Miti shamba/mizizi ina nguvu katika mapenzi?

Mizizi aina ya dawa na si kila mzizi ni dawa ipo special inategemea unataka umwite mpenzi wako wa zamani au unataka umkamate mpenzi wako asikohoe au unataka mpenzi wako asiende kwa nyumba ndogo sasa kuna dawa za kienyeji aina ya mizizi au miti shamba.

Ni kweli hizo dawa zinafanya kazi au ni Imani tu,maana navyoelewa mimi chochote unachotumia ukiamini kuwa kitakusaidia inakua kama dawa,kwa mfano nikiamini kwa % nyingi kuwa nikitaka kumpata Fidel80 kwa kutumia mbinu fulani ni kweli naweza kumpata,Je sasa na hiyo tunaweza kusema ni dawa(Mizizi)
 
Hizo dawa kwa % naamini zinafanya kazi.
Mi naweza nikatumia mbinu ya kimiti shamba nikakupata na ukanipenda mpaka balaa ukasahau mzee hahahahaha nakwambia sio imani wala nini ila kimzizi kiulaiiiiiini unanipenda lakini wewe unakuwa hujui mimi nakuwa na mvuto kwako nakuvuta na unavutika.
 
Fidel hiyo yako kali uwiii, kuziba/kuzibuliwa! kweli kuwa uyaone.

nakwambia amini usiamini jamaa alikuwa na wivu na huyu mtoto akaamua kuziba kabisa asitoke nje nilisahau ilibidi nimwambie njoo nitest kama na mm nitashindwa kuzibua.
 
Kuna uvumi mwingi sana wakutumia mizizi katika mapenzi? Wapo wengine wana imani kuwa akitumia mizizi anaweza akampata kwa mfano hata mke wa mtu au mpenzi wa mtu kama Nyamayao au Belinda au Mwanajamii......je ni kweli hizi dawa zinafanya kazi na zinauwezo wakukushawishi ukubaliane na matakwa ya huyu mtu katika mapenzi na ukampenda gafla?

Mh kaka hii nasikia sana kuwa ipo na kuwa watu hasa wanawake hutumia miziziology kumpumbaza bwana wa mwenzie wanajua wanavyofanya but ninachoelewa ni kuwa hawa wawili lazima wawe na ukaribu wa aina flani kwani dawa hizi ni lazima mlengwa awekewe kwenye kilaji au kinywaji au zipo za kupuliza impate? Mbaba ukikaribishwa glasi ya maji klwa sauti nyororo ah wanywa kumbe kuna punje umekwisha.

Ila nasikia kuna wale waganga wanaokuitia mtu wako kwenye sufuria wamwona nawe wanuiza (nimeona kwenye picha za kinigeria) sijui kama in real life zipo.

Nakumbuka sie wakati twasoma tulikuwa tunaambiwa ukisalimiwa na mwanaume njiani ukiitika tu basi wageuza njia wamfuata aendapo yaani unampenda kufa kiasi kwamba ukijachukuliwa unakuwa mkali na shule unaacha. Asa sijui tulikuwa tunatishwa tu ili tusiharibikiwe mapema?

Lipo tena jambo jingine wapo watu wanawake na wanaume wanao wapumbaza waume au wake zao anakuwa haongei kitu mtu mmoja katika familia anakuwa na kibezi anasauti na ndo mwenye maamuzi inasemekana iwa wanalishwa limbwata kwa hiyo mwanaume au mwanamke anakuwa amenywea mpaka watu walio nje na ile familia wanaona kama yule mama au baba kama anaonewa kama ni mwanaume kafanyiwa mzizi mwanamke anaweza akawa anarudi muda anaotaka usiku na kumwachia majukumu yote ya pale nyumbani na mwanaume haongei kitu .

Ndugu zangu hii mizizi ina nafasi katika mapenzi?
Je mizizi au mitishamba ina nafasi kubwa katika ulingo wa mapenzi?
Karibuni nyote tuchangie.

Fidel80

Hayo yote yanasikika mitaani inawezekana ni ya kweli but pia inawezekana ni hulka ya mtu tu mama kaolewa kaamua kupanda juu ya kichwa cha mumewe na bahati mbaya mumewe mpole in nature sasa anakuwa hana jinsi. Binafsi siamini katika miziziology kwani kinachonijia akilini ni kwa nini nipendwe kwa nguvu za dawa je hili ni pendo la dhati? Sio so why tourturing yourself kwenda kurenew kila mara? Kwa nini umpende mtu unayejua fika hakupendi (eh kwani bila hizo dawa angekupenda?)

Mh nisiseme sana pengine ni kwa vile hayajanikuta!
 
Ushirikina ni mtandao wa uwongo kuwadanganya watu kuwa kuna vitu vinatokea kwa sababu ya nguvu fulani fulani. Huu nao ni ushirikina na mambo haya hujitokeza sana kwa jamii fukara na maskini.

Mapenzi ya mitishamba ni ushirikina na hayana ukweli wowote. Ila kama ilivyo kawaida ya ushirikina ukweli kidogo huongezewa chumvi kibao ili kuufanya uonekane ni ukweli halisi.

Kuna mtandao wa kueneza imani kama hizi na washirikina hasa hao wanaojiita waganga wa kienyeji wanayo mitandao yao ya siri ya kuwalisha watu uongo ili waamini. Hii ni mojawapo ya uongo unaoaminika sana. Mwingine ni katika mpira n. k. na yote hii ni kazi ya mitandao ya kishirikina. Wanufaikaji wa mambo kama haya ni hao waganga na makuwadi wao.

Ukiamini huo ushirikina utaenda kwa waganga. Ukienda huko utakuta mbwembwe nyiingi. Wengine huwaingizi wadada dawa kwenye uke wao kwa kutumia viungo vyao vya kiume, ndo masharti ya dawa, na anayeamini huridhia.

Na hayo matokeo yanayosemwa ni uwongo tuu, na mara nyingi aliyerubuniwa akaiva ataona kama mabadiriko yametokea hata kama hakuna lolote la maana. Hiyo kusema eti mwanaume alikuwa anashindwa kuingia wakati eti kwa sababu kafanyiwa dawa na mpenzi wake wa zamani ni uongo vile vile. Nimeshasikia stori nyingi za hivyo, lakini zote huwa hazina proof yoyote. Jambo hilo lingekuwa linawezekana tusingekuwa tunaona frustrations tunazoona kwenye mahusiano, hasa hasa huko uswahilini yanapoendekezwa mambo hayo.

Ni uwongo na uzushi tu. Dawa wanazouza wamasai ni mizizi tuu ya kuongeza nguvu za kiume kama ilivyo VIAGRA. Na hizo zipo na uwezo wao wa kufanya kazi umethibitishwa.

Mengine ni uwongo tuuu wa kuongezea chumvi ili wateja wengi waje!!
 
Mwana mi naamini kwa kiasi kikubwa miti shamba ina nguvu sana katika mapenzi nakwambia mi naweza nikamlisha kitu mchumba angu nikawa nakuja na nyumba ndogo na asiulize kitu chochote.
 
Ni uongo mtupu kuwa unaweza kwenda na nyumba ndogo halafu huyo uliyenaye akaridhika kwa sababu umefanya dawa!!! No huu ni uongo tuuu.
 
Fidel anazuga tu hapa ili apate michango mingi zaidi kuthibitisha dhana yake!Hajui cha dawa wala nini huyu!
 
Ni uongo mtupu kuwa unaweza kwenda na nyumba ndogo halafu huyo uliyenaye akaridhika kwa sababu umefanya dawa!!! No huu ni uongo tuuu.

We amini ni uongo lakini nahisi hujakaa uswazi wewe hivi vitu common sana bana.Kuna mzee ana mke wake kampiga kizizi kaleta nyumba ndogo pale pale na wanaiva kama balaaa kama mtu na mdogo wake kumbe mke mwenza.
Muulize WOS au Mwana kama wapo tayari kupokea wake wenza waishi wote nyumba mmoja.
 
Thubutu!!
Huyo nyumba ndogo wako hakuna rangi ataacha kuona!
 
Dawa zilizomo kwenye miti shamba ndo hizo hizo, aspirini, clorokwini, n.k. Lakini hakuna dawa zinazoweza kukufanya umpende mtu na kubaliana na mambo machafu wakati unaona ni machafu. Watu huwa wanakubaliana na manyanyaso si kwa sababu wamelogwa bali hali halisi inawafanya wakubali yaishe. Usisahau madhara ya mfumo dume na dini zetu. Wanawake wengi uswahilini huona kuwa ni sawa mwanaume kuwa na mke zaidi ya mmoja na wengine hudhani ni haki yake. Sasa ukileta nyumba ndogo akaelewana nayo si kwa sababu umelishwa mzizi. Inawezekana anadanganywa kuwa hiyo ni kazi ya mzizi. Lakini ukweli si hivyo.
 
Fidel anazuga tu hapa ili apate michango mingi zaidi kuthibitisha dhana yake!Hajui cha dawa wala nini huyu!

wewe WOS upo tayari kupokea mke mwenza na ukaishi naye nyumba moja?
Njoo mtaani kwetu uone na huyu mzee anasifika kwa mizizi kwa hiyo kamnyamazisha mke wake kwa kizizi haongei kitu mke mkubwa zaidi ya heshima tu.
 
Mwana mi naamini kwa kiasi kikubwa miti shamba ina nguvu sana katika mapenzi nakwambia mi naweza nikamlisha kitu mchumba angu nikawa nakuja na nyumba ndogo na asiulize kitu chochote.

Fidel hadithi yako ya huyo shwahiba wako alokuwa ametengenezewa bikra ya lazima hukushawishika kujaribu kumzibua kabla hujamshauri aende kwa dada kondoa?

Ni sawa Fidel but kuna raha gani ukiwa unajua kabisa niko na MwanajamiiOne kwa nguvu ya dawa? Haina maana bwana labda kama nia yako ni kumkomoa mtu na kujichumia dhambi tu.
 
Hakuna cha kukomoana wala nini. Hizi dawa hazifanyi kazi na hazipo. Ni uongo na uzushi tuu. Ni sawa na kule wanakowang'oa meno watoto wachanga eti ni meno ya plastiki. Huu ni uongo tuu
 
Fidel hadithi yako ya huyo shwahiba wako alokuwa ametengenezewa bikra ya lazima hukushawishika kujaribu kumzibua kabla hujamshauri aende kwa dada kondoa?

Ni sawa Fidel but kuna raha gani ukiwa unajua kabisa niko na MwanajamiiOne kwa nguvu ya dawa? Haina maana bwana labda kama nia yako ni kumkomoa mtu na kujichumia dhambi tu.

Mwana huyu alizibwa na jamaa asitoke nje ya ndoa ikabidi ndugu wamzibue.
Lakini si nitakuwa nimetimiza lengo langu la kuwa na wewe na kufrahi na kufrahika jamani Mwana...
 
Mkuu na wanaume wanao nyanyaswa na wake zao tuiite mfumo jike nao?

Dume means musculinity. Kwa hiyo mfumo dume ni mfumo unaotawala kwa kutumia musculinity. Ikiwa mwanamke anamfanyia mumewe kama midume inavyowafanyia wanawake, naye anatumia musculinity. Hivyo anampelekesha mume wake kidume dume. Bado anaendesha mfumo dume ingawa ni mwanamke. Mfumo dume hauna maana ya gender kuwa anayefanya ni mwanaume tuu. Nooo.
 
Ok nimekuelewa.
Tuje kwenye swala la miti shamba wewe unadefend kidini au kiscience?
 
Mwana huyu alizibwa na jamaa asitoke nje ya ndoa ikabidi ndugu wamzibue.
Lakini si nitakuwa nimetimiza lengo langu la kuwa na wewe na kufrahi na kufrahika jamani Mwana...

Huu wote wa kufungwa na kufunguliwa ni uwongo tuu. We ukiwa mwanaume jaribu kufanya jaribio la kumfunga mkeo. Au ukiwa mwanamke jaribu kufanya jaribio la kumfunga mumeo. Waganga utamaliza, hela utamaliza na mmeo/mkeo hatafungwa wala kufunguliwa. Utabaki kusikia stori tuu. Kila mganga atakuambia sababu ya kushindwa, mara zote lawama zitarudi kwako kwa kushindwa masharti.

Wakati mwingine utapewa masharti yasiyotekelezeka. Ukishindwa unaambia wenzio wengi tuu mbona wanaweza. Lakini ukiwatafuta hao, utapata makuadi wa waganga au waganga wengine.

Huu ni ushirikina na hausaidii chochote. Ni uongo na uzushi tuuu.
 
wewe WOS upo tayari kupokea mke mwenza na ukaishi naye nyumba moja?
Njoo mtaani kwetu uone na huyu mzee anasifika kwa mizizi kwa hiyo kamnyamazisha mke wake kwa kizizi haongei kitu mke mkubwa zaidi ya heshima tu.

Suala la nyumba ndogo usichanganye na mitala.Mitala hata kama siyo rasmi bado si sawa na nyumba ndogo.Nyumba ndogo ni kitu ingine kabisaaaaa.
 
Back
Top Bottom