Horseshoe Arch
JF-Expert Member
- Aug 10, 2009
- 13,139
- 12,284
Baada ya kila kitu kukamilika ndipo tutajua la kufanya...watu tupo makini, hawawezi kucheza na rasilimali zetu kiasi hiki...
January alishaonyesha njia, na ujio wa mwarabu ndiyo hivyo tena. Mkataba huo utakuwa siri ili wachache waneemeke! Kufa kufaana wakuu,
Waziri Mkuu Mizengo Pinda leo ametamka rasmi kuwa TANESCO itaingia mkataba mpya na Dowans wa kuzalisha umeme.
Amesema mitambo ya Dowans itawashwa muda wowote kuanzia sasa licha ya kesi iliyopo mahakamani kuhusu tozo ya ICC.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuhutubia mkutano ulioandaliwa na The Economist kwenye hoteli ya Kempinski jijini Dar es Salaam, Pinda alisema kuwa ni vyema SONGAS au kampuni nyingine binafsi inakununua mitambo ya Dowans siku zijazo ili iendelee kuzalisha umeme nchini.
Alisema hivi sasa kuna upungufu wa 160MW kwenye gridi, hivyo 100MW ya Dowans ingesaidia kupunguza makali ya mgao.
Pinda alisema serikali kununua mitambo ya Dowans imeleta maneno mengi kuwa haiwezekani serikali ikanunua mitambo iliyotumika, hivyo ameona suluhisho ni kwa SONGAS au mfanyabiashara mwingine mkubwa anunue mitambo ya Dowans na aingie kwenye mkataba wa muda mrefu na TANESCO wa kuzalisha umeme.
Tayari Baraza la Mawaziri limetoa kibali kwa TANESCO kuingia mikataba ya kukodi umeme kama ya Richmond/Dowans ili kupata 260MW.
Sasa hivi inasubiriwa bodi ya wakurugenzi ya TANESCO itoe tamko rasmi kuwa serikali itaingia mkataba mpya na DOwans.
Kweli mafisadi wa Dowans wataendelea kupora pesa za wavuja jasho wa Tanzania!
Kuwasha mitambo ya Downs ni sawasawa na Mkeo kufile kesi ya divorce mahakamani halafu anaendelea kulala na mumewe kabla kesi haijawa finalised
kuhusu ule mzigo ndo wamesamehe au?du kama bado wanatudai kweli sisi shamba la bibi kwani ule mzigo c watosha kuagiza kamtambo kapya/WADAU HEBU NI JUZENI
Yaliyotokea Misri,Tunisia na Libya sio bahati mbaya! Na walioandama ni binadamu kama sisi, ila tunazidiana uvumilivu tu!Waziri Mkuu Mizengo Pinda leo ametamka rasmi kuwa TANESCO itaingia mkataba mpya na Dowans wa kuzalisha umeme.
Amesema mitambo ya Dowans itawashwa muda wowote kuanzia sasa licha ya kesi iliyopo mahakamani kuhusu tozo ya ICC.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuhutubia mkutano ulioandaliwa na The Economist kwenye hoteli ya Kempinski jijini Dar es Salaam, Pinda alisema kuwa ni vyema SONGAS au kampuni nyingine binafsi inakununua mitambo ya Dowans siku zijazo ili iendelee kuzalisha umeme nchini.
Alisema hivi sasa kuna upungufu wa 160MW kwenye gridi, hivyo 100MW ya Dowans ingesaidia kupunguza makali ya mgao.
Pinda alisema serikali kununua mitambo ya Dowans imeleta maneno mengi kuwa haiwezekani serikali ikanunua mitambo iliyotumika, hivyo ameona suluhisho ni kwa SONGAS au mfanyabiashara mwingine mkubwa anunue mitambo ya Dowans na aingie kwenye mkataba wa muda mrefu na TANESCO wa kuzalisha umeme.
Tayari Baraza la Mawaziri limetoa kibali kwa TANESCO kuingia mikataba ya kukodi umeme kama ya Richmond/Dowans ili kupata 260MW.
Sasa hivi inasubiriwa bodi ya wakurugenzi ya TANESCO itoe tamko rasmi kuwa serikali itaingia mkataba mpya na DOwans.
Kweli mafisadi wa Dowans wataendelea kupora pesa za wavuja jasho wa Tanzania!
duu mitambo kuwashwa???hivi hawa viongozi wetu wameletwa na nani???JAMANI NISIDIENI JE HUU SI UTAWALA WA SHETANI??????
Nilisema kule nyuma, na ninasema tena, sio tuu tumeingia mkataba mpya, hata deni tutalipa!.
tufwile nnyambalaDaaaaa kweli tufwile! , tosue mweeee!
Kama kweli nyie wazalendo basi mjue kuna zaidi ya Dowans inanitia shaka nadhani kuna kitu kwenye hii Dowans ndio maana ikitajwa wote mnaruka uwiiiii, jamani tumevamiwa na longo longo jingiiiii hamjengi haja za msingi kwanini Dowans isiwasheshwe. Pengine hamfahamu kuwa IPTL yenye mkataba wa miaka 20 ndio ni kampuni ya kufua umeme ghali maradufu ya Dowans mbona yenyewe mmeinyamazia? au yenyewe haikuingia mkataba na tenesco kwa kutumia hila? Sisi wananchi lazima tuwe na upeo wa kujiuliza mambo tusikurupushwe na wanasiasa kisha tukawa tunaitikia viitikio vyao.
Umeme wa Dowans lazima uwashwe ili kuwapunguzia makali wananchi! utasaidia kuongeza production viwandani! sioni tatizo la kuwashwa mitambo ya Dowans ikiwa maslahi ya taifa yataangaliwa upya katika huo mkataba mpya. Sitapenda kulalama na kuropoka mpaka pale nitakapojua IPTL, AGGREKO na SONGAS WASAFI kiasi gani.......
My take.
Tuache ushabiki wa kishamba tuchambue hoja ili kujenga hoja...............
sina la kuongezaHuu ni ushindi mnono kwa mafisadi. Inasikitisha sana! Pinda alishasema hawa watu ni hatari, na kweli tunaona.
Wamefanikiwa kumweka Makinda, then January na agenda zao sasa zinasonga mbele. Wamefanikiwa kuliondoa suala hili katika baraza la mawaziri kuwakwepa wapambanaji na kutwika mzigo TANESCO, Wamefanikiwa.
Wamemleta Tapeli ili kuficha mmiliki halisi,wamefanikiwa.
RA alikana kuijua Dowans na Al adawi alikana kuijua Dowans, leo wameweza kuiteka serikali na kuifanya ikubaliane na kila wanachosema, serikali ifanye kama wanavyotaka tena kwa masharti yao. Tunajua Dowans ni zao haramu la Richmond, kuingia nao mkataba ni kukana mimba na kukubali mtoto. Nchi ina wenyewe sisi wananchi tuna bendera, pesa inanunua kila kitu, next ni mnada wa roho zetu.
Kwa hili la Dowans ninahakika hata shetani anaona aibu akilisikia.
so sad.
duh,nimekukubali kaka hii sikujua unajua humu kuna magreat thinker lakni sio.mi mgeni humu ila nishajua kuna jamaa humu wana lao jambo tu na sivingine na wengi wako majuu yani oovyo hasa
duh,nimekukubali kaka hii sikujua unajua humu kuna magreat thinker lakni sio.mi mgeni humu ila nishajua kuna jamaa humu wana lao jambo tu na sivingine na wengi wako majuu yani oovyo hasa