Mapenzi yanapo waunganisha watu wawili na kupelekea mushkeri katika jamii

Intelligent businessman

JF-Expert Member
Sep 6, 2022
26,126
52,868
Kuna siku niliwahi kuona chapisho lililosema."Najiuliza jinsi Dr Nandipha aliweza kupenda, kuishi na kufanya mapenzi na muuaji bila kuogopa, kwa mara ya kwanza nitakubaliana na watu wasemapo ogopa wanawake"Baada ya kuona chapisho hilo nikajiuliza huyu Dr Nandipha ni nani?

Nikagundua ni mwanamke aliyezaliwa Eastern Cape katika kijiji cha Bizana South Africa, kisha akaja kukulia huko Port Edward kwazulu-natal.Dr Nandipha ni mrembo anayevutia kumtazama Na zaidi ni mwanamke aliyejiweza kipesa, anamiliki nyumba nzuri, magari ya kifahari pamoja na
clinical yake inayoitwa Optimum Medical Aesthetics Solutions.

Hapa nikajiuliza tena why alishi na kufanya mapenzi na mwanaume Mwizi, Tapeli, muuaji na mbakaji.Na hapo ndipo kiu yangu ya kutaka kufahamu nisiyoyafahamu iliongezeka.Kwanza kabisa niliona chapisho lingine!!.
kwenye mtandao likisema.."Polisi wa Tanzania wamethibitisha kumkamata Thabo Bester na Nandipha Magudumana na mtu mwingine aliyefahamika kwa jina la Zakaria Alberto"Taarifa zilisema watu hao wameshikiliwa na jeshi la polisi la Tanzania na mawasiliano baina ya nchi 2

Tanzania na South Africa yanafanyika ili watu hao warudishwe South Africa.Bado udadisi wangu wa mambo ulitaka kudadisi juu ya watu hao wawili walifikaje Tanzania na why wote waitwe wauaji.?
Niligundua watu hawa ni wapenzi, ila nikaja kushangazwa.

nilipofahamu mwanaume ambaye ni Thabo Bester alikuwa gerezani kwa takribani miaka 10 Na hata Penzi Lao, lilianza rasmi wakati mwanaume huyo yuko gerezani.Hili likanifikirisha zaidi, jinsi gani na kwanamna gani mwanamke alivutiwa na mwanaume mfungwa.

Na hapo ndipo nilipopata
Kufahamu mwanaume ambaye ni Thabo Bester alikuwa gerezani kwa takribani miaka 10Na hata Penzi Lao, lilianza rasmi wakati mwanaume huyo yuko gerezani.Hili likanifikirisha zaidi, jinsi gani na kwa namna gani mwanamke alivutiwa na mwanaume mfungwa.

Na hapo ndipo nilipopata
taarifa chache za Thabo Bester,Kwamba mwaka 2006 Thabo Bester alikutana na Nandipha magudumana katika mchezo wa Tennes na majukwaa tofauti ya maonyesho. Bester alikuwa ni mjanja mjanja alijihusisha na mitindo na uimbaji.

Ndiko kulikofanya akutane
na Nandipha mara kwa mara sababu wakati huo Nandipha pia alikuwa akijitafuta kupitia uwana mitindo.walikuwa ni wadogo urafiki wao ulianzaia hapoMaisha yaliendelea huku Bester akiwa ni kijana wa mtaani tu! Asiye na kazi wala uhakika wa kula milo mi3, kuishi kwake hata kusoma kwake kuli tegemea juhudi zake.

Ni kijana aliyetelekezwa na wazazi wake kwa kuachwa na bibi yake, lakini bibi pia alikuwa ni mlevi wa kutupwa.Alijikuza mwenyewe, hakukuwa na mtu wa kumwambia ili fanya lile usifanye, yeye alifanya chochote ili mkono uende kinywani.

Alikuwa ni tapel katika mitaa ya Durban na Cap Town, vijana wenzake wakamuita chokolaa Mwaka 2009 Thabo Bester alikamatwa kwa tuhuma za utapeli na alihukumiwa miaka Miwili jera.Akiwa jera alipitia maswahibu mazito, alibakwa na kundi la wafungwa kisha akaingiziwa chupa sehemu ya haja kubwa.

Watu hao walidai Bester ana mali kwenye mwili wake ivyo walimlazimisha azitoe Baada ya tukio hilo Bester alipeleka malalamiko mahakamani.

Kwamba huko jera wafungwa kadhaa humfanyia mchezo mchafu, lakini mahakama haikutaka kusikiliza malalamiko hayo.

ikatupilia mbali mashtaka na kumuacha Bester aendelee kusota hapo jera.
Hakikupita kipindi jamaa zake aliofahamiana nao walikuja na kumtoa.Thabo Bester akarejea tena uraiani.
Akiwa uraiani akili na mawazo yake yote yaliwaza pesa, jamaa zake wakampa dili mbalimbali za kuiba vitu vya samani.

Anamuonekano mzuri "Body Language" hata jamaa zake waliliona hilo, walimtumia kuwalaghai wanawake.

Aliijua vyema mitandao ya kijamii Aliitumia hiyo kujiingizia mamilioni ya pesa, mtandao aliokuwa akipenda kuutumia ni Facebook.

ndani ya mtandao huo alitapeli makundi ya wanawake.

Aliijua miji mingi ya South Africa, miji mikubwa na maarufu alikuwa na nyumba hapo au pango kwa ajili ya kufanya kazi zake za kitapeli.

Mwaka 2011 mwezi wa7 Thabo Bester alijitambulisha kama mtu anayetokea kwenye kampuni ya kuandaa matamasha ya mitindo, aliwafanyia usahili wanawake wengi ambao walilazimika kulipia pesa za usahili.

Akiwa anatumia jina la Tom kelly, alikodi mabasi mawili na kwenda Cap Town ndani ya mabasi hayo kulikuwa na warembo aliotoka nao Johannesburg.

Kulikuwa na wapiga picha waliokuwa na vifaa vyao vya kazi, safari hii ya kwenda Cap Town ilikuwa ni yakwenda kuwapiga picha warembo hao ambao tayari walisha lipia pesa za usahili wa awali na pesa za upigaji picha.

Walipofika Cap Town, Bester alilipia chakula cha mchana na kuandaa kikao kifupi.

Akawataka wapiga picha wake pamoja na warembo waache vitu vyao vyote kwenye mabasi kwa sababu za kiusalama.

Thabo Bester ambaye sasa alifahamika kama Tom Kelly, aliwatuma vijana wake wakaiba vitu vyote vilivyopo kwenye mabasi hayo.

Kisha yeye akawa wa kwanza kwenda kuripoti polisi kuwa wameibiwa mali zao na vifaa vyao hivyo.

Kati ya warembo hao alikuwepo pia Nandipha Magudumana ambaye Wakati huo tayari alikuwa anasoma chuo na huku akiendelea kufanya uwana mitindo.

FwkQoxlWIAAgJ0n.jpeg
FwkQpH0XoAAyQhB.jpeg

I will be back, I mean no malice to nobody

Salute to wisdom,
 
Back
Top Bottom