USSR, World of socialism

Comred Mbwana Allyamtu

JF-Expert Member
Jun 28, 2016
348
847
MUUNGANO WA KISOVIET YA URUSI: DOLA-HIMAYA NA MILIKI KUU YA 7 YA DUNIA KATIKA ULIMWENGU WA KIJAMAA, URUSI IKAWA UKOMINIST NA UKOMINIST UKAWA NDIO MOYO WA URUSI.

Na. Comred Mbwana Allyamtu
Thursday- 27|08|2020.
Dumila Town- Morogoro, Tanzania

Muungano wa Kisoshalist wa Jamuhuri ya Soviet uliundwa baada ya Mapinduzi ya Oktoba 1917, baada ya kikosi cha bolshevik, wakiongozwa na Vladimir llich Lenin walipo ipindua Serikali ya kifalme iliyokuwa ikiongozwa na Tsar Nicholus.

Mapinduzi hayo yalifanikiwa baada ya Jeshi jekundu la Bolshevik kuvishinda vikosi vya serikali ya kifalme, na mnamo 1922 chama cha Bolshevik waliofata itikadi ya Kikomunisti waliuunda taifa la Soviet na umoja wa jamhuri ya Urusi.

Hivyo basi.....

Neno soviet limetokana na neno la Kirusi "Sovet (Kirusi: совет), linalo maanisha "baraza", "mkutano", "ushauri", "maelewano" au "makubaliano".

Hivyo Jamuhuri ya Kisovieti ya Urusi ni muungano uliokubaliana kuanzishwa chini ya mfumo wa kufuata siasa zenye mrengo wa Kisoshalist ambao baraza la uongozi litasimamiwa na mfumo wa siasa za mrengo wa shoto za kikomunisti.

Umoja wa kisoviet uliundwa na jumla ya nchi 16, ikiwa na ukubwa wa eneo za kilomita za mraba 17,075,200 milioni sawa na maili 6,592,800, huku majira ya saa yanayotumika katika taifa hilo ambalo ni taifa moja linalotumia majira kumi na moja (11) tofauti ya saa (time zones ), Yani ukiwa ndani ya Urusi maeneo Kumi na moja hupishana majira.

Kufuatia kifo cha Lenin mnamo 1924, Joseph Stalin aliingia madarakani, Stalin alikandamiza upinzani wote wa kisiasa ndani ya Chama cha Kikomunisti, aliweka itikadi ya serikali kua Marxism-Leninism, akanzisha uchumi uliopangwa na serikali, nchi ilipitia kipindi cha ukuaji wa haraka wa uchumi na ujumuishaji wa kulazimishwa, ambayo ilisababisha ukuaji mkubwa wa uchumi, lakini pia ilileta njaa kubwa ya mwaka 1932-1933.

Kufuatia kifo cha Stalin mnamo mwaka 1953, kilifatia kipindi kilichojulikana kama de-Stalinization na Khrushchev Thaw kilitokea chini ya uongozi wa Nikita Khrushchev, Nchi iliendelea haraka kiuchumi, kwa kuwa mamilioni ya wakulima walihamishiwa katika miji yenye uchumi mkubwa, USSR ilichukua nafasi ya kwanza kabisa kama taifa lilokuwa na maendeleo makubwa katika maisha ya binadamu duniani, Mnamo miaka ya 1970, kulikuwa na marekebisho mafupi ya uhusiano na Marekani, lakini mivutano ilianza tena wakati Umoja wa Kisovieti ulipotuma vikosi huko Afghanistan mnamo 1979.

USSR ilizalisha mafanikio makubwa ya kijamii duniani hasa mafanikio ya kiteknolojia na uvumbuzi wa karne ya 20, pamoja na mageuzi ya kwanza ya afya ulimwenguni, kwani Urusi ndio ilikuwa nchi ya kwanza kupata maendeleo kwenye suala la afya duniani, satelaiti ya kwanza kurushwa angani ilirushwa na USSR, wanadamu wa kwanza kwenda angani na kutua kwenye sayari nyingine kama mwezi na Venus walitoka Urusi.

USSR ilikuwa na uchumi mkubwa duniani na ndio nchi iliyokuwa na ukubwa wa jeshi kubwa zaidi duniani, USSR ndio nchi muasisi wa kuanzisha silaha za nyuklia, pia Ilikuwa mwanzilishi wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na pia mwanachama wa Shirika la Usalama na Ushirikiano huko Ulaya mashariki, Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Ulimwenguni na mjumbe anayeongoza Baraza la Msaada wa Uchumi duniani.

Sasa turudi nyuma kidogo........

URUSI ni moja kati ya nchi zenye historia kubwa sana ya kufurahisha Kwanza Urusi zamani iliitwa Russian Empire Kabla ya kuja kuitwa USSR na baadae Russia.

Haikuwa na eneo kubwa huko mwanzo kama unavyoliona sasa, Urusi ilitawaliwa kwa zaidi ya miaka 300 na familia ya RAMANOV ambayo utawala wake ulifikia kikomo mwaka 1917 baada ya mapinduzi matakatifu ya wafanyakazi na wakulima na sehemu kubwa ya wakomunisti kama nilivyo eleza huko juu.

Kihistoria mfalme anayekumbukwa kuipanua urusi kuwa kubwa mara mbili anaitwa "Czar Peter the great" au St.Peter kama ambacho baadae mji wa St Petersburg ulivyo kuja kipewa jina kwa heshima yake.

Urusi ilikuwa na nguvu kwa miaka mingi kijeshi kwasababu ya ukubwa wake, rasilimali nyingi na hali yake ya kijeografia ambapo ni baridi sana utoweza kuruhusu wageni kuvamia kirahisi mfano mzuri ni pale ambapo mfalme Napoleon Bournaparte wa Ufaransa alivyoivamia na jeshi la watu kama laki sita hivi mnamo miaka ya 1800's na kupigwa vibaya na mfalme Alexander wa Urusi ambapo aliiamuru miji yote ichomwe moto na kisiachwe chakula ili wafaransa wakija wapigwe na baridi kali ili wafe na kwa bahati nzuri ilitokea hivyo.

Kadiri miaka ilivyoendelea Urusi ikaanza kuwa dhaifu kwasababu ya mfumo wa Feudalism ambao uliruhusu rushwa na utawala wa watu wachache juu ya wengi walio maskini,kumbuka urusi ni moja ya rainbow states since ina multiple ethnical groups, kama Caucasian, Jews, Mongols...

Urusi ilijiingiza kwenye struggle for power mnamo miaka ya 1800's hadi 1900's na matifa ambayo ni madogo kuliko yeye lakini yalikuwa tayari yamesha fanya mabadiliko ya kiviwanda kuliko yeye hivyo kupelekea kushindwa vita hata na kitaifa kama Japani na Uturuki.

Mnamo miaka ya 1914 ilitokea vita ya dunia ambapo mfalme wa Urusi bila kufikiria aliliingiza taifa la Urusi vitani kisa kulinda tu heshima yake,wakati huu Urusi ilikuwa haina silaha za kutosha na za kisasa kama automated rifles,aircrafts,tanks and submarines hivyo alitegemea sana silaha kutoka kwa Muingereza,..

Mrusi alijiunga na muingereza na Mfaransa kuwapiga adui na majirani zake Germany Empire, Uturuki kipindi hicho ni Ottoman Empire na Austria, Warusi wengi kama 4 million walikufa hivyo kuifanya Urusi kuwa Taifa maskini sana na chovu kuliko yotee ulaya.

Vuguvugu la mapinduzi..............

Mnamo mwaka 1917 mfalme wa Urusi alianza kuua wanaharakati ambao walitaka asitishe vita na kufanya mabadiliko ya kimfumo,watu kama Vladmir Lenin walikuwa nje ambapo alirudi mwaka 1917 kuendesha mapinduzi makubwa ya kikomunisti ambayo yalipelekea Civil war hadi mwaka 1919 ambapo mataifa mengi dunian hayakupenda ukomunisti hivyo yakasupport wapinzani wa Lennin ila walishindwa.

Baada ya mapinduzi ya chama cha Bolsheviks ambacho kilijiita chama cha watu wote wa tabaka la chini kama wakulima na wafanyakazi wa aina zote waliokua wakifanya kazi ndani ya serikal ya Tsar au zar au emperor au kwa kiswahili fasaha ni "Mtawa" ambao waliokua wanatawala dola ile ya Urusi toka miaka ya 1880 na 1894 ambao walibadilisha fikra za watu wa Urusi ambao akili zao ziliamka kwa ajili ya kudai haki kwa ajili ya mabadiliko.

Kwamba............

Kabla ya Vladimir Lenin na marafiki zake wakubwa wawili Joseph Stalin na Leon Trotsky ambao walizaliwa mwaka mmoja 1879 tayari mapambano katika nchi ya Urusi yalikua yameanza mda kudai Uhuru wa watu ambao walikua wakiteswa na tawala ya serikal ya Alexander lll ambapo yeye aliondoshwa madarakan mwaka 1894 na kufanya Czar Nicholas ll aingie madarakani kwa kuitawala Urusi hivyo watu pia waliendelea kudai haki zao kwani nae aliwanyanyasa watu wa tabaka la chini.

Mwaka huo watu wa jiji la Petrograd waliandamana katika kasri la mfalme Alexandre ll kwa ajili ya kudai haki zao lakn walipigwa risasi na kadhaa kujeruhiwa na wengne kuuwawa hivyo watu kushindwa kufanya mapnduzi uko urusi .

Mwanzo wa 1914 Wakati vita ya kwanza inaisha urusi ilikua upande wa allied yana katika shirikisho la nchi zilizokubaliana kuisaidia kijeshi Uingereza, Ufaransa, n.k Ujerumani walivamia baadhi ya sehemu za Urusi ya zamani na sehem kadhaa ambapo vikosi vya Urusi vilipigwa vibaya na Wajermani hadi mwaka 1916 Warusi zaidi ya 50000 walikua either wameuawa au wamejeruhiwa na kupotea (missing in action) sababu za kushindwa kwa vita hii

kwanza kutojiandaa kivita ambapo hawakua na silaha za kutosha mda mwingne walitegemea za watu waliokufa kivita zaidi APA (tazama enemy at the gate) hivyo walipata gharama kubwa za maandalizi na kufanya watu maisha yapande.

Pili ni vyakula Vingi kupelekwa kwa wanajeshi kukosa chakula mavazi na kadhalika hivyo kumfanya mtwawa Alexandre ll kuingia kama command person na madaraka kumuachia mke hapo lilikua kosa kwake kwan kwa mda huo alishindwa kutawala vyema na vitendo vya rushwa kuongezeka na watu ikiwa ni pamoja na kupanda kwa gharama za maisha kama kutokuwepo kwa vyakula hasa jiji la Petrograd

Na kufanya watu waanze kuunda fikra za mapambano na kufufuka dhana ya mapinduzi iliyokuwa imeshidwa mwaka 1905 waongeze mapambano hasa kuanza kuundà vyama vya Kijamaa kwa kufuata dhana ya Karne Max.

Kwa wakati huo Urusi walikuwa wakitumia calendar iliyokuwa inayoitwa Julian ambayo kimsingi ilikua haendi sawa na nchi nyingne mwezi wa pili wa mapinduzi yaliyomng'oa Nicholas ll na kufanya kijana mdogo anayeitwa "Alexander Kerensky" apewe serikal ya mda lakin naye nchi ilionekana kushindwa kutawala kwa kutokua na mfumo mzuri wa kitawala.

Mapinduzi ya October 1917 toka February hadi October Lenin alirudi Petrograd kupitia Ujerumani na kuingia Urusi kuongoza kusonga mbele kwa chama cha Bolshevik kwakua Lenin aliingilia mji wa "Petrograd" hivyo Basi Mapinduzi hayo yalipewa jina la "Leningrad" kwa maana ya (mji wa Petrograd na Lenin).

Hivyo Basi pamoja na Lenin kuingia Urusi alianza kukusanya wanachama na wengi zaid hadi September alikua na member 200000 mapinduzi ya oktoba waliomwondoa mtawa Alexander Kerensky na Vladimir Lenin kuingia madarakan kupitia chama cha Bolsheviks ambapo alisaini mkaba kuziachia baadhi ya nchi ziwe huru kama Poland Finland n.k.

Makao makuu ya chama cha Bolsheviks yalihamia Moscow kutoka Petrograd maarufu kama St.Petersburg city sasa 1918 na sasa Lenin alianza kukumbana na changamoto za kiutawala kama kuibuka kwa migogoro ya ndani (Civil war) mwaka 1918-22 Watu walikua na ushirikiano mkubwa sana kwa Lenin na walikua na kikosi chao cha red guard ambapo 1919 red army iliundwa rasimi kama kikosi cha umma na Leon Trotsky aliteuliwa kuwa general secretary

Jeshi hilo la umma pia Ukraine ilipewa jukumu maalumu ilijulikana kama Green army kwa ajili tu ya kusaidiana na Lenin nchi kama USA, UK, Japan na France walitoa misada ya kijeshi kwa white army kupigana na Bolshevik part lakn sapoti aliokua nayo Lenin alishinda vita hio mwaka 1922 ikawa imeisha huku Urusi yote ikawa Chini ya chama cha Bolshevik.

Hivyo basi.................

Kabla ya hapo urusi ilijulikana kama RSFSR 1917 yani (Russian Soviet Federal Socialist Republic) ambapo neno "Soviet" lilitolewa kutoka kwenye chama cha "Petrograd Soviet council" ambapo neno "Soviet" linamaana ya "council" kwa Lugha ya kingeleza yani "Baraza" kwa kiswahili, kwa matiki hiyo na ndipo kutokana na kuwepo kwaa vyama kadhaa vya kijamaa wakaunda umoja huo RSFSR na hatimye mwaka 1922 ikaundwa USSR.

USSR yani (Union of Soviet Socialists Republic) iliundwa na pia ilijulikana kama "Soviets union" Urusi chini ya Lenin na ukomnisti iliweza kuunda nchi inayoitwa USSR au The UNION OF THE SOVIET SOCIALIST REPUBLICS au CCCP, ambayo iliweza kuanzisha ujamaa ambao kwanza uliwaunganisha warusi wote kwasababu walikuwa na uchumi sawa na hali sawa, pili iliwekeza sana kwenye elimu na pia mwisho jeshi la Urusi lilikuwa linaanza kufundisha watoto wakiwa na umri wa miaka 6.

Lenin aliunda mifumo ya kipelelezi iliyoitwa Cheka, NKVD na GRU hivi ndivyo vyombo vilivyoifanya Urusi iwe leo unavyoiona.

Hapa ni kwamba......................

Urusi ilipo undwa mwaka 1917, iliamua kuundwa kwa misingi ya ujamaa, ujamaa ulio jengwa kwa miundo ya Ukominist.

Ukominist ndio ukawa moyo wa Urusi na Urusi ikawa Ukominist, misingi hii ikalifanya taifa la Urusi kuwa taifa lenye maadui wengi duniani, hasa mataifa ya magharibi yakiongozwa na Marekani.

Kufatia hatua hii Urusi ikaunda shirika la kijasusi ili kulinda maslahi na usalama wa Shirikisho la Kisoviet ya Urusi liloitwa KGB.

KGB, au Komitet Gosudarstvennoy Bezopasnosti (Committee for State Security) lilifahamika zaidi kama shirika la ukusanyaji wa taarifa za siri ambalo lilikuwa linafanya kazi zake ndani la muungano wa nchi za Kisoviet lilipata kuwepo katika karne ya 20, shirika hilo limebadilishwa majina tofaut tofaut na kufanyiwa maboresho zaidi ya mara 5 tokea kipindi cha mapinduzi ya Urusi ya mwaka 1917.

Jina la KGB lilikuwa jina rasmi kuanzia mwaka 1954 hadi mwaka 1991, Kazi za shirika ziliongezwa zaidi kutoka katika mambo ya siasa ambayo yalikuwa yakifanywa kwenye shirika la mwanzo liloitwa Okhrana, lilokuwepo kwenye kipindi cha utawala wa Tsar Nicholas II.

Mwaka 1917 Illich Vladimir Lenin aliamua kuunda shirika la kijasusi la Cheka kwa kutumia mabaki ya shirika la mwanzo la kijasusi liloitwa Okhrana, hili shirika la KGB liloundwa baadae lilipokea majukumu kutoka kwenye hiyo taasisi ya kijasusi ya Cheka ambayo yenyewe ilikuwa na majukumu hadi nje ya Urusi katika kukusanya taarifa za kijasusi na pia kulinda siri za kisoviet na Ikiwa ni pamoja kukusanya taarifa za mataifa hasimu ya nje.

Turudi nyuma kidogo....................

Mwaka 1880 Tsar Alexander II mfalme wa Urusi wakati huo aliunda idara ya polisi kwa ajili ya taifa la Urusi, ambayo kwa wananchi wengi wa Urusi shirika hilo lilitambulika kwa jina la Okhrana.

Majukumu ya mwanzoni ya shirika hili ilikuwa ni kuchunguza, kujipenyeza na kuzuia itikadi za siasa kali katika taifa hilo la Urusi katika kipindi cha karne ya 19 na 20, kwa kuweka watu wa Okhrana katika makundi mbali mbali ya kimapinduzi.

Tsar aliendelea kujulishwa aina zozote za mipango ya hatari katika utawala wake na kuweza kuzuia mipango hiyo kwa haraka zaidi.

Mwaka 1908 na 1909, wanachama wa 4 wa kamati ya St.Petersburg ya chama cha Bolshevik Party walikuwa ni maafisa wa Okhrana, Nicholas II alikuwa na uhakika zaid wa kiusalama kwa jinsi alivyoweza kujipenyeza katika makundi ya kimapinduzi na hili lilipelekea kupuuzia onyo la mapinduzi ya karibuni ya mwezi 11 mwaka 1916 kutoka kwa baadhi ya wanachama wa serikali yake ambayo ilikuwa inaelekea kuanguka

Mwezi wa pili mwaka 1917 zaidi ya wafanyakazi 400,000 wa viwandani wa jiji la St. Petersburg walichoshwa na hali ya njaa na mazingira mabovu ya kufanyia kazi, katika maandamano haya, Tsar Nicholas alishindwa kuyazuia kwa sababu katika makundi yote ya kimapinduzi ambayo Okhrana walikuwa wanafuatilia mienendo na taarifa zao, makundi haya ya kimapinduzi hayakuhusika katika maandamano haya ya wafanyakazi kupinga
Utawala wa Tsar Nicholas.

Maandamano katika miji, Jeshi la Urusi liliamua kusimama pamoja na wananchi kupinga Serikali wakati serikali inavunjika, bunge la Nchi hiyo (DUMA) kuona hivyo liliamua kushikilia madaraka katika kipindi cha serikali ya mpito, pia Tsar alilazimika kung'atuka madarakani.

Katika kipindi cha miezi 9 ya kutokuwa na demokrasia ya kueleweka iliwapa uhakika wakina Illich Vladimir Lenin na chama chake cha Bolshevik ambapo kwa siri waliweza kuunganisha nguvu zao, Baada ya mapinduzi ya mwezi wa saba mwaka 1917 kushindwa kufanikiwa, chama cha Bolshevik waliweza kupata ushawishi mkubwa katika kamati la jeshi la mapinduzi ambapo mwaka huo huo waliweza kuvamia Winter Palace (jumba la utawala wa kifalme enzi hizo) na jeshi la mapinduzi hawakupata upinzani sana kuweza kudhibiti winter palace na hivyo Lenin akawa kiongozi wa serikali mpya ya Urusi

Lenin alikuwa ana amini zaidi katika mabavu/utemi na hii ni kutoka na kuvutiwa zaid na kikundi cha "The jacobs" kilianzishwa huko paris mwaka 1789 hiki kilikuwa ni chama cha kisiasa chenye ushawishi mkubwa katika kipindi cha mapinduzi ya Ufaransa na kilikuwa ni chama chenye itikadi kali na kilikuwa chama ambacho hawana huruma.

Lenin alimteua Feliks Dzerzhinsky kama mwenyekiti wa baraza la People’s Commissariat katika mambo ya ndani (NKVD), Shirika hili majukumu yake ilikuwa ni kuhakikisha wanazuia na kuzima harakati zozote za mapinduzi ndani ya Taifa hilo, kwa kuhakikisha wanafanya kazi kwa kiwango bora zaidi.

Baadae Vecheka ilianzishwa kama mbadala ya NKVD , jina la CHEKA lilifupishwa na watu tu wakati wa kutamka, shirika hili lilikuja kuwa
msingi kwa KGB.

Baadae Lenin alimteua Dzerzhinsky kuwa mwenyekiti wa shirika hilo, huyu bwana Dzerzhinsky aikuwa ni mchoraji ambaye aliwahi kufungwa jela miaka 11 kwa tuhuma za kujihusisha na njama za mapinduzi kipindi cha utawala wa Tsar, hili lilikuwa ni chagua la kwanza kabisa la Lenin la kumteua kuwa mwenyekiti wa shirika la CHEKA.

Baada ya Bwana Dzerzhinsky kuwa mzoefu kwenye nafasi yake hiyo alianza kufanya mabadiliko ya kiutendaji na kimuundo ndani ya shirika la CHEKA ambapo aliamua kuhamisha makao makuu ya shirika la CHEKA kutoka St.Petersburg kwenda jiji la Moscow ambapo shughuli za shirika hilo la CHEKA walizihamishia kwenye jengo la zamani la kampuni ya Bima ya All Russian Insurance, Shirika liliongezewa nguvu kutoka kuwa chombo cha kuchunguza hadi kuwa na uwezo wa kumata, kufungulia kesi na kuwa na uwezo wa kufunga watuhumiwa wowote.

Pia CHEKA walipewa uwezo wa kuongeza makambi kwa ajili ya kuwafunga wafungwa wote wa kisiasa na wengine wa kijasusi.

Kabla ya kubadilishwa jina shirika la CHEKA walihusishwa na mauaji ya Watu tofauti 500,000 tokea shirika hilo lianzishwe kwa ajili ya kuboresha mahusiano ya kibiashara na kiuchumi na mataifa ya magharibi na hivyo shirika la GPU lilianzishwa kuchukua nafasi ya CHEKA ambapo kimamlaka lilikuwa chini ya NKVD na halikuwa na nguvu sana kama ilivyokuwa kwa CHEKA lakin baadaye kwa shinikizo la Lenin bwana Dzerzhinsky aliweza kubakia kuwa mwenyekiti wa GPU na aliweza kufanya shirika la GPU kuwa na nguvu sana kama kipindi cha CHEKA.

Baaada ya kupatikana kwa katiba mpya ya Muungano wa Kisoviet mwezi wa saba mwaka 1923 GPU lilibadilishwa jina na kuitwa OGPU likiwa na lengo la mshikamano ambapo Lenin alikuwa anataka kutimiza ndani ya Taifa hilo la Kijamaa kuwa wenye mshikamano

Mwaka 1924 baada ya Lenin kufariki dunia, Joseph Stalin alikuwa kiongozi wa taifa hilo na hivyo Dzerzhinsky ambaye alikuwa anamuunga mkono Joseph Stalin kipindi cha harakati za kupata uongozi, kupitia hilo Joseph Stalin aliamua kumwacha abakie katika nafasi ya kuwa mwenyekiti wa shirika la OGPU na baada ya Dzerzhinsky kufariki mwaka 1926 nafasi yake ilichukuliwa na Vyacheslav Menzhinsky.

Moja ya majukumu ya OGPU ilikuwa ni kuhakikisha wananchi wote wa taifa la Kisoviet wana utii, ambapo Joseph stalin alianzisha mashamba ya ujamaa kwa wanananchi wote kuhakikisha wanakidhi mahitaji ya nje OGPU.

baada ya kifo 1934 cha Vyacheslav Menzhinsky ambacho kilikuwa ni kifo chenye utata sana, nafasi yake ilikuja kujazwa na Genrikh Yagoda ambaye kitaaluma alikuwa ni mfamasia, chini ya utawala wake OGPU waliweza kupanua maabara zake na walianzisha tafiti za kisayansi, katika tafiti za kibailojia na kemikali za kiangamizi, ambapo Yagoda mwenyewe alipenda zaidi kufanya tafiti za binadamu akiwatumia wafungwa wa makosa mbali mbali, baaaye Yagoda alikuja kuuliwa baada ya kukili kosa la kufanya mauaji ya Menzhinsky ili aweze kushika nafasi ya uenyekiti wa shirika la OGPU.

Nikolai Yezhov alichaguliwa mwenyekiti mpya wa OGPU, katika kipindi hiki matukio ya kigaidi ndani ya Taifa la kisoviet yalikuwa yamefikia kilele, katika kipind hiki vijana 3000 wa Yagoda waliuliwa kati ya mwaka 1936 na 1938, na baadaye Stalin kwa hofu ya kuja kushindwa kumdhibiti Yezhov wakiwa pamoja, Stalin alimpiga risasi Yezhov na kumuua ilikuwa ni mwaka 1938 baada ya hapo aliteuliwa Lavrenti Beria kuwa mwenyekiti mpya wa OGPU
aliongoza kwa miaka 15 ambapo Beria alikuwa ni kiongozi mwenye Akili sana ambapo aliweza kutanua NKVD ikiwa chini ya OGPU na mwaka 1941 mashirika yalitenganishwa ambapo shirika jipya la NKGB likaundwa kutoka kwenye OGPU.

Hawa NKGB wao walikuwa na wajibu wa usalama wa ndani wa taifa hilo la usoviet na kuzuia aina yoyote ya kazi/mipango ya majasusi kutoka nchi zingine, kusimamia makambi ya kukusanya na kusimamia maaskali katika vita ya msituni na kazi mbalimbali kipindi cha vita na mjeruman wakati wa vita kuu ya pili ya dunia.

Mkuu wa kwanza wa shirika jipya la NKGB alikuwa anaitwa Vseveolod Merkulov ambaye alikuwa ni mtiifu sana kwa Beria na hivyo kugeuza NKGB kama chombo cha Beria, Stalin ili kumdhibiti Beria ndani ya NKGB mwaka1950 Merkulov alibadilishwa na Viktor Abakumov akawa boss wa NKGB ambaye hakuwa na mahusiano ya karibu na Beria lakin baadaye Beria aliweza kumshawishi Stalin kuwa Viktor Abakumov alikuwa anataka kumpindua hivyo mwaka 1951 aliuliwa.

Baada ya kifo cha Stalin 1953 Beria alijaribu kushika nafasi ya Stalin kama dikteta wa taifa hilo lakin alidhibitiwa na kuuliwa mwaka 1953, baada ya Nikita Khrushchev kuwa kiongozi wa Taifa hilo la kisoviet aliweza kufanya mabadiliko ya shirika hilo la NKGB na kilipa jina la mwisho mwaka 1954 na kuitwa KGB ambapo shirika lilikuwa na wajibu wa kudhibiti jeshi la polisi, kuendesha oparesheni mbali mbali, kulinda mipaka ya nchi na kuhakikisha usalama wa ndani wa taifa hilo.

KGB ya mwaka 1954 mpaka 1991...........

Kwa watu wengi tumezoea kuita KGB ila kirefu chake ni "Komitet Gosudarstvennoi Bezopanosti of the Soviet Union" shirika hili lilianzishwa mwaka 1954 huko Moscow, shirika hili awali lilianzishwa kama kamati ya ulinzi ya Taifa la Usoviet na lilijumuishwa kwenye baraza la mawaziri, ila KGB walifanya kazi zao kwa uhuru na kwa kujitegemea kuliko taasisi yoyote ya serikali ya Taifa hilo la Usoviet.

KGB lilikuwa ni shirika kubwa zaidi la kipelelezi duniani na chombo cha ulinzi cha Taifa hilo, pia KGB ilijihusisha kwenye kila idara na kila kitu katika maisha ya wa watu ya kila siku katika Taifa hilo la muungano wa Usoviet, KGB ilikuwa ni siri na ni shirika ambalo lilijitenga zaidi, na inasemekana kuwa ilikuwa ni vigumu sana kufahamika kwa wananchi, hawakujua nini kinaendelea au kinafanywa na shirika hilo, pia KGB ilikuwa imegawanyika katika idara mbali mbali na kila idara ilikuwa inaongozwa na mwakilishi ambaye lengo kuu ni kusimamia kanuni za usalama wa Taifa hilo la usoviet, zaidi ya watu 500,000 wamefanya kazi ndani ya shirika la KGB na maelfu ya wapelelezi KGB walikuwa katika kila kona katika mataifa mbali mbali ulimwenguni kwa malengo ya kutimiza majukumu mbali mbali yenye manufaa kwa taifa
hilo.

Mwaka 1977 katiba ya Usoviet ilitamka kuwa baraza la mawaziri lita ratibu na kuongoza kazi za mawaziri pamoja na kamati za kitaifa ikiwemo KGB, Tarehe 5 mwezi wa saba mwaka 1978 mabadiliko mapya ya kisheria yalipitishwa ambapo yalibadili hadhi ya KGB, na kuwa Mwenyekiti wa Baraza la mawaziri wa Taifa hilo la kisoviet

Jukumu la msingi kabisa la KGB ilikuwa ni kukusanya taarifa za kijasusi kutoka mataifa mengine duniani, kulinda na kuzuia mataifa
mengine kuweza kupata taarifa za kijasusi kutoka katika taifa hilo la Kisoviet, kuhakikisha na kulinda usiri katika polisi, Askari wa KGB,
kuzuia migomo na maandamano katika Taifa hilo, kuhakikisha kuna usiri kwa walinzi wote wa boda za Taifa hilo, na walikuwa na jukumu la kukusanya taarifa za kijajusi (electronic espionage) kupitia kutegesha simu kwa ajili ya kupeleleza, kutumia tap recorder, keywatchers, n.k lakin pia KGB walisimamia maadili ya Kisoviet yanafuatwa na pia walisambaza itikadi za Kisovieti kwa propaganda.

Majasusi katika kitengo hiki walihakikisha wananchi wanapata taarifa ambazo zimeruhusiwa tu na serikali ndiyo ambazo wananchi wapata.

Kama ilivyokuwa kwa mashirika mengine ya kisoviet, KGB lilianza kuanguka baada tu ya aliyekuwa Raisi wa Taifa hilo Mikhail Gorbachev kuchukua Madaraka.

Sasa tutejee Moscow mwaka 1924.......................

Kwa bahati mbaya Mwaka 1924 Lenin alifariki dunia kwa ugonjwa wa kupooza (Stroke) na dola lilokuwa chachu na chimbuko la Usoshalist duniani likawa limempoteza Baba Wao na muasisi wa ujamaa. Na ndipo akaingia raisi anayeitwa Joseph Stalin ambaye alikuwa ni dikteta na kiongozi hodari katika historia ya ustawi wa USSR ambaye alivitumia vyombo hivyo kuua maadui wa ukominist wa Urusi na kuiba technolojia ya mataifa ya magharibi na kuiletea Urusi.

1939 dunia iliingia vitani tena ambapo Urusi ilionyesha umahiri mkubwa saana kijeshi baaada kumshinda Hitler alipoivamia Urusi hapa napo walifanya tena kama kwa Napoleon walikimbia kuelekea Red Square ili Wajerumani wadhani kwamba warusi hawana nguvu kumbe walikuwa wanasubiri winter ianze ili baridi iwasaidie.

Now sasa the second world war came to an end in 1945 ambapo the Super power Germany Empire iliyokuwa inapambana na Great Britain walikuwa wamechoka vibaya sana kiuchumi hivyo Marekani kama taifa ambalo lilokuwa limeimalika kiuchumi na kiviwanda likajikuta sasa Lina ushawishi mkubwa katika dunia na pia likaitajika kuukomboa Ubepari uliokuwa umedidimia.

Huku upande mwingine himaya ya USSR ikajikuta ndiyo taifa leyenye nguvu duniani (world Super-Supremacy empire). kumbuka mrusi na marekani ndiyo walikuwa wa kwanza kuingia berlin walianza kufanya sabotage na assassinations za Nazi leaders lakini kikubwa walichokifanya GRU ya Urusi ni kuwateka scientists wa nazi na kurudi nao urusi huku na marekani alikuwa akifanya vivyo hivyo.

Marekani aliiba project kubwa sana ya Ujerumani na kuipa jina la The Manhattan Project ambapo ilipomalizika we all know what happened to Hiroshima na Nagasaki.Mwaka 1945 raisi Franklin Delano Roosevelt alifariki dunia na kumwachia madaraka makamu wake mwendawazimu aliyeitwa Harry S Truman ndiye aliyeruhusu mabomu ya atomic code Name "FAT MAN na THE LITTLE BOY" kuangushwa pale japan.USSR under Joseph Stalin hawakukipenda kile kitendo provided that Japan aliisha surrender na viongozi wake kama General Hedaki Tojo na Sugiyama walikuwa wamejiua.

USSR alitumia mwanya wa vita ya pili kujitanua ambapo nchi kama poland, Georgia, Kazakhstan, Ukraine, East Germany na vijitaifa vya Eastern Europe vilimezwa kinguvu kitu ambacho kiliyaogopesha mataifa ya Magharibi kwamba nayo yatakuja mezwa siku moja.

USSR ilikuwa ndiyo nchi kubwa sana duniani kuliko zote ambapo kijeografia ilikuwa inastretch almost Eleven time zones(11%) Pia ilikuwa na nguvu kubwa kijeshi kuliko taifa lolote duniani na hii ni Kotokana na uwezo mkubwa wa technology ya kijeshi hasa katika siraha na vifaa.

Ilikuwa na kituo kikubwa cha kijeshi kilichoitwa "Kosovo" eneo Hili lilikuwa na ukubwa wa Karibu wa nchi ya Uingereza, hapa ndio lile Bomu lilopewa jina la "bomu la maangamizi" (Bombastic Bomb) nje na hiyo uchumi Wao ilikuwa mkubwa sana Karibu Mara mbili ya uchumi wa marekani nakuifanya USSR Kuhodhi 30.7% ya uchumi wa dunia nzima kwa kipindi hicho huku pato la taifa la USSR ilikuwa ni (8 trillion $ US) huku marekani uchumi wake ilikuwa $ 4.9trilion) .

Marekani kwa kuigopa Urusi alishauri mataifa ya Ulaya ili kujilinda yatengeneze umoja wa NATO (North Atlantic treaty organization) mwaka 1947, Na pia kwa kushauliana na Uingereza waliona kuna haja ya kuanzisha Dola mkakati (State defence platform) yani "formation of Israel nation in the middle East" mwaka 1948 kumbuka Israel ilitakiwa iwekwe hapa East Africa kwetu lakini walipima ni jinsi gani wataizuia the Soviet advance? (Russian advance).

Warusi walitumia mitandao yao kufinance vikundi vya kikomunisti ikiwa ni njia ya Kuhodhi dunia katika kupandikiza viongozi duniani (Implant of leaders as oversees States) kwa kuanzia na China wakati wa Mao Zedong 1949, Cuba nchini ya Fidel Castro 1950, Yugoslavia ya Slobadan Mcholovck, Vietnam ya Hoch Minh, Korea ya kaskazini ya Kim Jung Sun, pamoja na nchi kama Venezuela, Bolivia, Chile, Ghana, Libya, Angola, Mozambique, South Africa, India, DRC, na mataifa mengine Mengi.

Mfano kwa Uchina kuanzia mwaka 1948 hadi kupelekea mwaka 1949 urusi ilifanikiwa na kushinda na kuwaumiza Wamarekani kwa kiasi kikubwa saaaana kiuchumi.Mwaka 1949 Urusi aliishangaza dunia baada ya kurusha kombora la nuclear ambapo marekani alijua analo peke yake hivyo kupelekea mahusiano yao kudorora, na kupelekea kuzuka kwa zama za maangamizi yani "Almagadoni" kipindi hichi ndicho kukaw na wasiwasi wa kuzuka kwa vita ya tatu ya dunia. Kwani Mrusi ndiye aliyekuwa anaongoza kwa kuwa na sophisticated Rocket technology kuliko Marakani hivyo kufanya the red army yani jeshi la umma la Urusi kuogopwa saaana duniani hasa hawo wamarekani na washilika wake.

Mnamo miaka ya 1949 hadi mwaka 1950's nchin USSR kulikuwa na kitu kinaitwa The Molotov Plan ambao ulikuwa mpango wa ku counter The Marshall plan ya Marekani ambao ulikuwa unatoa mikopo kwa mataifa yaliyoumizwa kiuchumi na vita ya pili.Warusi walikuja kufanya maajabu tena baada ya kuanza mpango kabambe wa ugunduzi yani "extensive innovation project" ambapo Kalashnikov aligundua bunduki yenye nguvu saana aina ya AK47 au Avtomot Kalashnikov tena miaka ya 1957 Urusi pekee ndiye aliyekuwa wa kwanza kurusha Artificial Sattelite kwenye Orbit na tena pia Urusi ndiye aliyekuwa kwanza kupeleke MTU (cosmonaut)outer space nadhani alikuwa anaitwa "Yiri Gargarian" hii iliifanya USSR kuwa Ndimi Dola kuu katika ushawishi wa kisiasa, kiuchumi na kijeshi duniani.

Kama sijasahau Urusi alitumia mitandao ya upelelezi yani Intelligence Enhanced Technology (tekinolojia iliyoboleshwa katika ujasusi) kama NKVD na GRU ambapo walipeleleza serikali za marekani, Uingereza, na mataifa ya NATO ambapo walikuwa wakiwauwa viongozi wakubwa kwa sumu (poisoning na other tactics) mfano mzuri waliweza kuunda kitu kinachoitwa THE RING OF FIVE pale Yale UNIVERSITY ambacho kilikuwa kinaua wanafunzi ambao wanaonekana ni vipandikizi wa marekani yani "future potential American leaders" umoja huu uliundwa na wanafunzi ambao walikuwa wakijhami dhidi ya vipandikzi wa wamarekani.

Urusi ilikuja kuugopesha dunia ambapo mwaka 1961 walipeleka makombora ya Nuclear pale Cuba huku wakilenga miji mikubwa ya Marekani kama Chicago,Atlanta na New York huku raisi wa Urusi wakati huo alikuwa anaitwa Nikita Krushchev alikuwa anawatishia NATO kwamba "I WILL BURRY YOU" yani angewazika na kuwaangamiza" ,ilibaki kidogo ianze Nuclear War laikini wakubwa huwa wanaogopana yakamalizwa kwa diplomasia, lakini hata CIA wanakiri kwamba vita ingeanza wangeshindwa vibaya kwasababu walijiamini na kujua kwamba vita haiji kuingia jirani na USA, they were wrong coz this time the bad men was at their door step.Urusi alikuwa na military bombers ambazo zilikuwa na uwezo wa kufanya mashambulizi makubwa saaana USA ukiangalia ujirani kati ya Cuba na USA.

Mrusi alikuja kushikwa pabaya na USA kwenye the Six Days War ambapo mmoja wa mjasusi wake alikimbia Urusi kama alivyofanya Snowden na kuelekea Uingereza ambapo alitoa secret files za majina ya secret ghost agents wa Urusi ambao walikuwa wanaoperate middle east hivyo kupelekea wauawe wanajeshi wengi wauwawe na Israel kushinda vita, kushindwa huku kulipelekea Urusi chini ya rais mpya bwana Leonid Brezhnev kutengeneza the lethal weapon ambayo itaweza ku undermine all world intelligence agencies na kuirudisha Urusi katika hali yake,waliunda kitu kinachoitwa KGB.

Trust me people even the Mossad feared the KGB,it was notoriuos,efficient killing machine,efficient tool for collecting information,tromendous tool in drafting national policies,masters of infiltration and good suppressors of internal dissidents.KGB itakumbukwa kwa kuifanya Urusi iwe the most feard country in the world hasa chini ya boss wake aliyeitwa Yuri Andropov ambaye alikuja kuwa rais wa Urusi baadae.

KGB ilianza kupenyeza majasusi wake hadi kwenye jeshi la Marekani ambapo waliweza kumrecruit US NAVY chief Anthony Walker ambaye alifanya kazi kwa miaka 18 na KGB.

Urusi na China walihusika saaana kuwaua Wamarekani kwenye Vietnam war,Urusi ndiyo waliilinda India mwaka 1971 ili USA wasiivamie na kweli USA alishindwa kuvamia India.

Ikumbukwe Mrusi anakuwa na Nguvu saaana kwasababu huwa habetray allies wake kama USA, USSR yeye anawalinda NORTH KOREA,VIETNAM,SYRIA,IRAN na mataifa mengine washirika wake wakubwa.

Urusi kailinda sana Syria kwasababu kwanza ni nchi ambayo inavitega uchumi vikubwa sana vya Urusi kuna makampuni ya mafuta kama Tatneft pia kampuni la mafuta la Syria linanua vifaa kama pipes kutoka Russia pia Syrian Air and Marine companies vessels zake nyingi ni za Mrusi na pia mbali na south Asia soko kubwa la silaha liko Syria sasa. Urusi hawezi ruhusu mataifa ya magharibi kuvamia kwasababu amewekeza saana Syria kwenye manufacturing industry profits.

Anguko la Urusi...........

Anguko la Urusi lilianza kushika kasi chini ya utawala wa Mikhaili Gorbachev kufatia makubaliano yaliyoitwa Start Treaty, aliyoingia na Marekani.

Kufatia mkataba huo Gorbachev aliaamua kuruhusu mfumo wa kidemokrasia wa vyama vingi na hili lilikuwa wazo la kiufundi toka kwa Bush kwa lengo la kudhoofisha Ukomunist.

Uchaguz uliofuatia mwaka 1990 Gorbachev alijikuta akiwa katika mshawasha au njia panda kutokana na msigano toka siasa za ndani. Boris Yeltsin na watu wengi wengine walikuwa wakitaka uelekeo mpya wa kidemokrasia na mabadiliko ya haraka ya kiuchumi wakati wakomunist kindakindaki wakitaka kutupilia mbali muswada huo wa Gorb.

Wakiwa katika mkanganyiko wa waungane na nani katika ya Gorb na Yeltsin utawala wa Bush ukaamua kufanya kazi na Gorbachev kwa sababu waliona kuwa huyu alikuwa reliable. Mwenye kuaminika ukilinganisha na Yeltsin. Waliangalia maamuzi mengi ambayo aliyafanya nyuma yalikuwa pia ni ya manufaa kwao.

Ukafanyika mpango wa kutia saini makubaliano yaliyoitwa START ambapo moja ya makubaliano hayo yalikuwa ni kuondoa majeshi ya Red Army toka Ujerumani mashariki ambayo yalikuwa yakiikalia Ujerumani. Kwa kuondoa majeshi hayo huko inamaana Gorbachev aliamua kuachia kuungana kwa Ujerumani hizo mbili. Tukumbuke zilijitenga na kuwa na Ujerumani Mashariki na Ujerumani Magharib. Na wakati ule Saddam ameivamia Kuwait USA na Viongozi wa kisoviet walishirikiana pamoja kumkemea na kumwondoa.

Lakini ndani ya Usoviet bado changamoto ziliendelea kuwepo ambapo Moscow wakawa wanamshinikiza Gorb abakize nguvu za chama ili kiweze ku control utawala wa kikomunist ulaya ya mashariki.Baada ya kuanguka kwa Ukomunist Ujerumani Mashariki, Majimbo ya Baltic na Caucas wakaanza nao kudai Uhuru kutoka Moscow. January , mwaka 1991 machafuko yakatokea Lithunia na Latvia. Usoviet ikapeleka vifaru kuingilia na kukomesha harakati zao za kujitafutia Uhuru. Jambo ambalo Bush alililaani sana.

Mwaka huo 1991 Utawala wa Bush ukakaa chini tena kuangalia namna gani Utashughulika na utawala wa Kisoviet. Kukawa na mawazo matatu .

i. Utawala uendelee kumuunga mkono Gorbachev kwa kumpa matumaini kuwa itasaidia kuzui kuvunjika kwa muungano wa kisoviet.

ii. Pia wakati huo huo USA ikimsaidia Yeltsin na viongozi wa Jamhuri mbalimbali ili kuwafanya watimize malengo yao ya kutaka muundo mpya au kujitoa katika Muungano huo. Hivyo waliweza kucheza na pande zote mbili kwa umakini sana.

iii. Na wazo la mwisho lilikuwa ni kumsaidia Gorbachev kwa masharti ambayo yangeweza kuendelea kumletea shida kutoka kwa wapinzani wake na wao kutaka mabadiliko ya kiuchumi.

Mapinduzi ambayo hayakufanikiwa August 1991 dhidi ya Gorbachev yalipigilia msumali kuanguka kwa Muungano wa Soviet. Haya yalikuwa yamepangwa na wakomunist kindakindaki ambapo waliishia kupunguza nguvu ya Gorbachev na hivyo yakamsaidia zaidi Yeltsin na harakati zake za kidemokrasia. Bush alilaumu jaribio hilo la Mapinduzi ila ikawa wazi kuwa Gorbachev sasa alikuwa dhaifu.

Na hapo akaamua ku jiuzulu nafasi yake ya Uongozi wa chama cha kikomunist.na badaye muda mfupi chama kikatenganishwa na Urais katika Muungano wa Kisoviet.Siku chache baada ya jaribio hilo la Mapinduzi Ukraine na Belarus wakatangaza Kuwa Huru kutoka Muungano wa Kisoviet. Majimbo ya Baltic ambayo hapo mwanzo yalijitangazia uhuru yakawa yanataka sasa kutambulika kimataifa.

Kutokana na mabadiliko haya ya ghafla utawala wa Bush ukaanza kuangalia kwa ukaribu kusije kuokea balaa la matumizi ya silaha za kinyuklia kutokana na machafuko yaliyoanza kutokea maeneo hayo. Hivyo September 4 mwaka 1991 aliyekuwa katibu wa Secretary of State wa USA bwana James Baker alipendekeza kuwe na kanuni 5 muhimu ambazo zitawaongoza USA katika sera zake za siasa za nje kuhusiana na hizi Jamhuri mpya.

i. Kuwe na utawala wa kidemokrasia

ii. Kutambua mipaka iliyokuwepo (wasivamie nchi jirani kwa nia ya kujipanua)

iii. Kuunga mkono tawala za kidemokrasia

iv. Kulinda haki za binadamu

v. Kuheshimu sharia za kimataifa

Na kuwa kama Jamhuri hizi mpya au nchi hiz mpya zingefuata taratibu hizo basi USA ingewaunga mkono. Baker akakutana na Gorbachev na Yeltsin katika kusudio la kuwasaidia katika mikakati yao ya kiuchumi na kuandaa fomula ambayo itawasaidia kiuchumi Russia nan chi hizo ambazo zimemeguka.

Wakati huo huo kuruhusu mabadiliko ya kisiasa kwa njia ya Amani kabisa. Mwanzoni mwa December Yeltsin na Viongoz wa Ukraine na Belarus walikutana Brest kuunda Ushirikiano wa Nchi huru (CIS) na hapo kuangusha kabisa Muungano wa Kisoviet.

December 25 mwaka 1991 ile bendera ya Nyundo na Nyengo (Sickle) ikashushwa na kubadilishiwa na Bendera ya Russia yenye Rangi Tatu. Mapema siku hiyo Gorbachev alijiuzulu nafasi yake kama rais wa Muungano wa Kisoviet na kumuachia Boris Yeltsin kuwa Rais mpya wa Russia/Urusi mpya na huru. Na watu dunia nzima walingalia kwa mshangao namna hii ya kubadilishana madaraka kwa njia ya Amani kutoka kwenye iliyokuwa jamhuri ya kikomunist katika muungano wa kisoviet na kuwa Taifa lenye mitizamo mbalimbali tofaut tofaut.

Kwa kuangusha Soviet Union utawala wa Bush ukawa kuifanya Russia iwe imara kiuchumi na kuleta Amani Urusi,Baltics na Majimbo mengine ya iliyokuwa Muungano wa Kisoviet, Bush akatambua Uhuru wa jamhuri nyingine 12 na kuanzisha mahusiano ya kidiplomasia na Urusi,Ukraine,Belarus,Kazakhstan,Armenia na Kyrgyzstan. Na February mwaka 1992 Baker alitembelea Jamhuri zilizokuwa zimebakia na kuanzisha ushirikiano nazo wa kidiplomasia zikiwemo Uzbekistan, Moldova, Azerbaijan, Turkmenistan na Tajikistan.

Vita vya wao kwa wao vilivyotokea Georgia vilizuia isitambulike na kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia na USA mpaka May 1992. Yeltsin alikutana na Bush huko Camp David February 1992 na baadaye kumtembelea ikulu rasmi Washington June. Viongoz wa Kazakhstan na Ukraine wakamtembelea Ikulu pia May 1992.

Kifupi huku ndo kulikuwa kuanguka kwa Soviet Union na hitimisho lake mwaka 1991.

Kuporomoka kwa USSR na kuibuka Putin..............

Jina la Vladimir Putin ni maarufu sana miongoni mwa viongozi wa dunia kama lilivyo la Donald Trump, Rais huyu wa taifa kubwa la Urusi aliyekuwa afisa wa Shirika la ujasusi KGB kwa miaka 16 akiwa na cheo cha Luteni Kanali alianza kugonga vichwa vya habari alipojimwaga kwenye ulingo wa kisiasa Saint Petersburg 1991 alipojiuzulu kazi hiyo ya ukachero.

Saint Petersburg, ulirudishiwa jina lake hilo la zamani uliposambaratika Muungano wa Jamhuri za Kisovieti 1991, lilipofutwa baada mapinduzi ya 1917 na kuitwa Leningrad, kumuenzi muasisi wa mapinduzi hayo, wajina wake Vladimir Lenin.

Agosti 1999 kwa mshangao wa wengi, Putin aliteuliwa na rais Boris Yeltsin kuwa Waziri mkuu na kusema ndiye anayemtaka awe mrithi wake.

Katika tukio lisilotarajiwa mkesha wa mwaka mpya Desemba 1999 Yelstin akalitangazia taifa anajiuzulu na kwa mujibu wa katiba Putin akawa kaimu Rais na kuanza kujiimarisha akijitokeza kugombea uchaguzi uliofanyika miezi mitatu baada ya Yeltsin kujiuzulu.

Sababu za mwanasiasa huyo mkongwe Yeltsin kuamua kuacha madaraka ilikuwa ni pamoja na hali yake ya afya iliochangiwa na unywaji pombe kupita kiasi. Alishindwa kuongoza na kuonekana dhaifu katika utoaji maamuzi, huku akikosolewa vikali kwa upendeleo. Rushwa ilikithiri na jamii kuanza kujiuuliza kama hayo ndiyo matunda ya Demokrasia ambayo Yeltsin aliyemuangusha madarakani Michail Gorbachev akiinadi .

Warusi wengi na hasa wafuasi wa chama tawala cha zamani cha Kikoministi wanashutumu Gorbachov kuwa chanzo cha kusambaratika dola lao kubwa, Muungano wa Jamhuri za Kisovieti na vile vile ndiye sababu ya kuzuka hatari ya kuporomoka kwa nguvu ya Urusi katika kukabiliana na Marekani, kuweka wizani wa kisiasa na kijeshi duniani.

Udhaifu wa Yeltsin ambaye alionekana dhahiri kutokuwa na dira, uliifungulia mlango Marekani kuwa dola pekee lenye usemi na lililofanikiwa katika kupambana na ukoministi. Yote hayo yalijiri baada ya Gorbachov kuanza kutekeleza sera yake ya Perestroika na Glasnost ( Mageuzi na Uwazi). Wakosoaji wake wanaamini alifungua milango wazi ya Uhuru, ambao haukuwa na mipaka na hatimaye akashindwa kuudhibiti.

Kwa upande wake Yelstin aliyetambua madaraka ni mazito na yamemshinda akatafuta muokozi na ndipo alipomuona Putin .

Mara tu baada ya Putin kushika hatamu za kuliongoza taifa hilo kubwa aliposhinda uchaguzi mwaka 2000, akaanza kujenga nguzo za Urusi iliokuwa ikiporomoka na zaidi katika sekta yakiuchumi na kijeshi. Lengo lake lilikuwa kurudisha hadhi ya Urusi kama taifa lenye nguvu. Ni dhahiri hatari ya hali hiyo akiiona kutokana na maarifa yake kama afisa wa ngazi ya juu wa zamani wa Shirika la ujasusi KGB. Alifahamu enzi za chama cha kikoministi ilikuwa imeanza kuzikwa, lakini aliutumia mfumo ule ule wa kuongoza na kudhibiti, akiibuka kuwa kiongozi mwenye ujasiri.

Ninaporudi nyuma na kuidurusu historia ya kisiasa ya Urusi baada ya vita vya pili vya dunia, nina mfananisha na Leonid Brezhnev aliyechukua nafasi ya Nikita Krushchev kama Katibu mkuu wa Chama na Kiongozi mkuu 1964 na kutawala miaka 18. Brezhnev ni mmoja wa viongozi wakuu shupavu wa uliokuwa Muungano wa Jamhuri za Kisovieti (Urusi ya zamani).

Alhamisi iliopita Machi 26, Putin alitimiza miaka 20, mihula miwili kamili tokea aakabidhiwe hatamu za kuiongoza Urusi. Warusi wanaamini kwa namna moja au nyengine ameliokoa taifa lao na wafuasi wake hawakubaliani na hoja kwamba utawala wake ni sawa na uimla. Wanaamini chini ya utawala wa Yeltsin nchi yao ikielekea katika janga kubwa la kisiasa na kiuchumi.

Mahasimu wake wakiwemo wakoministi walimkosoa na kushangazwa kuwa alijitenga na falsafa iliomlea ya ukoministi na kufuata sera ya soko huru. Wadadisi wengine lakini, walimsifu kwa kuuona na kuutambua ukweli wa mambo. Putin akaanza kuchukua hatua za mabadiliko, kujenga uchumi na kurejesha hadhi ya taifa hilo.

Kufanikisha malengo yake, katika jukwaa la Kimataifa alirejesha uhusiano mwema na China, ambao uliharibika kwa miaka mingi , wakati ndugu hao wawili katika ukoministi walipofarakana 1962 kutokana na tafauti za kifalsafa. Urusi iliiunga mkono China na kuisaidia, baada ya wakoministi kushinda vita vya wenyewe kwa wenyewe na kuunda Jamhuri ya Umma wa China 1949.
Putin aliuita uhusiano mpya na China kuwa ni “ushirika” na maka jana alikuwa miongoni mwa viongozi waalikwa katika sherehe ya miaka 70 ya kuundwa kwa Jamhuri hiyo.

Akijua ana mshirika wa uhakika kijiografia , mwenye nguvu na ushawishi katika siasa za kimataifa, Putin akaanza kukabiliana na Jumuiya ya kujihami ya NATO yenye wanachama 29 na inayoongozwa na Marekani. Mvutano wa pande hizo mbili ukatuwama zaidi kutokana na hatua ya Urusi kulitwaa eneo la Crimea la Ukraine , kuingia vitani na Jamhuri hiyo ya zamani ya Kisovieti na kulitia msukosuko eneo lake la mashariki kukiibuka hisia za kutaka kujitenga na Ukraine. Pia suala la Syria likawa eneo jengine la kupimana nguvu. Putin akajiunga na Iran kuunga mkono utawala wa Rais Bashar al-Assad .

Tangu matukio ya kuangushwa kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi 2011, Urusi imekuwa ikijiweka upande wa pili unaokinzana na Marekani katika migogoro yote, Hali hii inafuatia kutoaminiana kulikozuka na NATO baada ya azimio la Umoja wa Mataifa kuzuwia ndege Gaddafi kuwashambulia raia wanaompinga katika mji wa Benghazi kuliko anzia uasi dhidi yake. Urusi ilioliunga mkono azimio hilo inaamini lilikiukwa na Marekani, Uingereza na Ufaransa, wanachama wenzake katika Baraza la Usalama na zikalitafsiri vyengine na kumshambulia Gaddafi kwa kuwaunga mkono waasi, hadi alipoangushwa na kuuwawa.

Katika vita vya kuwania madaraka vinavyoendelea nchini Libya, Urusi inamuunga mkono Jemedari Khalifa Haftar dhidi ya serikali inayotambuliwa kimataifa mjini Tripoli ya waziri mkuu Fayez al-Saraj, kukiwa na taarifa za kuwepo kwa askari wa kukodiwa kutoka Urusi wanaomsaidia Haftar.

Lakini pembezoni Putin amekuwa akiuma na kupuliza ili yatakapogeuka aendelea kuwa na ushawishi hasa panapohusika na masilahi ya kiuchumi ambayo ni utajiri mkubwa wa mafuta nchini Libya. Hilo lilidhihirika alipoitisha mkutano wa upatanishi mjini Moscow Januari mwaka huu kwa akishirikiana na Rais Recep Tayep Erdogan wa Uturuki na kuwaalika Haftar na Saraj kujaribu kuleta suluhisho la mgogoro huo.

Mkutano huo lakini haukua na mafanikio na wala mahasimu hao wawili nchini Libya hawakukutana ana kwa ana .

Putin ana usuhuba wa kimkakati na Rais Recep Tayep Erdogan wa Uturuki licha ya kuwa ni mwanachama wa NATO na pamoja na kwamba wanatafautiana juu ya kuendelea kuweko madarakani Bashar al-Assad nchini Syria.

Uhusiano wao hata hivyo hauifurahishi Marekani hata kidogo huku kuelewana kwa Rais wake Donald Trump na mwenzake wa Urusi kukiwa sawa na maji kujaa na maji kukupwa. Hupongezekana na kushutumiana ikitegemea kila mmoja anafaidika vipi na hali na hali iliojitokeza tukio husika.

Ili kutanua ushawishi wake katika mashariki ya kati Putin ana mahusiano mazuri na Iran na Saudi Arabia mataifa mawili yenye utajiri mkubwa wa mafuta na ushawishi wa kisiasa katika eneo la ghuba na mashariki ya kati kwa jumla. Wakati akiwa ametimiza mihula miwili ya kuliongoza taifa hilo kubwa la Urusi, inaelekea bado Putin hana mpango wowote wa kun´gatuka mapema.

Mbinu zake zilianza 2008 alipomaliza mhula wake wa pili kama Rais na kuzuilika kikatiba kugombea kipindi cha tatu . Alibadilishana wadhifa na Waziri mkuu Dmirty Medvedev aliyechukua kiti cha Urais na Putin kuwa Waziri mkuu hadi 2012, wakati Putin aliporudi tena.

Mwezi Januari mwaka huu Medvedev alijiuzulu pamoja na baraza zima la mawaziri na Putin kumteuwa Waziri mkuu mpya. Lakini hakumtupa sahibu yake wa chanda na pete aliyekuwa awali kabisa meneja wa kampeni yake ya uchaguzi , bali alimteuwa Medvedev kuwa Makamu mwenyekiti wa baraza la usalama la taifa.

Ukiwa muendelezo wa mbinu za kubakia madarakani, Putin amependekeza mabadiliko ya katiba ambayo yalikuwa yapigiwe kura ya maoni na umma mwezi ujao, lakini imeahirishwa kwasababu ya janga la Corona. Mabadiliko hayo yanamfungulia nafasi ya kubakia madarakani hadi 2036 baada ya muhula wake kumalizika 2024.

Putin ana umri wa miaka 67 na wakati huo atakuwa na miaka 83, kisiasa hakuna anayeweza kutabiri matukio, lakini kwa sasa bado Urusi ni Putin na Putin ndiyo Urusi .

Urusi chini ya Putin.......................

Pamoja na kuporomoka kwa USSR bado Putin Unaendelea kuifanya Urusi iendelee kujisimika katika ukuu wa Hegemony, bado Putin anahamu ya kufanya Urusi awe kiranja wa dunia kiuchumi, kisiasa na kijeshi.

Urusi chini ya Putin inarejea upya kupitia Shirikisho la Urusi baada ya anguko la dola ya Umoja wa Nchi za Kisovieti (USSR) mwanzoni mwa miaka ya 1990, Nayo ina maumivu yake kwa sababu Marekani ndiyo iliyoiandama Sovieti na kuchochea nchi za USSR kujitenga na umoja huo.

Marekani na Urusi ni nchi zenye kisasi. Urusi inaamini kuwa kama USSR isingeanguka, maana yake ubabe wa Marekani leo usingekuwepo. Marekani haitaki Urusi irejee nguvu zake za Sovieti.

Pamoja na hayo kiuchumi, Urusi inaachwa nyuma na sasa ushindani unaonekana kati ya China na Marekani, Kijeshi mataifa yote hayo yapo imara na kwenye siasa tayari Urusi imeshaonekana tishio kwamba kumbe inaweza mpaka kuiingilia Marekani.

Kwa sasa Urusi ina mashirika ya upelelezi mengi ambayo kwa asilimia 90 hufanya kazi ya ushushushu duniani, Urusi ina mashirika ya upelelezi 15.

Katika medani ya kijeshi Urusi ya Putin ina wanajeshi 771,000 askali wa akiba ni 1.9 milioni, Bajeti ya Jeshi la Urusi kwa mwaka 2020 ilikuwa dola 93.9 bilioni, sawa na Sh210 trilioni.

Urusi ndio nchi inayoongoza duniani kwa kumiliki Nyuklia inamiliki silaha za nyuklia ambazo ilizirithi kutoka USSR, Mkoba wa nyuklia wa Urusi unaitwa Cheget ambao Rais wa Urusi muda wote yupo nao pembeni, Kama akitaka kulipua nchi yoyote ni suala la kufungua mkoba na kuchagua sehemu ya kuelekeza shambulio, Watu wengine wenye dhima ya kutunza Cheget ni waziri wa ulinzi na mnadhimu wa jeshi.

Pia Urusi wana aina moja tu ya Stealth Fighters ambayo ni F-22. Aina nyingine ambayo itakuwa ya pili kwa Urusi ni T-50 ambayo bado hazijazinduliwa.

Kwenye ujasusi Urusi ina Jumuiya ya Ujasusi ya Urusi inayo undwa na vyombo 15. 1. Huduma ya Ujasusi wa Kimataifa (SVR), wao huripoti kwa Rais. 2. Kurugenzi ya Ujasusi ya Jeshi la Urusi (GRU). 3. Kurugenzi Kuu ya 12 (12th Chief Directorate) hii inafanya kazi chini ya Wizara ya Ulinzi na inashughulika na usalama wa nyuklia.

Namba 4. Shirikisho la Usalama (FSB), inahusika na usalama wa nchi pamoja na mapambano dhidi ya ugaidi. 5. Shirikisho la Udhibiti wa Teknolojia (FSTEK) ambayo jukumu lake ni kuchunga mawasiliano na kudhibiti wizi wa kiteknolojia. 6. Shirikisho la Ulinzi (FSO), jukumu lao ni kutoa walinzi binafsi kwa viongozi.

Namba 7. Shirikisho la Ulinzi wa Rais (SBP), wao kumlinda Rais tu. 8. Kurugenzi Maalum ya Mawasiliano (SSSR), kulinda mawasiliano ya Serikali. 9. Kurugenzi Kuu Maalum (GUSP), jukumu lake kulinda hazina za Serikali. 10. Shirikisho la Forodha (FTS), kupambana uharamia wote wa forodha.

Namba 11. Shirikisho la Mihadarati (FSKN), jukumu lake ni kupambana na dawa za kulevya. 12. Shirikisho la Kudhibiti Pombe (FSKA), kupamabana na pombe bandia. 13. Shirikisho la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi (MVD), kushughulikia utekelezwaji wa sheria.

14. Shirikisho la Polisi (Politsiya) yenyewe ni upelelezi wa mambo yote ya kipolisi. 15. Shirikisho la Udhibiti wa Fedha (Rosfinmonitoring) ambalo hupambana na utakatishwaji wa fedha haramu pamoja na ugaidi.

Ndimi: Comred Mbwana Allyamtu
Copyrights of this article reserved
written by Comred Mbwana Allyamtu.
Email-mbwanaallyamtu990@gmail.com

Copyright 2020, All Rights Reserved.

Maktaba KuuView attachment 1876373View attachment 1876376View attachment 1876374View attachment 1876377View attachment 1876375View attachment 1876379View attachment 1876378View attachment 1876380
FB_IMG_1627819774029.jpg
FB_IMG_1627819768943.jpg
FB_IMG_1627819774029.jpg
FB_IMG_1627819777840.jpg
FB_IMG_1627819782219.jpg
FB_IMG_1627819789583.jpg
FB_IMG_1627819793266.jpg
FB_IMG_1627819796364.jpg
FB_IMG_1627819799354.jpg
FB_IMG_1627819807037.jpg
FB_IMG_1627819807037.jpg
FB_IMG_1627819815225.jpg
FB_IMG_1627819821480.jpg
FB_IMG_1627819827024.jpg
FB_IMG_1627819832193.jpg
FB_IMG_1627819841328.jpg
FB_IMG_1627819845675.jpg
FB_IMG_1627819854346.jpg
FB_IMG_1627819858313.jpg
FB_IMG_1627819863158.jpg
FB_IMG_1627819877082.jpg
FB_IMG_1627819885475.jpg
FB_IMG_1627819889918.jpg
FB_IMG_1627819898246.jpg
FB_IMG_1627820101948.jpg
FB_IMG_1627820091837.jpg
FB_IMG_1627820116850.jpg
 
Sijaelewa kwanini ukubwa wa nchi unapimwa na Nguvu ya Jeshi umetumia Nguvu nyingi kuiongelea USSR ktk eneo la kivita zaidi .

Sijaelewa mpaka leo kwanini nchi zenye uchumi mkubwa zimewekeza zaidi kwenye silaha za kivita
 
Sijaelewa kwanini ukubwa wa nchi unapimwa na Nguvu ya Jeshi umetumia Nguvu nyingi kuiongelea USSR ktk eneo la kivita zaidi .

Sijaelewa mpaka leo kwanini nchi zenye uchumi mkubwa zimewekeza zaidi kwenye silaha za kivita

Zinapimwa kwa nguvu ya jeshi kwa sababu jeshi ndo kila kitu kwa dunia ya Sasa ukiwa na jeshi dhaifu ni rahisi watu kukuingilia na kupeleleza

wanajilinda ndo maana wanawekeza zaidi kwenye silaha kali za kivita na pia hili kuogopwa
 
Zinapimwa kwa nguvu ya jeshi kwa sababu jeshi ndo kila kitu kwa dunia ya Sasa ukiwa na jeshi dhaifu ni rahisi watu kukuingilia na kupeleleza

wanajilinda ndo maana wanawekeza zaidi kwenye silaha kali za kivita na pia hili kuogopwa
Nashangaa hata sisi Tz siku ya Uhuru tunatumia Nguvu nyingi kuonesha silaha za kivita kuliko kuelezea maendeleo yetu kiuchumi
 
Back
Top Bottom