Mjadala: Gharama na njia nafuu za kujenga nyumba ya kuishi Tanzania

Na kwa mtanzania wa kawaida hawezi kununua kiwanja magomeni ajenge, nazungumzia hata huko periphery (ulikokudharau) bado kuna watu wanakatisha tamaa wenzao. Kumiliki nyumba Kivule it's much better than kupanga Kinondoni, kwa mtazamo wangu.

Big up kwa response nzuri. Afterall with all due respect Magomeni sidhani kama ni eneo la kuishi kwa maana halisi ya kuishi, limekaa kibiashara zaidi!
 
Hiyo mpaka hapo 42m
 

Attachments

  • 1419483135132.jpg
    1419483135132.jpg
    109.8 KB · Views: 662
Bado napambana na ndani kiukweli finishing sio mchezo ila kikubwa nikujibana tu watu wasikukatishe tamaa kabisa jambo la msingi mafundi nao upate wazuri na uwe msimamizi mzuri. Yote yanawezekana ndugu zangu
 
mbona unamtisha?

Nashangaa mkuu hawa siwaelewi kbs kwani wanamfanya mtoa mada ni zombi hafahamu anakoenda.

Mfano nimetoka Dar kwa nauli za kuungaunga nikielekea Arusha. Ni makosa kwangu kumshukuru Mungu nikiwa Korogwe wkt sijawahi hata kuwa na nauli nzm ya Dar-Korogwe? Usinitishe kwamba bado Korogwe-Arusha ni mbali kwani hilo nalifahamu kabla sijaanza safari Dar. It's true wapo watakaonza safari baada yangu na kufika kabla yangu hilo halina shida kwangu tumejaliwa tofauti, nitafika pia ila kwa speed ninayoimudu. Wapo wengine pia ambao wana kipato zaidi yangu na wanahitaji kufika Arusha na hawatafika kamwe kwani wanasubiri wawe na nauli nzima ya Dar-Arusha kitu ambacho ni kigumu sana kwa usawa huu.
 
Mwanaume anatakiwa apambane, usitishwe na gharama za ujenzi, ukishindwa bado ulipoishia itakuwa ni mali yako na wala haiozi
 
Pia hapo ulipofikia ni jambo la kushukuru sana wako ambao wanapiga mahesabu wataanzaje ila nawahakikishia sio kazi ngumu kabisa cha muhimu vijana ku punguza starehe. ...! Kila kitu kinawezekana kabisa.
 
Hongera lakini bati umechemka zimeshapitwa na wakati, jeshini kuna connection ya kupata bati za kisasa kwenye duty free shop zao. Halafu usije kufanya kosa lingine ukapiga chupingi hiyo nyumba chupingi imeshapitwa na wakati ukipiga.

Wewe ndo umechemka unaefikili usichokiweza,bati ziko dukani kwa ajili ya nyumba useme zimepitwa na wakati,ni namna tu ya kujifaragua kwa maneno.utaja sema babu yako au baba kapitwa na wakati,nina hasara gani kupiga hizo bati kingali kijana ili nihamie na nianzishe ujenzi mwingine.
 
Jombaaa!!!!!apo hatuangalii thamani ya jengo n umejenga eneo gn!apo tunaangalia ww umeweza kumiliki jengo lako mwenyewe ,hongera
 
Mi nimeweza kwa kujipanga na kipato changu ni kidogo. Vijana tusitishwe na wanaotaja mamilioni ili kujenga nyumba. Hii inakaribia kuisha na sijafikisha hata m 20!

Mkuu hiyo ramani imenivutia kweli nami nataka nianze kuinua pango,sijui unaweza kunisaidia please!!
 
Kafikia hatua nzuri sana kwasababu wengine hapo wanahamia kabisa..
Naamini utakuwa unarekod hesabu zako kama hutojali ukimaliza tupe hesabu kamili mkuu.
Narekodi, na naamini haitafika m35, Maana milango na madirisha almost tayari yapo, mambo mengini ya tiles, gypsum na wiring najua mdogo mdogo yatafanyika tu.
 
Back
Top Bottom