Mjadala: Gharama na njia nafuu za kujenga nyumba ya kuishi Tanzania

Unajua dirisha la aluminium complete haipungui kilo 3 una dilisha i11 mlango mzuri mninga 250000 ceiling gypsum kwa nyumba yako hyo makadilio M 3.5 tiles bado Mabomba mziki wake usikie tu bado shimo la Maji taka bado Fundi hajaimba cement name
Gypsum powder kaka hapo bado sana wiring nilisahau
Nikusahihishe Mlango wa Mninga Dsm ni zaidi ya Laki 5, na mninga ni inferior kwa Mkongo(I work in that sector, dont argue) Mkongo ni bora zaidi ya Mninga. Na tayari ninayo milango yote 10(Didnt buy in Dar).
Hoja yangu ya msingi ni kuwa 'kidogo kidogo with determination inawezekana' tusikatishane tamaa.
 
Na hayo mamilioni wanayotaja wenzio yanajumuisha pia eneo la ujenzi! Ili nyumba iwe n thamani kubwa zaidi inabidi iwe imejengw kwenye eneo ambalo lina thamani pia,maana hata bei ya kiwanja tu ni zaidi ya nusu ya gharama za ujenzi wa nyumba yenyewe,ila kama umejenga dar maeneo kama ya vikawe au mbande sawa,maana kiwanja cha milioni mbili unaweza jenga numba tatu kama hizo,na material nyingine kama mchanga ni bure tu,hivyo wale wanaolalamikia gharama za nyumba(siyo ujenzi tu)waache tu walalamike,Hongeraa sana mkuu kwa hatua hiyo kubwa uliyofikia.
Na kwa mtanzania wa kawaida hawezi kununua kiwanja magomeni ajenge, nazungumzia hata huko periphery (ulikokudharau) bado kuna watu wanakatisha tamaa wenzao. Kumiliki nyumba Kivule it's much better than kupanga Kinondoni, kwa mtazamo wangu.
 
Askari muoga na anayetisha wenzie uwanja wa mapambano hafai na yafaa aondolewe site mara moja..huo ni uoga na kumtisha mwenzio.nani alikwambia ujenzi huwa unaisha siku hyo hyo kwa uwezo wetu wa kibongo??kuna simulizi za kweli ukiambiwa humu na ukishuhudia mijengo ilivyosimama,ukawacheki waliosimamisha na ukaambiwa mipango mikakati yao hutashangaa.ujenzi sio kula bia counter kwa mikwala ukafananisha na ujenzi..nimewasalisha jct 'in good faith'

Yaani umenena vema sana, Hakuna kitu kinakwaza kama tabia ya kumkatisha tamaa mtu, yey amejitahid kafika hapo na anajua hajamaliza, anajua hatua inayofuata nin, kama aliweza kununua kiwanja, akatafuta raman, akaanza kujenga hadi akafika hapo haiwezekan kuwa hajui anamaliziaje, anayo plan yake namna ya kumaliza, watu unakuja na kuanza kumpigia hesabu za kukatisha tamaa si unafiki huo. wew kama unaona gharama kujenga kwa kudunduliza usimkatishe tamaa mwenzio.

Endelea kusubir uokote pochi ya mzungu ndio utajenga, acha wa2 wajidundulize ila mwisho wa siku ataishia kukaa kwenye nyumba yake na kuepuka kero za kupanga
 
Exactly@Preta,hata km ni kibanda kinachoweza kupigwa teke na kuku ila aliyejenga bwana lazima aheshimiwe..binafsi hata ukimiliki range na vogue ila km nyumba huna sijui nakuonaje yani..thumb up mkuu..kikubwa cha kutambua ni kuwa ujenzi si wa siku moja..hata roma ilijengwa kwa miaka 40,mdogo mdogo ila kwa plan na mikakati inawezekana.
Word, mkuu!
 
Nahamasisha vijana wenzangu kumiliki nyumba zetu na tuachane na ujinga wa kushindanishana kununua magari ya kifahari huku tumepanga. Tabia kama hizi zinakuwa za kitoto.
Kijana mzima ambaye life yako unaoshi kwa kutegemea salary eti unanua simu ya milioni!! Na kijana huyo anayenunua hiyo simu hata kiwanja hana. Tubadirikeni vijana wenzangu.

Mzazi hufurahi anaposikia kijana wake sasa ana mji wake anaoumiliki kwa 100% sio kupanga. Kijana unakuta kajaliwa kazi nzuri mshahara mzuri eti yeye akili zake anazielekeza kuwa mtu wa kulewa lewa a.k.a chapombe na malaya.

Tuige mfano wa jamaa huyu.
Ni kweli kaka, ujana huo umepitwa.
 
Nikusahihishe Mlango wa Mninga Dsm ni zaidi ya Laki 5, na mninga ni inferior kwa Mkongo(I work in that sector, dont argue) Mkongo ni bora zaidi ya Mninga. Na tayari ninayo milango yote 10(Didnt buy in Dar).
Hoja yangu ya msingi ni kuwa 'kidogo kidogo with determination inawezekana' tusikatishane tamaa.

Kweli mkuu......mkongo ndio habari ya mujini.......milango yake inavutia japo sio tofauti sana na mninga na bei pia kwa hapa nilipo hazipishani sana............
 
Yaani umenena vema sana, Hakuna kitu kinakwaza kama tabia ya kumkatisha tamaa mtu, yey amejitahid kafika hapo na anajua hajamaliza, anajua hatua inayofuata nin, kama aliweza kununua kiwanja, akatafuta raman, akaanza kujenga hadi akafika hapo haiwezekan kuwa hajui anamaliziaje, anayo plan yake namna ya kumaliza, watu unakuja na kuanza kumpigia hesabu za kukatisha tamaa si unafiki huo. wew kama unaona gharama kujenga kwa kudunduliza usimkatishe tamaa mwenzio.

Endelea kusubir uokote pochi ya mzungu ndio utajenga, acha wa2 wajidundulize ila mwisho wa siku ataishia kukaa kwenye nyumba yake na kuepuka kero za kupanga
Umenena kiongozi!
 
Ya kwangu pia hiyo hapo mpaka hapo hata m15 bado...uwanja wa million 3.inawezekana bana

Hongereni sana vijana.......mnahamasisha sana........sio kupiga mdomo na kujifanya sehemu zote za kula bata unazijua..........na kununua magari ya mbwembwe..........kumbe unalala nyumba ya watu.......siku zote hakuna baba mwenye gari jamani.......ni baba mwenye nyumba.........
 
Preta,umenena mom...yaani huwa tunatofautiana sn katika vipaumbele sie vijana..wengi wa vijana dreamz nyingi hulenga kumiliki verosa,alteza,murano and the like..mgusie sasa habari za plot na ujenzi,huchelewi kuonekana una wivu then hujui bata za town..yaani ndo ile kuja kushtukia umri wa le mutuz huu hapa kwenye kona..
 
Last edited by a moderator:
Kitu kigumu ni kupata kiwanja,ujenzi ni majaaliwa kw kuwa tayari unakua na Idea Vijana pambaneni
 
mbona unamtisha?

We muache tu aisee..utamu ngoma tunaijua sisi,anaeogopa acha aendelee kuogopa,ununue kiwanja uanze kusomba mawe,tofali,ujenge,ulipe fundi,ununue maji,uje ushindwe madilisha na plasta na rangi?nani kasema...hahahahaa.hakuna mchezo mtamu kama kujenga aisee,sikuwahi kujua na kudhania kwa kuogopeshwa na watu kumbe wapi bwana.kila kitu kinawezekana bwana,mpaka sasa mimi najua finishing ya nyumba yangu itagharimu kiasi gani,wala sio kitu cha kutisha kama watu wafikiliavyo.
 
Tatizo lao wanataka wahamie papo hapo nyumba ikiwa imekamilika kila kitu na ukicheki kipato chake ni cha kudunduliza..hilo halitakaa lije litimie otherwise liwe jizi km ile mijizi mingine...mbwembwe na mikwala ya kutaka nyumba iwe full furnished zinawafaa wenyewe.nina uhakika mtu anaweza kujenga nyumba bila ya ulazima wa kukopa wala nin...ukizunguka zunguka na kufanya utafiti kwa wengi utagundua kuwa walijenga wakiwa na kias cha kawaida sn cha pesa..mkuu nakuunga mkono
 
Apo tu ishapendeza. Ukiwa na shida na pa kukaa unaweka madirisha yako na milango na choo chako tu unahamia. Mambo ya tiles, sijui tarazo izo mbwembwe tu hata baadae sana unaweza ukaweka
 
Unajua dirisha la aluminium complete haipungui kilo 3 una dilisha 11 mlango mzuri mninga 250000 ceiling gypsum kwa nyumba yako hyo makadilio M 3.5 tiles bado Mabomba mziki wake usikie tu bado shimo la Maji taka bado Fundi hajaimba cement name
Gypsum powder kaka hapo bado sana wiring nilisahau

Acha kutisha watu. Unaanza mdogo mdogo. Dirisha moja. Tiles chumba kimoja. Mirango ya temporary. After few yrs, mtu anaishi kwake. Kikubwa ni kujua unalolifanya, na kutumia unachokipata kwa uangalifu. Kama kipato kidogo usitume mtu usiyemuamini kukusimamia kazi.
 
Back
Top Bottom