Mitambo ya Dowans sasa kuwashwa - Waziri Mkuu Pinda

Waziri Mkuu Mizengo Pinda leo ametamka rasmi kuwa TANESCO itaingia mkataba mpya na Dowans wa kuzalisha umeme.

Amesema mitambo ya Dowans itawashwa muda wowote kuanzia sasa licha ya kesi iliyopo mahakamani kuhusu tozo ya ICC.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuhutubia mkutano ulioandaliwa na The Economist kwenye hoteli ya Kempinski jijini Dar es Salaam, Pinda alisema kuwa ni vyema SONGAS au kampuni nyingine binafsi inakununua mitambo ya Dowans siku zijazo ili iendelee kuzalisha umeme nchini.

Alisema hivi sasa kuna upungufu wa 160MW kwenye gridi, hivyo 100MW ya Dowans ingesaidia kupunguza makali ya mgao.

Pinda alisema serikali kununua mitambo ya Dowans imeleta maneno mengi kuwa haiwezekani serikali ikanunua mitambo iliyotumika, hivyo ameona suluhisho ni kwa SONGAS au mfanyabiashara mwingine mkubwa anunue mitambo ya Dowans na aingie kwenye mkataba wa muda mrefu na TANESCO wa kuzalisha umeme.

Tayari Baraza la Mawaziri limetoa kibali kwa TANESCO kuingia mikataba ya kukodi umeme kama ya Richmond/Dowans ili kupata 260MW.

Sasa hivi inasubiriwa bodi ya wakurugenzi ya TANESCO itoe tamko rasmi kuwa serikali itaingia mkataba mpya na DOwans.

Kweli mafisadi wa Dowans wataendelea kupora pesa za wavuja jasho wa Tanzania!

Wanaofahamu kama Mh. Sitta na Mwakyembe wameridhia haya maamuzi watujuze. Au maamuzi yataishia kwenye Bodi ya Tanesco ili kuwakwepa hawa wapambanaji kwenye Baraza la Mawaziri?
 
Kuna tatizo la msingi kwanini wengi wanapinga majenereta ya Dowans yasiwashwe. Tatizo ni hili Dowans ni kampuni hewa au tuseme hivi haijathibitishwa kama ni kampuni ambayo inaaminika. Kwa msingi huo Serikali haitakiwi kufanya biashara na kampuni za namna hii.

Raisi wa nchi alisema hawajuhi wenye Dowans na leo mnauliza kwanini watu tunalalamika? Kama serikali ina nia ya kweli kuhusu tatizo la umeme wasingeshindwa kununua majenereta kwa muda wote huu. Kama kuna kosa linafanywa lazima tuseme na tukemee kosa haliwezi kusubiri kujua kama mengine nayo yana makosa. Ndio kuna haja ya kufuatilia IPTL, SONGAS na wengine lakini isiwe sababu ya kunyamaza kuhusu Dowans.
 
Kama kweli nyie wazalendo basi mjue kuna zaidi ya Dowans inanitia shaka nadhani kuna kitu kwenye hii Dowans ndio maana ikitajwa wote mnaruka uwiiiii, jamani tumevamiwa na longo longo jingiiiii hamjengi haja za msingi kwanini Dowans isiwasheshwe. Pengine hamfahamu kuwa IPTL yenye mkataba wa miaka 20 ndio ni kampuni ya kufua umeme ghali maradufu ya Dowans mbona yenyewe mmeinyamazia? au yenyewe haikuingia mkataba na tenesco kwa kutumia hila? Sisi wananchi lazima tuwe na upeo wa kujiuliza mambo tusikurupushwe na wanasiasa kisha tukawa tunaitikia viitikio vyao.

Umeme wa Dowans lazima uwashwe ili kuwapunguzia makali wananchi! utasaidia kuongeza production viwandani! sioni tatizo la kuwashwa mitambo ya Dowans ikiwa maslahi ya taifa yataangaliwa upya katika huo mkataba mpya. Sitapenda kulalama na kuropoka mpaka pale nitakapojua IPTL, AGGREKO na SONGAS WASAFI kiasi gani.......

My take.

Tuache ushabiki wa kishamba tuchambue hoja ili kujenga hoja...............

Bora wewe kaka. Kubali yaishe, ila usije ukawa unatetea udini!!!!!!!!!!!!!!!!!!!. Ndugu yangu umeshindwa kuona uozo huu, eti kuna maslai ya Taifa. Iweje wanadai na huku kukiwa na wasiwasi wa kulipwa tena wakubali kuingia mkataba mwingine.

Baba Pinda, Mhe. kuna haja gani ya kununua mitambo hii wakati mmiliki wake ni mwenzetu. Au ameseme hataki kuingia mkataba tena. Tatizo lenu ni kuficha mwenye mitamba wakati hanajulikana!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Hawajui wananchi wakishachukua nchi hizo pesa za ufisadi zitakuwa frozen baada ya revolution?Hata assets zao zitakuwa frozen kwasababu ni jasho la wananchi,hawa watu hawajui dunia imebadilika...Yani very out of touch,they dont connect with the people for they dont live the same world!

Wanadhani wananchi bado ni wajinga,nani alisema mitambo ya Dowans haiwashiki?We both knew that mitambo ya Dowans ni mizima na kuna watu miongoni mwao baadhi ya wanasiasa wetu ambao wanataka mitambi hiyo iwashwe,si kwasababu wanauchungu na shida ya watanzania bali ether wametumwa na wenye mitambo hiyo ama wana maslahi na uwashwaji wa mitambo hiyo,tatizo si mitambo,bali tatizo ni uwazi wa mikataba ya mitambo hiyo ambayo iliwahi kumilikiwa na kampuni hewa!

watawala watumie akili kwasababu wananchi wanataka uwajibishwaji wa viongozi wote ambao wamelisababishia Taifa hasara kutokana na mikataba hiyo,wananchi wanajua mitambo hiyo iko ila kabla haijawashwa,wanataka kujua itawacost kiasi gani,na pia kama wanatakiwa waendelee kulipa fidia za mitambo hiyo kuwa chini na wakati viongozi waliofanya hayo madudu bado wako madarakani na wengine ndio wenye kampuni,sasa ni kama wanatoa pesa mfuko wa kushoto na kuhamishia wa kulia.
 
Du Mhe. Pinda, Vipi boss wako umemjulisha nani mwenye mtambo!. Au umeamua kuingizwa mkenge. Kama Raisi hatambui wamiliki iweje tusaini mkataba tena!!!!!
 
Safi sana Pinda!

Kila binadamu mwenye akili timamu lazima apende kuwa na "mchango kwenye jamii & heshima ya kutambulika pia" - "meaning & contribution" - LEGACY!

Kwa hili Pinda you will be remembered, my brother!
The Following User Says Thank You to Kyabushaija For This Useful Post:
Teamo (Today)

aisee vipi?
leo bia tunakunywa?
 
Utamkumbuka wewe peke yako

Safi sana Pinda!

Kila binadamu mwenye akili timamu lazima apende kuwa na "mchango kwenye jamii & heshima ya kutambulika pia" - "meaning & contribution" - LEGACY!

Kwa hili Pinda you will be remembered, my brother!
 
Wamechelewa kama uwamuzi ndo huo walipaswa kufanya maamuzi muda mrefu.
 
Are the following mere coincidences??

1: The Chairman of Parliamentary Energy and Minerals (January Makamba) not only represents Bumbuli but Chairs same Committee previously headed by his predecessor in Bumbuli. Noteworthy, Richmonduli saga
2: There is an imminent water shortage at Mtera again in 2011 and that as of todate no CONTINGENCY MEASURES ARE IN PLACE to address chronic power shortage
3: Masquearding as DOWANS owner, an OMANI who is said to be a Zanzibari and a close buddy of our very own RA SHOWS up in Tanzania just as the POWER BLUES TAKE A HARDER BITE
4: All forces are unleashed in order to tap the 100 MW Dowans power into tour grid while other zimamoto attempts are approved to get newer Richmonds
5: Vasco da Gama then jets-off!!
 
Nilijua commedy hiyo itaendelea kudumu na kudumu na kudumu, maana wenye dowans ni haohao walioshika rungu la serikali. Mkono wa kulia kamwe hauwezi kwa makusudi ukakikata kichwa cha aliyeubeba mkono huo isipokuwa akili zimeruka juu.
 
Kama kweli nyie wazalendo basi mjue kuna zaidi ya Dowans inanitia shaka nadhani kuna kitu kwenye hii Dowans ndio maana ikitajwa wote mnaruka uwiiiii, jamani tumevamiwa na longo longo jingiiiii hamjengi haja za msingi kwanini Dowans isiwasheshwe. Pengine hamfahamu kuwa IPTL yenye mkataba wa miaka 20 ndio ni kampuni ya kufua umeme ghali maradufu ya Dowans mbona yenyewe mmeinyamazia? au yenyewe haikuingia mkataba na tenesco kwa kutumia hila? Sisi wananchi lazima tuwe na upeo wa kujiuliza mambo tusikurupushwe na wanasiasa kisha tukawa tunaitikia viitikio vyao.

Umeme wa Dowans lazima uwashwe ili kuwapunguzia makali wananchi! utasaidia kuongeza production viwandani! sioni tatizo la kuwashwa mitambo ya Dowans ikiwa maslahi ya taifa yataangaliwa upya katika huo mkataba mpya. Sitapenda kulalama na kuropoka mpaka pale nitakapojua IPTL, AGGREKO na SONGAS WASAFI kiasi gani.......

My take.

Tuache ushabiki wa kishamba tuchambue hoja ili kujenga hoja...............

Kuwasha mitambo ya Downs ni sawasawa na Mkeo kufile kesi ya divorce mahakamani halafu anaendelea kulala na mumewe kabla kesi haijawa finalised
 
Du! Kweli sisi mbumbu wa mambo ya uchumi... yaani hilo nalo tatizo na wanasiasa wakombozi kama CHADEMA hawaoni ni vyema kupata 100MW kunusuru uchumi kuliko kupiga makelele yasiokuwa na maana kweli taifa limetekwa.
 
..kwanini Tanesco hawanunui mitambo yao wenyewe toka kwa watengenezaji wa mitambo ya umeme?

..kuna kila dalili kwamba kuna HUJUMA inaendelea ktk sekta ya nishati na madini.

NB:

..kuna suala lingine la uagizaji[bulk importation] mafuta ambapo ilipendekezwa TPDC[serikali] ndiyo wafanye shughuli hiyo. ghafla tukasikia Ngeleja amewabadilishia kibao.
 
Kasheshe said:
Du! Kweli sisi mbumbu wa mambo ya uchumi... yaani hilo nalo tatizo na wanasiasa wakombozi kama CHADEMA hawaoni ni vyema kupata 100MW kunusuru uchumi kuliko kupiga makelele yasiokuwa na maana kweli taifa limetekwa.

Kasheshe,

..kaka, hili tatizo ni la kutengenezwa.

..muda wote wahusika hawakuchukua hatua za kutunusuru wananchi kufika ktk hali hii ya uhaba wa umeme.
 
Kasheshe,

..kaka, hili tatizo ni la kutengenezwa.

..muda wote wahusika hawakuchukua hatua za kutunusuru wananchi kufika ktk hali hii ya uhaba wa umeme.

Kwa kweli mimi sio muumini wa miujiza.... I can see everything openly! Kwamba mabwawa yanaelekea kukauka... hilo nalo uongo? kwamba Songas ilipata hitilafu ya mitambo yake.... amkeni Watanzania... angalieni vitu kwa mapana zaidi.
 
wananchi tulikuwa tunadiscuss kuhusu kulipwa kwa DOWANS au wasilipwe....hatukudiscuss kama mitambo iwashwe tena au isiwashwe.......sasa issue ni kulipa au kuwasha?
 
remembered for what?
Safi sana Pinda!

Kila binadamu mwenye akili timamu lazima apende kuwa na "mchango kwenye jamii & heshima ya kutambulika pia" - "meaning & contribution" - LEGACY!

Kwa hili Pinda you will be remembered, my brother!
 
Kwa kweli mimi sio muumini wa miujiza.... I can see everything openly! Kwamba mabwawa yanaelekea kukauka... hilo nalo uongo? kwamba Songas ilipata hitilafu ya mitambo yake.... amkeni Watanzania... angalieni vitu kwa mapana zaidi.
hapa bado kuna kitu kinapikwa zaidi ya hicho..
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom