Leo ni tarehe 30 July 2009,na hakuna dalili yeyote kwamba wafanyakazi wa serikali watapata mishahara yao.Mitaani tunasikia wafanyakazi wa serikali kuu wakiilalamikia serikali yao katika kiwango cha kutisha sana.
Tunacho hoji ni kwamba inakuwaje maagiza ya Rais yanakiukwa bila hata wafanyakazi husika kupewa taarifa yeyote?Itakumbukwa kwamba Rais alishaagiza ifikapo tarehe 23 ya kila mwezi wafanyakazi wawe wameshapata mishahara yao.Akaongeza kwamba kama itakuwa lazima kucheweshewa mishahara yao,basi isizidi tarehe 25 ya kila mwezi.
Ikumbukwe kwamba mishahara ya wafanyakazi wa serikali ni midogo mno,na kwa sababu hiyo wengi wao hawana njia nyingine yeyote ya kujipatia kipato.Kwahiyo wakicheleweshewa mishahara athari ina kuwa kubwa sana kwa wao wenyewe na wale wote wanao wategemea.
Tunaiomba serikali iwe makini zaidi katika swala hili ili kuwaepushia wafanyakazi usumbufu usio wa lazima.Tunaelewa fika kwamba kuna uzembe katika swala hili,kwa hiyo wale wote wanaochelewesha mishahara aidha kwa makusudi au kwa uzembe,wachukuliwe hatua kali za kinidhamu zinazostahili.
Mungu wabariki wafanyakazi wa Tanzania na naomba uwape nguvu ya kuendelea mbele hata katika mazingira yao magumu.