Mjadala kuhusu Babu wa Loliondo na dawa yake.

Tunashuhudia mabadiliko ya gafla ya MJK kama mtu alieamka usingizini, akianza kurudia ile hali yake ya mwanzo alipoingia madarakani, mwenye nguvu, hoja nzito nzito na kauli zenye matumaini kama kiongozi, mwenye maono na hata kutoa amri tunazozitarajia kwa kiongozi na kuanza hata kujichanganya kwenye sekta nyeti na kuapear kwenye luninga akiwa na mambo mazito tu na mwenye kujiamini. Je Mheshimiwa huyu ambae tayari watu walikuwa wameanza kukata tamaa ndo kazinduka baada ya dozi ya kikombe cha babu? Ni vigumu kuamini ninayoona yuanatokea kaanza gafla kwa spidi ya ajabu... inanishawishi kuwaza kuwa kuna jambo la kiafya ya kipsycholojia, kimwili au hata kiroho iliyokuwa inamsumbua na yawezekana amepata matibabu muafaka. Mimi kama kada wa chama chake wa muda mrefu, huyu ndie mtu niliyuekuwa na mjua hapo mwanzo na kubadilika kwake kipindi hiki kilichopita kilinitia mashaka maana waliokuwa chini yake walianza kufanya mautumbo na hakuna aliyekuwa anawaambia kitu, na kushindwa kupata jibu chama hiki kinaelekea wapi... ingawa tunahitaji muda kujua kwa uhakika chama hiki kilichopoteza umaarufu kwa kiasi kikubwa kina mkakati gani kurudisha imani hasa kwa wasomi na watu waishio mijini....

Mfano ngalia: HabariLeo | Wanafunzi wanaofeli wamkera Kikwete

na Home?

pia Rais Kikwete Atembelea Mamlaka Zilizochini ya Wizara ya Fedha

Nasubiri kwa hamu nione kama hotuba yake ya mwisho wa mwezi itafananaje kama kuna improvements zozote hasa kama itaweza kuwa na solid directives za maana na positions za serikali kwenye maswala nyeti badala ya bables
 
kikombe cha babu na utendaji kz wa jkkuna mahucano gan? alwayz jk huwa anaongea bila kutake measure wala kutolea ufmbuz je alipokerwa na matokeo kaamua nini
 
Mie nashangaa kidogo nnaposikia wapo wenye dhambi, mimi nasikia kuwa Yesu alishabeba dhambi zote kwa ajili yetu, sasa vipi tena wawepo wenye dhambi?
 
Mie nashangaa kidogo nnaposikia wapo wenye dhambi, mimi nasikia kuwa Yesu alishabeba dhambi zote kwa ajili yetu, sasa vipi tena wawepo wenye dhambi?
Upeo finyu wa kufikiri ukijumlisha na malaana machache toka mababu na wazazi ndio tunatoa pumba kama hizi
 
Unaweza kuwa sawa!

Lakini tazama kwa mtizamo huu!!

Maana halisi ya tiba mbadala ... Ni kutibu UTU wa MTU kwanza then ndio Magonjwa yake.

Ina maana gani?

Dawa zisibebeshwe mizigo isiyo yake!!..

Ni wendawazimu kuuchezea utu wako na watu wengine alafu upate magonjwa alafu ukatafute dawa ya kuyatibu.

Utu wetu tuubebe wenyewe na dawa ziachiwe zibebe kazi ya kutibu magonjwa yetu!!

Lazima kila mgonjwa kutekeleza kila jambo kwa misingi ya utu na maadili yote ya utu ..kabla ya kwenda kunywa dawa yeyote ....Loliondo au hospitalini!

Dhambi sio UTU!!

Sifikiri Rostam na familia yake ..wana UTU au maadili ya Utu yanawatawala..kama ni hivyo ...it sok to what is happening to them..
Lakini bado wana nafasi ...
Wajirudi ...waupende Utu utawale fikra na matendo yao ..then waanze kutumi dawa..
 
Sikumbuki mara ya mwisho alipokerwa na jambo fulani angalau kukerwa na ilikuwa nini.... then ndo hamu yangu kubwa lilipo je ni moto wa makuti au ndo kaanza kuamka Mipango Miji.

Mpangwa, usije ukanletea zile za kusema nabii hakubaliki nyumbani... nimekuchokoza tu...nina hamu ya kuona huyu tulienae anakuwa converted into vissionary abnd action oriented awake leader... maana mwaka unaisha na itapita cost ya kukaa nae wakati tukijua uwezekano wa kumbadili bado unafifia.... kiukweli sio kiushabiki.... basi hata kwa kikombe cha babu awe tu angalau anakerwa... wakati akila ajue kuna aliyelala njaa sio chini ya siku moja... wakati akitembea kwenye gari la kiyoyozi ajue kuna wagonjwa wanafia njiani kwakuwa hawawezi kufika kwenye huduma ... wakati watoto wake na wa wenzake wanakwenda shule nzuri ajue kuna wanaotamani kuwepo hata kwenye zile za chini ya mti licha ya kuwa wapo wengi hawajui kwanini wako pale kama matokeo yalivyuotuonyesha... basi naafikiana nanyi atafanya nini? Kauli zake ndio sera, misimamo yake ndio misimamo ya serikali, maamuzio yake ndio dira na atakachokataza yeye ndio kinga basi vyote hivi vikiwa na nia njema sio kukandamizana... Akerwe na afanye kitu, aidha kupitia kauli zenye vishindo maana hali yetu ni duni sana tunamhitaji atoe kishindo tuanze kusogea... ndo maana nasema natamani anywe kikombe cha babu kama kitamsaidia kiongozi wetu mkuu na kama ndo chenyewe basi tunamtaka alete kishindo cha mabadiliko bila mzaha, muda uliobaki ndio kipimo chake cha heshima au dharau katika kustaafu kwake....
 
sasa kwani kafanya nini!au ni ile reli ya dar-iasaka aliyokua anapigia stori jana?? kwani ndo mara ya kwanza kusikia ahadi kama hizo??
naamini ukada ni kama ulevi.mtu hujiambui.
 
my friend kama topic yako ni kikombe cha babu then let it be...kama ni query as to why the sadden change (albeit in terms of words) of the president JK, then let it be...but I find no correlation between the two at least the way this topic is framed....mmmmhhhh ama kweli great thinkers!!!! in the making or what?
 
Hakuna kitu hapo! Kauli nzito nzito hajaanza leo, cha zaidi ni blah blah tu, inapokuja kwenye utendaji, hakuna kitu. Kutembelea maeneo ni kawaida yake, hamna kitu hapo!
 
Tunashuhudia mabadiliko ya gafla ya MJK kama mtu alieamka usingizini, akianza kurudia ile hali yake ya mwanzo alipoingia madarakani, mwenye nguvu, hoja nzito nzito na kauli zenye matumaini kama kiongozi, mwenye maono na hata kutoa amri tunazozitarajia kwa kiongozi na kuanza hata kujichanganya kwenye sekta nyeti na kuapear kwenye luninga akiwa na mambo mazito tu na mwenye kujiamini. Je Mheshimiwa huyu ambae tayari watu walikuwa wameanza kukata tamaa ndo kazinduka baada ya dozi ya kikombe cha babu? Ni vigumu kuamini ninayoona yuanatokea kaanza gafla kwa spidi ya ajabu... inanishawishi kuwaza kuwa kuna jambo la kiafya ya kipsycholojia, kimwili au hata kiroho iliyokuwa inamsumbua na yawezekana amepata matibabu muafaka. Mimi kama kada wa chama chake wa muda mrefu, huyu ndie mtu niliyuekuwa na mjua hapo mwanzo na kubadilika kwake kipindi hiki kilichopita kilinitia mashaka maana waliokuwa chini yake walianza kufanya mautumbo na hakuna aliyekuwa anawaambia kitu, na kushindwa kupata jibu chama hiki kinaelekea wapi... ingawa tunahitaji muda kujua kwa uhakika chama hiki kilichopoteza umaarufu kwa kiasi kikubwa kina mkakati gani kurudisha imani hasa kwa wasomi na watu waishio mijini....

Mfano ngalia: HabariLeo | Wanafunzi wanaofeli wamkera Kikwete

na Home?

pia Rais Kikwete Atembelea Mamlaka Zilizochini ya Wizara ya Fedha

Nasubiri kwa hamu nione kama hotuba yake ya mwisho wa mwezi itafananaje kama kuna improvements zozote hasa kama itaweza kuwa na solid directives za maana na positions za serikali kwenye maswala nyeti badala ya bables

Kweli naungana na wewe kweli anaonekana ni mtu aliye hamka usingizini kikombe kimemsaidia,lakini ubongo wake bado hapo nilipopigia mstari bado,anazidi kuwa kiongozi wa kulalamika bbadala ya kutupa ufumbuzi na hatua gani anachukua kama kazi haitaenda sawa.

Jk amedhihirisha uwezo wake mdogo wa uongozi kwa kutokuwa mtu wa kutoa ufumbuzi na kuchukua hatua.Hiyo ndiyo sifa kubwa na ya kwanza kwa kiongozi mwadilifu.Amekuwa akijionyesha alivyotegemezi katika maamuzi na ndiyo maana anafanyiwa kazi zake ,wanaotoa maamuzi wanakuwa wengine kabisa.
 
Kundi moja la wabongo waishio nje, hususan Uingereza na Marekani limewasili KIA tayari kabisa kwenda kupata kikombe Loliondo. Duh!
 
tumechoka na hiz habari za babu,kwanza hii thread sio mahali pake huku,pse mod deal na hizi tread za babu
 
Kundi moja la wabongo waishio nje, hususan Uingereza na Marekani limewasili KIA tayari kabisa kwenda kupata kikombe Loliondo. Duh!

mimi kwa babu hunipeleki hata kwa winchi.

manabii walikuwa wanatoka na kuwatangazia watu kila 'walipooteshwa na Mungu'. Rejea Yona 3:1---

huyu babu anasema kaoteshwa, lakini mbona hatukumsikia akitangaza?

kwa mtizamo huo, mimi namchukulia babu kama 'a new sangoma in Tanzania'.
 
Back
Top Bottom