mjane hana haki ya kupendwa tena?

Unajua Dark City, mwanamume umri ukienda anaweza bado kuoa binti ambaye anamzidi 20yrs, lkn mwanamke akiwa hata na mwanaume wanayepishana 7 yrs (she has to be rich ili kumpata huyo kaka), jamii inamuangalia kwa macho mawili. Na mbaya zaidi wazee wenzake (wanaume) go for younger girls hivyo huishia au kuokoka (kumpenda Yesu) au kuiba waume za watu au kutafuta viserengeti boys!

Mimi nafikiri jamii iwaruhusu wabibi nao wamiliki viSBs na ukizingatia vijana wa sasa hivi wanapenda mteremko, au unaonaje Babu DC?

Aaaha Kaunga umenikumbusha wabibi wa ulaya wanavyomiliki viSBs vya kiafrica huku ughaibuni
 
Unajua Dark City, mwanamume umri ukienda anaweza bado kuoa binti ambaye anamzidi 20yrs, lkn mwanamke akiwa hata na mwanaume wanayepishana 7 yrs (she has to be rich ili kumpata huyo kaka), jamii inamuangalia kwa macho mawili. Na mbaya zaidi wazee wenzake (wanaume) go for younger girls hivyo huishia au kuokoka (kumpenda Yesu) au kuiba waume za watu au kutafuta viserengeti boys!

Mimi nafikiri jamii iwaruhusu wabibi nao wamiliki viSBs na ukizingatia vijana wa sasa hivi wanapenda mteremko, au unaonaje Babu DC?

Ndugu yangu Kaunga,

Nimesema toka mwanzo kwamba haya mambo yanatawaliwa na forces za kisayansi (biological) na kijamii (socialogical) na bahati mbaya sana, hizi forces zimemkalia vibaya mwanamke!!

Binafsi napinga sana tabia ya vijana wadogo wa kiume kutembea na dada au mama zao....inakera sana na haivutii hata kidogo....!!

May be ni mimi tu..ila naamini wapo watu wengi ambao wasingependa watoto wao wa kiume kutembea na wanawake waliowazidi umri......

Hili nimeliongelea sana huko nyuma, na siyo kwa sababu ya kuwanyanyapaa dada na mama zangu ila kwa sababu nilizozitaja hapo juu ambazo mie binafsi naziamini sana!!

Kuna makabila kama majirani zangu Wahaya,...kijana mdogo kutembea na mwanamke anayemzidi umri inachukuliwa kama laana!!

Babu DC!!
 
Last edited by a moderator:
Aaaha Kaunga umenikumbusha wabibi wa ulaya wanavyomiliki viSBs vya kiafrica huku ughaibuni


Hayo unayoyaona yanatokana na njaa tu...binadamu mwenye njaa anapoteza hadhi ya utashi na huwezi kumweka kwenye kundi la watu wenye staha...anaweza kufanya jambo lolote la ajabu hata kama yeye mwenyewe anajua ni baya na halipendi kabisa...

Ego ya mwanamume siku zote inamtaka awe juu ya mke wake kwa karibia kila kitu....hata pale ambapo dume linakubali kubebwa, siyo kwamba kapenda bali kuna nguvu ya kimaumbile inamlazimisha kufanya hivyo!!



Babu DC!!
 
afadhali umeliona hilo,kufiwa siyo mwisho wa maisha jaman kwa yule anayebaki wapeni moyo wa upendo waweze kusonga mbele.
 
Jamii ndiyo hiyo ambayo ina wanawake na wanaume, kama hili lipo sijui linasababishwa na nini. Kuhusu muda unaofaa kwa mwanamke aliyefiwa na mumewe kuingia tena kwenye mahusiano, hakuna muda muafaka inatofautiana kati mtu na mtu. Mwingine anaweza kujiona tayari kuanza mahusiano mapya ya kimapenzi baada ya miezi sita na mwingine hata baada ya mwaka akajiona hayuko tayari pia inategemea mapenzi yaliyokuwepo kati ya mfiwa na marehemu mumewe.

Hi to all, napenda kuchukua nafasi hii kwenu kuomba ushauri juu ya sula la wanawake pindi wanapo ondokewe na waume zao mbona jamii inaangalia kwa mtazamo tofauti sana, tofauti na wanaume wanapofiwa na wake zao? Pili ni muda gani unafaa kwa mwanamke aliyefiwa na mume kuweza kuingia tena kwenye mahusiano na mwanaume mwingine?
 
Haki anayo ila na umri unamata,pata picha binti wa miaka 25 anafiwa na mumewe, ataweza kubak mseja kwel?kwanza itakuwa makosa kumwita mjane maisha lazima yaendelee bana
 
Malizia basi Kaunga...

Na huyo watakayependana asiwe kijana mdogo (single) au mume wa mtu....!!!

Babu DC!!

We Babu,
Kwani ujane una umri maalum? Mjane anaweza kuwa 18 yrs and above. Siku hizi bodaboda zinaondoa vijana wengi sana ambao wengi ni below 28 na unakuta wengine wameoa. Sasa hao wake za ambao nao ni 20s to 30s waolewe na wazee kisa ni wajane?

 
idimi umesema ukweli maana mimi nimefiwa na nina miaka 30 kwahiyo ni lazima nipendwe na wa miaka mingapi?watu waache mitazamo hasi juu ya wajane,sk hizi kila anayefiwa basi ameachwa na ukimwi jamani tubadili mitazamo.
 
Back
Top Bottom