Mkakati: Lowassa kuhamia UKAWA

Kama UKAWA lengo lao kuu ni kushinda uRais tu (kiasi cha hata kumtumia mtu kama Lowasa), basi HAWATUFAI! Nchi inahitaji marekebisho makubwa sana kisiasa. Watu kama Lowasa (na wenzake huko CCM) wanawakilisha uozo unaolitesa taifa letu leo hii.
 
Shida ni kuwa Lowassa ni mwizi

Nao wezi wanatofautiana sifa. Kuna wezi wanaiba faida yote na rasilimali. Wapo wanaoiba kidogo toka faida iliyopatikana na kukubakizia sehemu kubwa pamoja na rasili mali yako . Hili kundi ndipo unapoweza kumweka Lowasa. Kundi baya kabisa ni la wezi wa hela akaunti ya escrow wale hawakubakiza hata senti kwenye ile akaunti. Kama wote mjuavyo ccm hayupo alie msafi hata yule ambae hajawahi kuwa kiongozi ilimradi ni mwanachama wa chama hicho ila wanaachana tu kwa makundi niliyoyaeleza hapo juu. Ni wazi Edo ana nguvu kubwa sana kwenye chama hicho kuliko yeyote yule. Kusema kweli kwa sasa ndio mtaji wa ccm wakienda nje ya huyo mhesabuni Wilbrod Slaa mshindi. Kwangu kama unaniingizia faida kubwa na kuiba kidogo bado ni wa maana kwangu kuliko anaefanyia hasara hadi mtaji kuteketea au anaeiba faida na mtaji. La kulielewa nyie wote ni kuwa iwe iwavyo Lowassa hawezi kujiunga upinzani.Ila nec ya ccm isipompitisha madhara yake kwa chama ni makubwa mno kwa ushawishi alio nao huyu nguli mvuto na kukubalika kwake. Eleweni hata vyama vya upinzani vinamkubali huyu bwana ingawa hawawezi kukiri hivyo.
 
Kwa7bu hzo bora CCM ife kuliko kumweka huyu mtumwa wawahindi. Inaniuma sn kuona watu timamu mnamsafisha mtu alie tuingza kwenye hasara kubwa wakati wapo watu wasio fungamana na makundi jaman huyu mzee hafai
 
huyu ni mpiganaji wa kweli hawezi kamwe kuikimbia ccm , ni mtu amefanya vitu vingi tumeviona hasa alipokua waziri wa arthi na alipokua waziri mkuu , ni mtu ambaye binafsi kama atapitishwa niko tayari kumpigia kampeni kwa nguvu zote. naomba mola ampe afya njema LOWASA ili aweze penya mtihani huu wa kupitishwa na ccm kua mgombea. na sihofii hata kidogo atapenya tu. litapenya tu hili JEMBE.
 
Mtaongea yote lakini atakuwa rais. Mbio mnazokimbia alishasahau kumbe nyie ndio mnaanza kukimbia.. Mmechelewa sana.
 
Joto kuelekea uchaguzi mkuu 2015 linazidi kupanda. Kati ya mtu anayetajwa sana kugombea katika nafasi ya urais ni Edward Lowassa.

Pamoja na tafiti nyingi rasmi na zisizo rasmi kuonesha kuwa EL anaongoza kwa kuaminiwa na kupendwa na watanzania wengi, CCM inaonekana kwa siri na kwa dhahiri kutokumhitaji Lowassa.

Na kwa kuwa Lowassa anataka kuwatumikia watanzania na watanzania wanamhitaji yeye.. Ni ushauri wangu kuwa, kama CCM wakimzingua abadili uelekeo na kuelekea UKAWA ama Chama kingine chochote.

Nina imani EL atashinda 2015 iwe kupitia CCM, ukawa ama Chama kingine chochote.
 
Joto kuelekea uchaguzi mkuu 2015 linazidi kupanda. Kati ya mtu anayetajwa sana kugombea katika nafasi ya urais ni Edward Lowassa.

Pamoja na tafiti nyingi rasmi na zisizo rasmi kuonesha kuwa EL anaongoza kwa kuaminiwa na kupendwa na watanzania wengi, CCM inaonekana kwa siri na kwa dhahiri kutokumhitaji Lowassa.

Na kwa kuwa Lowassa anataka kuwatumikia watanzania na watanzania wanamhitaji yeye.. Ni ushauri wangu kuwa, kama CCM wakimzingua abadili uelekeo na kuelekea UKAWA ama Chama kingine chochote.

Nina imani EL atashinda 2015 iwe kupitia CCM, ukawa ama Chama kingine chochote.

Wakati Yeye Akijipanga Na Critics Wake Nao Wanajipanga ktk Kumwangusha Na Kwa Taarifa Nilizonazo Tena Za Ndani Jikoni Ni Kwamba Piga ua Rais Ajaye Wa Tanzania Ni Kati Ya Watu Hawa :

1. Sospeter Muhongo.....15%
2.Stephen Wassira.....20%
3. Jaji Augustino Ramadhani.....5%
4. John Magufuli.........60%

Makamu Wa Rais Iwe Isiwe Amepangwa Kuwa Mzee Samuel Sitta

Waziri Mkuu Ni Kati Ya Hawa Wafuatao:

1. Asha Rose Migiro ( Ila Kama Atagombea Ubunge Na Kushinda )....5%
2. Mark Mwandosya ( Ila Kama Atathibitisha Sumu Ile Imemtoka )....5%
3. Hussein Mwinyi..........70%
4. Harrison Mwakyembe......20%

NB. Endapo Hii Itabadilika Basi Mjue 100% UKAWA Wanashika Hatamu Na Padre Wangu Wilbroad Slaa Kuwa Rais Wangu Mpya.
 
Hhahaha majizi ndio wametawala bongo alafu nashangaa sana kuona watu wanamshobokea mtu alieilaza nchi gizani kwa muda mtefu huku wakipanga mgao wa umeme juu ya meza
 
Ni ukweli usiopingika mtu aliyebakia ndani ya CCM mwenye nguvu kubwa ni Lowassa ni kama ndoto lakini zinaweza kufanikiwa CCM hawawezi kumpitisha Lowassa kugombea urais kupitia CCM kwa sababu wanajua nguvu yake lakini UKAWA wakiunga na Lowassa watafanikiwa kuiondoa madarakani CCM mchana kweupe .UKAWA fanyeni kazi huu ushauri.
 
Nadhani Pia ya kwamba kuna umuhimu wa UKAWA kufanya kile kisichotegemewa. Kwenye Siasa hakunaga Adui na Rafiki wa kudumu. Kinachaangaliwa ni kufikia Malengo ya Kisiasa ambayo moja na kuu na la Mwanzo ni Kushika Dola.

Kuitoa CCM madarakani inahitaji mbinu za Ku-surprise na zisiwe za muda mrefu hii nayo ikiwa mojawapo.

Ili la Kuungana na Lowassa ni moja ya mbinu za Kuwatoa CCM madarakani na tena mkakati ufanyike kwenye dakika za mwisho-mwisho ili kuwapoteza Maboya.

Yawezekana utabiri wa Mwl Nyerere ndio unaweza kutimia kwa UKAWA kuungana na Lowassa, alisema upinzani wa kweli utatoka ndani ya CCM, na Lowassa ndio jibu la utabiri ule wa baba wa Taifa.

Ili Kushika Dola ni vema ubinafsi wa Kivyama ukawekwa pembeni kama UKAWA walivyoonyesha, Sasa basi kilichobaki ni Kusubiria kama CCM hawatamteau Lowassa, basi Lulu hii ikaribishwe UKAWA ili kufikia Malengo ya Kushika Dola. Tumeyaona Kenya kati ya Mweshimiwa Uhuru Kenyatta na Willium Rutto.

Watanzania wa leo walio wengi Wanatamani kuiona CCM ikiwa Chama cha Upinzani hapo October' 2015, maana walivyopigika na maisha hakuna hata mfano.
 
Back
Top Bottom