Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 13,504
- 51,099
Kwa miaka mingi Misri imekuwa ikidai kuwa ina haki ya kuingilia matumizi ya maji ya ziwa Victoria kwa nchi ambazo zipo katika chanzo cha ziwa hilo, hii ni kutokana na mkataba wa kikoloni ambao Misri iliingia na Waingereza na kuwapa haki kubwa sana ya maji yatiririkayo kwenda katika nchi ambayo yatokayo huku Afrika mashariki na Ethiopia.
Kwa miaka mingi Misri imekuwa ikifanya figisu kila mara tulipokuwa tukionyesha jitihada za kuyatumia maji ya ziwa victoria kwa kiwango kikubwa kujinyanyua.
Jitihada zetu za kuushinda ubabe huu wa misri zilitupelekea kuunnganisha nguvu na nchi za Ukanda huu wa Afrika mashariki kutangaza kwamba hatukubali madai ya Misri.
Katika Ukanda huu sisi ndiyo wakubwa zaidi kieneo, na kwa idadi ya watu na pia kwa asilimia za umiliki wa ziwa victoria
Kwa sasa nchi yetu imepambwa na maji kila kona lakini yana mgogoro, Ziwa Victoria hatuna uhuru nalo ipasavyo, Ziwa Nyasa tuna mgogoro na Malawi, Kule baharini tuombee Muungano udumu maana ukilegea Wazanzibari watadai bahari kuu. Tukichezea urithi wa Maji tutajikuta sisi ni watu tuliozunguukwa na maji lakini yana wenyewe
WIZARA YA MAMBO YA NJE TUNAOMBA MAJIBU!
TUELEZENI, JE DIPLOMASIA YETU JUU YA KUTETEA RASILIMALI ZIWA VICTORIA IMESIMAMIA WAPI BAADA YA WALE TUNAOGOMBANA NAO KATIKA HILO SUALA YAANI WAMISRI KUTUSAIDIA KWENYE STIEGLERS?

- Swali ninalojiuliza na ningependa kufahamu je Wamisri kutujengea Stieglers kumeambatana na sisi kuwapa Concenssions zozote juu ya haki ya maji ya ziwa victoria?
- Je kwa Msaada huu wa kujengewa Stieglers, uwezo wetu wa kidiplomasia wa kuongoza nguvu na Juhudi za kuukataa mkataba wa kikoloni uliowapa wamisri haki juu ya Ziwa victoria utakuwaje?
- Yameshatolewa madai mbalimbali humu JF kuwa Misri inawapa kitu kidogo baadhi ya watu potential ili kukwamisha juhudi zetu za kuclaim haki ya kutumia maji ya ziwa victoria , je serikali inatuleza nini?
- Hiyo habari ipo hapa: Kuna viongozi wanaolipwa na serikali ya Misri ili tusitumie maji ya ziwa Victoria - JamiiForums