Victor Mlaki
JF-Expert Member
- May 1, 2016
- 3,564
- 3,472
Chama Cha Mapinduzi ( CCM) ni chama kilichopitia changamoto nyingi nyingi na zinazoweza kuhatarisha uwepo wake kama chama tawala lakini licha ya changamoto hizo kimeweza kustahimili kutokana na sababu kadhaa nje ya ukongwe wake au uzoefu.
Moja ya sababu kubwa ni Misingi ya ujamaa ambayo CCM iliirithi kutoka kwenye Katiba ya TANU. Misingi hiyo ni:
(a) Usawa-Binadamu wote ni sawa.
(b)Heshima-Kila mtu anahitaji heshima.
(c) Ushiriki-Kila raia ni sehemu ya Taifa na anayo haki ya kushiriki sawa na wengine katika Serikali tangu ya Mitaa, Mikoa hadi Serikali Kuu.
(d) Uhuru wa kutoa mawazo-Kila mtu anayo haki ya uhuru wa kutoa mawazo yake, kwenda anakotaka na kuamini dini anayotaka, kukutana na watu ili mradi havunji sharia.
(e) Kupata hifadhi ya maisha na mali kwa mujibu wa sheria.
(f) Malipo ya haki-Kila mtu anastahili malipo ya haki kutokana na kazi yake.
(g) Kumiliki utajiri wa asili wa nchi kama dhamana kwa vizazi vijavyo.
(h) Kuhakikisha uchumi wa nchi unakwenda sawa- Serikali lazima iwe na mamlaka na mamlaka kamili juu ya njia muhimu za kukuza uchumi; na
(i) Kwamba ni wajibu wa Serikali ambayo ni watu wenyewe, kuingilia kazi kwa vitendo maisha ya uchumi wa Taifa ili kuhakikisha usitawi wa raia wote na kuzuia mtu kumnyonya mtu mwingine au kikundi kimoja kunyonya kikundi kingine na kuzuia limbikizo la utajiri kusikia kiasi ambacho hakipatikani na sasa ya watu wote kuwa sawa.
Misingi hiyo ndiyo misingi ya Utu na Utangamano wa Kitaifa pia ni raslimali muhimu kwenye Umajumui wa Afrika chini ya falsafa ya Kiafrika yaani UBUNTU.
Misingi hiyo ndiyo kigezo mkubwa cha ufanisi wa Chama na ndiyo inayotumiwa na wakosoaji kuonesha udhaifu.