kutusambaratisha. Balance ya muungano ni jambo ambalo linaweza kufanyika lakini dini ni choice ya mtu, anaweza kuibadili wakati wowote akipenda. Ukiendekeza dini katika utoaji wa vyeo, kuna watu watakuwa wanabadili dini zao kila leo kuelekea kwenye dini zenye mgao wa vyeo katika wakati huo.
 
Mtalii,
Kwanza nakuomba usome vizuri maelezo yangu na kutafakari nini hasa lengo la maandishi yangu!
1. Ahmadia wapo miaka mingi na hata hao wenye dini za ajabu lakini hawakuweza huru kutoa mahubiri yao kama hivi leo. Hata usenge ulikuwepo, kamari zilikuwepo na hata baadhi ya miradi nchini iliyosimamiwa na Wayahudi.

Nitaongezea kusema kwamba pamoja na kwamba Tanzania ilikuwa nchi ya Kijamaa lakini walikuwepo wenye biashara binafsi waliokuwa wakisafirisha mali zao nje, kulikuwepo na shule za private, maduka ya private, kampuni private na kadhalika lakini tunasema alofungua milango ni Mwinyi!...

2. Nimesema kwa sura mbili na wewe unaweza kuchukua yoyote ile kwa mtazamo wako lakini haiwezi kupotosha ukweli zaidi ya kuwa for ama against!.. Na huo mfano wa Uingereza ndio hasa tofauti kubwa kati yao na sisi. Wao wanaelewa kwamba dini sio kigezo cha Uongozi na wala dini sio culture inayoweza kutafsiri utendaji kazi wa mtu serikalini. Pamoja na yote hayo sheria zao bado zimesimamia kulinda maslahi na culture zao kiasi kwamba wewe mgeni ndiye unayetakiwa kufuata masiha yao na sio mwenyeji kuiga maisha ya mgeni.
Hii ni tofauti kubwa sana kati yetu na wao, Hata siku moja hutamwambia Muingereza kuanzisha lugha ya Kifaransa kuwa sheria pamoja na kwamba zipo shule za Kifaransa Uingereza.
Sijui nisema nini zaidi upate kunielewa lakini nachojaribu kusema hapa ni kwamba mambo mengi machafu hutokana na uzembe wa kiongozi ktk kulinda maslahi na tamaduni za nchi husika. Mwinyi alikuwa kipofu ktk hayo kama alivyokuwa Mkapa kipofu wakati wa Majambazi!..hii haina maana wakati wa Mwinyi hapakuwepo na majambazi!
 
Mkandara umeingia CHADEMA juzi tu tayari ushakua mhafidhina kiasi hiki?

Tanzanianjema
 
Mkuu Kichuguu.
Vipi kuhusu APIYO ambaye alikuwa katibu mkuu ofisi ya Rais kipindi cha Mwalimu Nyerere nasikia nae ni ndugu yake Mwalimu. vipi kuna ukweli?
 
Hapa shughuli ipo,acheni wananchi watafakari na ndio maana ya JF.

Tutangulize ukweli halisi ktk tafakuri zetu,kwa upande wangu always nasikia mchawi mpe mwanao akulelee;Mkapa alipewa akalea na sasa zamu ya JK analea la muhimu ni kila binadamu kumtendea haki mwenziwe,biliv or not-siyo wote tutateuliwa na Rais ktk nafasi hizo 60 au 120 maana tuko milioni 40.

Kufanya kazi kwa muda mrefu na mafanikio kunakupatia uhitimu wa kitaaluma ktk kazi hiyo,angalia wenzetu hutoa viwango vya admission ktk kozi mbalimbali na moja ya sifa ni kufanya kazi ktk kipindi kisichopungua muda fulani lakini si hivyo tu wanathubutu kukupatia wasifu wa kitaaluma pasipo kuingia class kwa sababu tu umefanya vizuri ktk eneo lako kama ambavyo angetakiwa kufanya msomi wa level fulani.
Tido yuko juu,sisi tunafahamu hilo na ameweza kujipambanua mwenyewe ktk safari yake ya uana habari kuliko walivyo wanahabari wetu wengi wakongwe wanaotaka waheshimiwe na kuteuliwa eti kwa sababu walimsaidia JK kuupata urais,jamani yule jamaa kama angeliuokosa huo urais bado angeliendelea kuishi tu,nyie mmeng'ang'ania kumuandikia rais risala tele na kumfunda,kila kukicha mwenzio aliyekuachia ni mla rushwa,kafanya biashara,miaka kumi yake ni uchafu mara na wewe unaonaje? Hivi ndivyo kweli dunia ya habari inavyotutaka kutufundisha wana jamii,tutambue dunia na wakubwa wa duniani wanamtambua Tido kuwa ni miongoni mwa watanzania bora kabisa.
 
Shule na level ya Sumaye vilitosha kuvivaa viatu vya Dkt wa heshima . Cleopa David Msuya,pengine Nungwi unaichambuaje elimu ya juu ?? Sidhani kama unamtendea haki msomi yeyote dunia kwa imani eti kila unachohitimu ni uwezo wako binafsi.

More than 11 years since frederick Tluway Sumaye alipoifanyia kitu njema Halmashauri ya jiji pekee zama hizo,nipe utafiti wa kisomi wenye milinganyo chanya ukisaidiwa na uwepo wa wasomi ambao ni zaidi ya Diploma ya Sumaye a.k.a.John Major(wakubwa wanamkumbuka sasa)Nisaidie hilo kitafiti
 
seniority kwenye ngazi ya judiciary ni jambo la muhimu sana...pale referal court the most senior supreme judges ambao wangekuwa eligble kuwa cj ni big.gen [retired] augustino ramandani,judge mrosso,judge lubuva,judge eusebio munuo na jaji kiongozi manento...majaji wa rufaa na mahakama kuu wamepangwa kwa namba kutokana na seniority[mfano ramandani alikuwa akijulikana kama JR 1..namba mbili baada ya JM....na kuendelea.hadu JR 11..namba zao hupanda kadiri wanavyositaafu au vinginevyo...kwa kuzingatia seniority protocal ya kujoin supreme court au high court..
kule kwenye bench la mahakama kuu kuna dadi J 50...sasa nimeangalia cv ya judge othman inalipa...huyu jaji mkuu bada ya kama miaka minne atakuwa amefikia retirement at any cost kwani hadi sasa amebakisha miaka miwili ya kustaafu kwa lazima na yupo eligible kwa extention ya two years contract..sasa kama muungwana akitaka kumpa othman ujaji mkuu ..itabidi ampe ujaji kiongozi ndani ya hii miaka miwili[since any judge kwenye bench anaweza kuchaguliwa kuwa jaji kiongozi na jaji mkuu]...then ampe ujaji wa supreme [since jaji mkuu anaweza kutoka kwenye bench la supreme au jaji kiongozi....so kwa kuwa bado ni kujana he is still a material and let us give him minimum of another five years ..if we want to think of him as CHIEF JUSTICE..although hata kuwa jaji peke yake ni heshima kubwa sana.
HATA jeshini mkuu wa majeshi lazima achaguliwe kutoka kwenye rank ya brig general kuendelea although mara nyingi au zote hutoka kati ya kundi la ma MAJ GENERALS...hii ni kwa sababu nchi hii ina system nzuri na ina amani so ni vigumu rais kukosa imani na senior officers ambao wako eligble kwa uteuzi akakosa hata mmoja wa kumwamini hadi aanze kutafuta makanali wakuwapandisha kuwarusha ngazi nne kama wanavyoweza kufanya marais wa nchi zisizokuwa stable..
upande wa polisi naona mara nyingi makamishana wa makao makuu wamerukwa sana kwenye uteuzi..mara zote maris wame prefer ma RPC...KUANZIA mzee mwinyi alimrusha ngazi HAROUN MAHUNDI kutoka RPC ARUSHA hadi IGP..Akafuatia mzee mkapa akamrusha OMAR MAHITA kutoka RPC arusha hadi IGP....NA KUWAACHA makamishna wa makao makuu wanashangaa..MUUNGWANA kamrusha SAID MWEMA ambaye alikuwa RPC mbeya [then seconded to interpal ] kuwa IGP na kusababisha kizaazaa kwa kuingia na makamishana wapya kabisa even tibaigana was not commissioner before...

seniority...

..mzee wa data!

..umesoma alichokisema jaji mkuu aliyepita,kwenye majira ya leo!
 
Mzee Kifimbo,
Timothy Apiyo ni MJALUO. Huyo ni jamii moja na Prof.Sarungi na Mabere Marando.

DAR-SI-LAMU,kichuguu,nungwi,
CJ Mstaafu kaeleza kwamba CJ wa India hachaguliwi na Raisi. Wanachofuata wao ni seniority. CJ aki-retire nafasi yake inajazwa na aliyekuwa namba 2.

Mimi nadhani kwa uteuzi huu JK amekuwa muungwana kwa kumteua Jaji aliyetumikia kwa muda mrefu pale Mahakama ya Rufaa.

Hata CJ Samatta naye alikuwa na exposure ya Kimataifa baada ya kufanya kazi ktk Mahakama ya Zimbabwe. Aliporudi Tanzania nadhani alikuwa posted Mahakama Kuu Dodoma. Baada ya hapo akawa Jaji Kiongozi, then akawa-promoted kuwa Chief Justice.

Jaji Othman Chande amekaa nje ya nchi muda mrefu sana. Zaidi hajawahi kuwa Jaji ktk Mahakama zetu. Kutegemea kwamba angeteuliwa kuwa Jaji Mkuu wa Mahakama ya Rufaa ni sawa na kuota ndoto. Hata kama JK angekuwa anataka kusaidia Waislamu sidhani kama angeweza kufanya kitu out of the ordinary kama hicho.
 
Mtalii,
Kwanza nakuomba usome vizuri maelezo yangu na kutafakari nini hasa lengo la maandishi yangu!
1. Ahmadia wapo miaka mingi na hata hao wenye dini za ajabu lakini hawakuweza huru kutoa mahubiri yao kama hivi leo. Hata usenge ulikuwepo, kamari zilikuwepo na hata baadhi ya miradi nchini iliyosimamiwa na Wayahudi.

Nitaongezea kusema kwamba pamoja na kwamba Tanzania ilikuwa nchi ya Kijamaa lakini walikuwepo wenye biashara binafsi waliokuwa wakisafirisha mali zao nje, kulikuwepo na shule za private, maduka ya private, kampuni private na kadhalika lakini tunasema alofungua milango ni Mwinyi!...

2. Nimesema kwa sura mbili na wewe unaweza kuchukua yoyote ile kwa mtazamo wako lakini haiwezi kupotosha ukweli zaidi ya kuwa for ama against!.. Na huo mfano wa Uingereza ndio hasa tofauti kubwa kati yao na sisi. Wao wanaelewa kwamba dini sio kigezo cha Uongozi na wala dini sio culture inayoweza kutafsiri utendaji kazi wa mtu serikalini. Pamoja na yote hayo sheria zao bado zimesimamia kulinda maslahi na culture zao kiasi kwamba wewe mgeni ndiye unayetakiwa kufuata masiha yao na sio mwenyeji kuiga maisha ya mgeni.
Hii ni tofauti kubwa sana kati yetu na wao, Hata siku moja hutamwambia Muingereza kuanzisha lugha ya Kifaransa kuwa sheria pamoja na kwamba zipo shule za Kifaransa Uingereza.
Sijui nisema nini zaidi upate kunielewa lakini nachojaribu kusema hapa ni kwamba mambo mengi machafu hutokana na uzembe wa kiongozi ktk kulinda maslahi na tamaduni za nchi husika. Mwinyi alikuwa kipofu ktk hayo kama alivyokuwa Mkapa kipofu wakati wa Majambazi!..hii haina maana wakati wa Mwinyi hapakuwepo na majambazi!

Tatizo tu ni kwamba, kuna aina za watu ambao hata ueleze vipi, hawataki kutoa nafasi ya kutafakari yanayosemwa na upande wa pili. Aina ya watu wenye misimamo isiyoruhusu kupima hoja mbadala.
 
Huu ushbiki wa dini watu wanauchukulia too personal hivyo hamtapata conclusive disscussion. Naona kuna watu wametumwa humu kuja kupima maji na kupeleka data kwa wakubwa. Goodluck guys!!!
 
Jaji Othman Chande amekaa nje ya nchi muda mrefu sana. Zaidi hajawahi kuwa Jaji ktk Mahakama zetu. Kutegemea kwamba angeteuliwa kuwa Jaji Mkuu wa Mahakama ya Rufaa ni sawa na kuota ndoto. Hata kama JK angekuwa anataka kusaidia Waislamu sidhani kama angeweza kufanya kitu out of the ordinary kama hicho.

..hata miye si-support haya mambo ya kusukumana[read push]hata kama mtu hana credits hizo.

..jambo hili ni hatari kama ilivyo cancer,itakula taratibu ukijashtuka,mguu wa kukata!

..nadhani ni bora kufahamu kuna mapungufu sehemu na kuyashughulikia kihaki na kwa kufuata taratibu na si upendeleo usio busara!

..ukweli ni kwamba hamna siku kuna kundi litaridhika kwamba limepata fair share. halafu haya malalamiko yanaanza kuwa unhealth sasa,yanazaa magonjwa ya kudai hata kisicho haki!

..nadhani kama jamii,waislam wanahitajika kusomesha watoto na kuhakikisha wanaendelea na masomo na kuwa na profession zao. wahitajika kujiendeleza kimaslahi na kushirikiana na jamii nyingine kwa karibu zaidi ili wanufaike nazo!.
ulalamishi hautasaidia,kwani nafasi katika serikali zinaweza kutolewa sana,tena sana na hata zaidi ya wengine. lakini je hii itasaidia jamii ya kiislam kujikomboa katika kuona kuwa inaonewa?je itabidi tu-nationalize mali za watu ili tuipe?kwa sababu hitaji moja huzaa jingine!

..hii wakati mwingine inanikumbusha matatizo ya waafrika na shutuma kwa wazungu. lakini,ni waafrika haohao wanaorudisha maendeleo yao nyuma,tena wakati mwingi kwa kushirikiana na wazungu na kwa faida ya wazungu!

..ukombozi wa fikra na ilimu dunia ni kitu muhimu sana katika maisha ya bin-adam.

asalaam aleykhum.
 
Kuna sensa au utafiti upi unaoonyesha idadi ya Watanzania kwa dini zao?

Ipo na inasema wazi kuwa waislamu wamewazidi wakristo kwa asilimia chache. Hata wakuu wa nchi wanakubali hilo lakini sio katika open platforms. Hii ni kwa kuwa wanahitaji kupunguza makali ya kina Ponda na wengine na hata CUF ambayo wanaona kuwa ina strong base katika suala hili.

Suala la Mkapa angeweza kufanya vizuri katika mgao wa madaraka linaweza kuwa kweli kwa kutumia logic kwamba kwake yeye usingekuwa upendeleo bali ni boldness lakini hata hivyo haikuwa rahisi kwake maana wakti tuna kina Sheikh Ponda vilevile tuna kina Mtikila na Pengo kama tulivyo na kina Kilaini na Gorogosi kwa upande mwengine.

hata hivyo muhimu ni capacity building kama vile kuziwezesha shule za waislam haswa zile za bakwata kutoa elimu bora zaidi ya bora elimu. approach nilishapendekeza hapo mwanzoni mwa hoja hii ingawa inaelekea wana jambo si wapenzi wa advise kama zangu. Changamoto ni kwa wale waliopenya ngome kubadili mentality ya baadhi ya watu wanaosumbuliwa na fikira mgando kuwa waislamu aka waswahili hawawezi kuongoza majukumu "nyeti".

Tanzanianjema
 
Mkuu Kichuguu.
Vipi kuhusu APIYO ambaye alikuwa katibu mkuu ofisi ya Rais kipindi cha Mwalimu Nyerere nasikia nae ni ndugu yake Mwalimu. vipi kuna ukweli?

Kifimbo Cheza,

Hapana, ukweli ni kuwa Opiyo alikuwa swahiba na msiri mkubwa sana wa Nyerere; ndiye aliyesuka ile security system ya nyerere. Hata hivyo hawana undugu wowote. Opiyo ni Mjaluo wa Utegi Tarime, wakati Nyerere alikuwa mzanaki wa Butiama Musoma.
 
Status
Not open for further replies.
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom