Mkandarasi aliyepewa kumalizia kuweka lami eneo korofi baada ya kuvuka daraja la Kigamboni (Mnadani) amegeuka kero kubwa Sana kutokana na staili yake ya ujenzi usiozingatia kanuni za ujenzi!
Tanroad/Tarura/RTO/DTO Mambo Kama haya mwisho wa siku ndiyo huchangia wananchi Kushambulia wajenga barabara!
- Kanuni za ujenzi zinamtaka Mkandarasi kutumia Alama na michoro (posters) kutoa maelekezo kwa watumia barabara LAKINI HUYU hazingatii Hilo
- Kanuni za ujenzi zinamtaka Mkandarasi kuandaa njia mbadala (njia mchepuko) kabla ya kufunga barabara, Huyu Mkandarasi hazingatii hili Wakati wowote anafunga barabara pasipo kuandaa/ kutoa maelekezo ya njia nyingine mbadala (mchepuko) kwa watumiaji wa barabara!
- Mkandarasi anatumia Vifusi na mawe kufunga barabara pasipo kuweka (Reflection sign ) kwa watembea usiku.
- Mkandarasi Huyu pamoja na kutambua kwamba eneo like Ni (busy area) lakini hafanyi kazi weekend wala USIKU zaidi ya kufunga njia na kuondoka Jambo linalosababisha kero kwa watumiaji wengine wa barabara.
Tanroad/Tarura/RTO/DTO Mambo Kama haya mwisho wa siku ndiyo huchangia wananchi Kushambulia wajenga barabara!