Mizengo Pinda aomba kujiuzuru

kama kweli mh. Pinda ameaamua kustep down, basi na aendelee na msimamo wake, na wala asikubali kuombwa kuendelea kwa namna yoyote, maana bosi wake ni kigeugeu hakawii kukubali kumvusha ngambo ya mafuriko na kisha kumtosa katikati ya maji yenye kasi. Pinda usipindishe maamuzi yako.
 
Hivi kumbe watu bado kabisa hamjui katiba. Kwani mmesahau kuwa waziri lazima atoke miongoni mwa wabunge? Sasa Lipumba ni mbunge wa wapi? Hili haliwezekani msitupotezee muda.

Bado anaweza kuteuliwa na Rais kwa sababu katika inamruhusu bwana mkubwa kuteua wabunge kumi na kwa kumbu kumbu yangu bado hazijaisha... Isipokuwa waziri mkuu mbali ya kuwa mbunge lazima awe mbunge wa Jimbo na siyo wa viti maalum au ubunge wa kuteuliwa... Nawasilisha!
 
Hivi kumbe watu bado kabisa hamjui katiba. Kwani mmesahau kuwa waziri lazima atoke miongoni mwa wabunge? Sasa Lipumba ni mbunge wa wapi? Hili haliwezekani msitupotezee muda.

Rais bado ana nafasi saba za kuteua wabunge.....anaweza kumteua na akasubili bunge la bajeti akaapishwa than akamteua kuwa waziri mkuu.
Mnapoambiwa kuwa JK atarikarabati upya baraza la mawaziri msimtegemee leo huyu jamaa aisee..... ila option hiyo inawezekana
 
Bado anaweza kuteuliwa na Rais kwa sababu katika inamruhusu bwana mkubwa kuteua wabunge kumi na kwa kumbu kumbu yangu bado hazijaisha... Isipokuwa waziri mkuu mbali ya kuwa mbunge lazima awe mbunge wa Jimbo na siyo wa viti maalum au ubunge wa kuteuliwa... Nawasilisha!

ingawa nimelike comment yako ila nilitaka kujua .....je kuna kipengele kinachosema (ktk katiba) kuwa ni lazima awe kutoka jimboni???
Nauliza
 
ingawa nimelike comment yako ila nilitaka kujua .....je kuna kipengele kinachosema (ktk katiba) kuwa ni lazima awe kutoka jimboni???
Nauliza

Katiba: Ibara ya 51(2):
Mapema iwezekanavyo, na kwa vyovyote vile ndani ya siku kumi na nne, baada ya kushika madaraka yake, Rais atamteua Mbunge wa kuchaguliwa kutoka katika Jimbo la Uchaguzi anayetokana na chama cha siasa chenye Wabunge wengi zaidi Bungeni au kama hakuna chama cha siasa chenye Wabunge wengi zaidi, anayeelekea kuungwa mkono na Wabunge walio wengi kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, naye hatashika madaraka hayo mpaka kwanza uteuzi wake uwe umethibitishwa na Bunge kwa azimio litakaloungwa mkono na kura za Wabunge walio wengi.
 
Magufuli Pombe John,Mzee wa takwimu, Mwanry Aggrey na makelele yake ya kujihami, na yule nanihii, huyu jamaa yetu huyu..kanitoka jina. hawa nilikuwa napima uwezo wao wa ku-crash wasiojiweza bungeni.
Kabla ya kuchagua hao mawaziri Mkuu wafanyiwe vetting kupata watu waadilifu, huyu Mhe Aggrey Mwanry amefunga fensi kubwa hapa A Town lazima naye ajieleze kapata wapi hizo fedha za kununua maeneo makubwa hivyo katikati ya mji wa Arusha???? Mkulu kama anaipenda Tanzania aweke watu waadilifu ingalao kulinda kile kilichopo na kuleta unafuu wa hali ya kiuchumi kwa Watanzania!!!!

 
Wana-JF Raia Mwema ninalo Mwandishi anajiita MsomajiRaia@yahoo.com na ndiye aliyeandika kila awamu ina rekodi ya kuua.toleo no. 232 la 28/3/2012 na Mhariri Mkuu kukanusha kwa maandishi madogo ukurasa wa mbele toleo no.235 mauaji yake mtoa thread kaacha maneno makusudi yasemayo Natamani hizi ziwe ni tetesi za kweli km zilivtto zingine
Kwa ufupi simsemei Pinda ila nuu uchochezi naq huenda Gazeti nalo llikakanusha tena

Je, wewe makusudi yako ya kuacha paraghraph zote 29 zilizobaki ni nini? Huwezi kuwafundisha watu kununua gazeti kama nimesema machache yaliyomo.
 
Tetesi na vumi unaleta jukwaa la siasa? na moderators kimya! Ngoja Ribosome alete hata habari za kweli uone nyuzi zinavyoyayushwa.
 
Mizengo Pinda akijiuzulu sawa, lakini atapunguza imani ya wananchi kwa Kikwete. Pinda pia amekuwa hana maamuzi yake binafsi hata pale alipoamini yukosahih. kwa hiyo ni dalili wazi kuwa anamsusia Kikwete. Ni vema, kama yasemwayo ni kweli, angepaswa kujiuzulu kabla na sio sasa
 
Ni bora aondoke nadhani amedharirishwa na kikwete vya kutosha. Kuanzia jairo, posho hadi mawaziri. Akiendelea kuwa w/m nitamcheka milele
 
Msimwonee Pinda Jamani, Katiba yenu ndiyo mbovu inayomdhalilisha waziri mkuu kuonekana kilaza na kiraka mbele ya Watanzania na hivyo kushikwa masikio na JK.

Kipindi cha Jairo alionyesha msimamo na baadaye kuzenguliwa na JK na mfano mwingine ni huu wa sasa hakuweza kuwawajibisha mawaziri na baadhi yao kutunisha misuli.

Hiki cheo cha Uwaziri Mkuu lazima kifanyiwe mabadiliko makubwa kikatiba ya kufanya maamuzi na siyo kuwa kama cheo cha house boy au house girl.

Mzee Pinda huhukumiwi ila pumzika umwachie mwingire cheo hiki fake(kanyaboya) naye apate mafao kipindi chake kikipita 2015 kwa amani au kwa shari, amen.
 
Mbona el alikuwa anawawajibisha wakurugenzi na watumishi wengine huyu mizengo amemwajibisha nani?
 
Kizee kinafiki hicho!

Mimi sikiamini mpaka nione barua yake ya kujiuzulu. Kisubiri tu Mkw.ere aking'oe.
 
... endapo Prof Lipumba atakubali kujiunga na hili li baraza la mawaziri uozo la CCM hakika nitamdharau milele na kutilia wasiwasi utashi wake na kazi ya usomi wake pia!!!!!!!!

Acheni CCM kimalizie uchafu wake wote kama walivyouanza mara baada ya Mwalimu Nyerere kufa ili hukumu ya walalahoi kwa chama hiki hivi karibuni isije ikasambaa hata kwa vyama ambavyo havihusiki na uhandisi wa UFISADI wote wanaolifanyia taifa hili.


Naomba ufafanuzi wa neno UHANDISI
 
Huyu jamaa ni mtu hatari kwani anatudanganya eti yeye ni mtoto wa mkulima huku akiwa kimya nchi lipotafunwa na watendaji wake tena wanaotembelea magari ya mabilioni ! Nafikiri ameiga staili ya maneno maneno kama bwana mkubwa wake! Aende tena hana lakukumbukwa zaidi ya kipindi chake cha propaganda kisicho na tija bungeni! nenda nenda nenda baba tena kamwe usifilirie kurudi hata kwa ubalozi
 
Back
Top Bottom