Mjadala: Gharama na njia nafuu za kujenga nyumba ya kuishi Tanzania

hv hili jukwaa limejaa wahaya? maana kila anae changia anaeleza uwezo wake kifedha as if ana bonge la roshen, du mnatsha
 
Jamani mimi nina kiwanja Kigamboni maeneo ya Kisota si kikubwa na najuta kwa nini nilikinunua miaka 5 iliyopita kina ukubwa wa SQM 610

nishaurini naweza kujenganini? Maana nilidhani bora kujenga walau kijigorofa kwenda juu kama gorofa mbili hivi maana chini naona space ndogo.

Muhimu kwangu ni sehem ya kupaki gari. kibanda cha mlinzi lakini muhum zaidi uwanza wa nyumba uwe mrefu kwani nyuma ndio naweza kufanya shughuli zenye kuhitaji space

Pembridge-Gardens-W11.jpg

Niko tayari kikuza ili nikajenge shamba nje ya Dar lakini kwanza nishaurini
 
Jamani mimi nina kiwanja Kigamboni maeneo ya Kisota si kikubwa na najuta kwa nini nilikinunua miaka 5 iliyopita kina ukubwa wa SQM 610

nishaurini naweza kujenganini? Maana nilidhani bora kujenga walau kijigorofa kwenda juu kama gorofa mbili hivi maana chini naona space ndogo

Niko tayari kikuza ili nikajenge shamba nje ya Dar lakini kwanza nishaurini

Ningejua kisota ni umbali gani kutoka ferry, ningekushauri vizuri.
Kama sio mbali sana kutoka ferry, jenga apartments (low cost housing) either upangishe au uziuze..
 
Ningejua kisota ni umbali gani kutoka ferry, ningekushauri vizuri.
Kama sio mbali sana kutoka ferry, jenga apartments (low cost housing) either upangishe au uziuze..

Mhh kaka umeoa ukubwa niliokutajia?

eneo hili hapa ni kilimita 7 au 8 toka Ferry

location.png
 
By bwegebwege Kwa kukupa picha kidogo:
Mimi nina ongoing project, imefika kwenye linter, (Nyumba ya kawaida): 1 Masterbedroom moja, 1 Guest Room with attached toilet, 2 other Bedrooms, Study room 1, Laundry, Kitchen, Public Toilet & Bath, Dinning Room na Sitting Room...hadi sasa tayari $65,000 zimekatika! I just received estimates ya kupauwa (Kwa bati pana) ni kama $18,000..hapo ni mbao, mabati na ufundi etc. Sasa nikianza kufikiria finishing nahaisi nitapaswa kuwa na kama $30,000 nyingine (total kuanzia kuezeka)! Hapo sijaweka hesabu ya fence.....
Kwa mantiki hiyo bosi waliosema uwe na kama 100,000,000/= kwa uchache hawajakosea (ingawa mimi nashauri uwe na kama 160,000,000/=

Daaaah! mkuu hizi gharama ni kweli unajenga wewe au unaondolea watu umaskini? These costs are not realistic kabisa! Utafanya watu waogope kujenga aisee, hebu zione mwenyewe kwa hela zetu za bongo:
Fanya rate yetu ni 1600Tsh and here we go:

Imefika kwenye lental cost ni $ 65,000 x 1600 = 104,000,000/=??????????????????????????????????
Kupauwa umeambiwa cost ni $ 18,000 x 1600 = 28,800,000/=
Finishing unakadria cost ni $ 30,000 x 1600 = 48,000,000/=
Total cost bila kuweka wastage etc................... 180,800,0000/=.....??????????????

My take: Hii nyumba naiona ya maajabu, kama umempa mkandarasi ndo anajenga sina ubishi kwa hilo maana najua wapi alipokupiga na unaweza kuongea naye akaimalizia yeye kisha wewe ukamlipa tu pesa ya kupauwa na finishing nyumba ikiwa imekamilika. Kama mtoto wa mjombako ndo anasimamia na kufanya manunuzi yote hongera zako kwa kumwondoa katika njaa. LAZIMA ANUNUE NOAH GHAFLA BIN VUU na......!!
Otherwise unaleta masikhara humu jf kwa kujenga boma kwa 104M kwa nyumba yenye details uloandika hapa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Wana jf mna uwezo wa kujenga nyumba bila tatizo, ila mkiendekeza complications za humu mtazeeka bila kuwa na nyumba hata kidogo. mambo ya kufanya ni haya:
1. NUNUA KIWANJA NA PATA HATI ZOTE
2. PATA MCHORO WA NYUMBA UNAYOITAKA NA ANDALIWA BOQ. KAMA HUWEZI KUITAFSIRI WAAMBIE WAKUTAFSIRIE.
mfano: conc C20, 20M[SUP]3[/SUP]Utahitaji Tripu ngapi za Kokoto, mchanga,mifuko ya cement mingapi n.k.(kubali gharama za watafsiri, QS,Civil Engineers,Technicians wanaweza kufanya hiyo kazi)
3. Anza kazi kwa namna unayotaka.(Ukifanya hivi ujuwe unasimamia mwenyewe au mkeo maana unapilot tayari)

Mkuu unajua kuna watu labda practical hawajafanya hayo hio hesabu labda kwenye tenda za serekalini boma la ukubwa alioleza hata kama itakuwa ni ghali sidhani kama itapita ml 15.
 
Wadau,
Mimi ni mpya hapa na ninahitaji msaada wenu. Nina Sh 28m na nataka kujenga nyumba Kibada Kigamboni. Kiwanja kipo, plan ya nyumba ninayo.
Ukubwa wa nyumba ni 120 sqm
Vyumba vya kulala: 3
Public toilet: 1
Bathroom for inmates: 1
Dining, sitting room and jiko pamoja: 1
Paa: ningependa iwe ya ubora mzuri ingawa pia sijui ni mabati ya aina gani.

Je, hii fedha itakidhi mahitaji ya kusimamisha hii nyumba?

Keyala anza wala usikatishwe tamaa kama kiwanja kipo anza unaweza kuja kukwama kwenye upauzi tena labda kimoja wapo tu either bati au mbao.
 
Mhh kaka umeoa ukubwa niliokutajia?

eneo hili hapa ni kilimita 7 au 8 toka Ferry

location.png

Kiongozi sqm 610 ni kubwa.. Unaweza kujenga maghorofa mawili each sqm 240, three floors, each floor containing two units of two bedrooms, sitting room, kitchen and public toilet... Meaning sixteen families can live on that piece of land you call small.. Inbox me your email if you really want to develope that land.
 
Duh

umenipa moyo kichizi

maana idea ni kutoa kijigorofa kiduchu kama hiki....mbele ni park gari walau 2 lakini muhim nyuma niwe na uwanja walau wa kuanika nguo na kufanya BBQ

Nakucheki kwenye PM sasa hivi

Pembridge-Gardens-W11.jpg
 
Jamani nilikuwa nafanya design ya low cost house kigorofa kimoja.
Na baadae nikakaa na engineer then qs.
Hivyo tukawa timu kamili ya mimi architect, structural engineer na quantity surveyor.
Tumekuja na design ya gorofa moja yenye vyumba 4, sitting, dining ndogo na jiko kwa tsh 65 million.
Kesho nitawaonesha kwenye picha muonekano wa jengo hilo
 
Nitaendelea kufanya research wapi watanzania tunakosea hadi tunajenga kwa gharama sana.
Lakini pia nitaendelea kuwashauri wateja wetu jitahidini sana kutafuta competent professional itakusaidia sana kuliko kukimbilia kwa wanafunzi kisa gharama ndogo.
Ku practice kwangu muda mrefu kunanifanya nitambue essence ya low cost house lakini zaidi kutambua makosa makubwa yanayofanywa na wateja wetu.
Shukrani pekee ziwaendew wateja wangu ambao wana exposure kubwa nje ya nchi hivyo wakinipa kazi wakisema low cost wanamaanisha kweli low cost.
 
Jamani mimi nina kiwanja Kigamboni maeneo ya Kisota si kikubwa na najuta kwa nini nilikinunua miaka 5 iliyopita kina ukubwa wa SQM 610

nishaurini naweza kujenganini? Maana nilidhani bora kujenga walau kijigorofa kwenda juu kama gorofa mbili hivi maana chini naona space ndogo.

Muhimu kwangu ni sehem ya kupaki gari. kibanda cha mlinzi lakini muhum zaidi uwanza wa nyumba uwe mrefu kwani nyuma ndio naweza kufanya shughuli zenye kuhitaji space

Pembridge-Gardens-W11.jpg

Niko tayari kikuza ili nikajenge shamba nje ya Dar lakini kwanza nishaurini

Toa vipimo vyake mean marefu na mapana.
Pia je we kwa sasa unafikilia nini nyumba ya kuishi wewe au kupanga.
Zaidi ni mbunifu majengo by professional so tunaweza kusaidiana mawazo zaidi kwenye hilo
 
Sijui unatumia aina gani ya matofali, lakini kama ni yale ambayo yamezoeleka yenye vipimo vya 18"x9"x5". Mzunguko wa chini utakuwa na matofali 4+6+4+6=20, na kama yatajengwa kwa kusimama na banda lako liwe na kozi 12, maana yake itakuwa ni tofali 240, hapo hakuna cha mlango wala dirisha, sijazingatia foundation. Lakini kama ni kibanda cha biashara (frame), utaondoa tofali za upande mmoja wa ft 6, hivyo utaondoa tofali kama 40, ukiweka na msingi roughly ni kama tofali 300.
 
We mkali brother. ...hivi kama ni frame yenye kozi 9 tu....mlango na dirisha LA foot 3x3 yanaweza fika hiyo idadi...mkuu
 
Wakuu,

Nataka kuanza ujenzi wa nyumba ya makazi ya gorofa moja kwenye kiwanja kilichopimwa na serikali, je kuna taratibu zozote natakiwa nifuate kama vibali n.k?

Naomba mnielimishe ndugu zangu.
 
naskia eti kwenye hizi gorofa inatangulizwa miguu ya wanyama kama kinga ya nguzo usipfanya ivo litaanguka, huwa naskia skia tuu ila sina uthibitisho
 
Back
Top Bottom